Elections 2010 Yaelekea mtandao wa kifisadi hapa nchini hauna mratibu....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Hebu tujiulize sakata la Mhe. Samweli Sitta na jinsi CC ya CCM ilivyojikanyaga hapo................Sasa tuna ushahidi ya kuwa CC ilikuwa na donge zito dhidi ya Mhe. Sitta na kauli za Makamba, Chenge, Kingunge na makada wa CCM wengineo wengi zathibitisha hayo..................hawa wote na wenziwao wamekuwa wakimlaumu Mhe. Sitta kwa jinsi alivyoruhusu mijadala bungeni ya ufisadi ambayo sasa CCM ndiyo imemshika mchawi wa kusababisha wananchi kwa ujumla kukichukia chama chao..........na kwa mantiki hiyo hiyo kuijenga Chadema..........wako ambao wamechukia Mhe. Sitta kwa kuhamasisha na kufadhili chama cha CCJ pamoja ya kuwa hapo hatuna ushahidi wa kuwa kweli alifanya hivyo.........lakini siasa always is a game of perceptions.......................

Wapo ambao donge lao dhidi ya Mhe. Sitta ni kuhusu mjadala wa Richmond na jinsi ulivyositisha malengo ya kisiasa ya baadhi ya vinara ndani ya CCM...................

Kundi hili lina chuki dhidi ya Sitta kwa kukataa mitambo ya Dowans isinunuliwe na Tanesco....Sitta alisisitiza ya kuwa utaratibu wa kununua mitumba na bila ya ushindani ni ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ambayo Bunge hilo lilipitisha..........

Kama mtandao wa kifisadi ungelikuwa na mratibu ungelijipanga kumshinikiza Mhe. Sitta asigombee ili kumnyima nafasi ya kujipatia simanzi tele ambayo hivi sasa amejinyakulia kutoka kwenye jamii..........

Sababu hizo hizo za kuwainua akina mama ingawaje kwa kubeza demokrasia wangelimpa Mhe. Sitta au hata kutangaza ya kuwa wanaoruhusiwa kuchukua fomu za kugombea uspika au wenye sifa safari hii ni wanawake tu ili kuondoa utapeli uliojitokeza wa CCM kuchukua hela za wanaume kumbe safari hii hawana hata sifa za kugombea Uspika!!!!!!!!!!!!...............

Kila mgombea alilipia fomu shs laki tano na hiyo siyo hela ya mchezo.......Mwishowe kumweleza kumbe alikuwa hana sifa na hela humrudishii ni utapeli wa kimataifa huo....na ni dhuluma za waziwazi kabisa...

Kwa kumdhalilisha Mhe. Sitta kumemletea kizaazaa hata Mhe. Anne Makinda sasa aonekana ni zao la mafisadi kwa sababu yeye pamoja na kuwa alikuwa ni Naibu Spika wa Mhe. Sitta haonekani kuwa alikuwa ni kikwazo kwa mafisadi ambao wamekuwa mstari wa mbele hata kutoficha ghadhabu zao dhidi ya Mhe. Sitta hadharani.....................Ama kweli mafisadi ni bora liende tu.................hawana hata mratibu wa shughuli zao na hata kama wanaye basi anapwaya ile mbaya............Hivyo basi hawa mafisadi tusiwaogope ni saizi yetu tupambane nao mpaka watakaposalimu amri wao wenyewe.....
 
It is too early for me to say anything as my conclusion.
Hata hivyo siwezi kusahau kwamba hata Sita naye ni fisadi mdogo.
Sasa anaminywa na Mafisai Wakubwa sisi tulofisadiwa eti tunatakiwa kumwonea Huruma??
Waacheni wafu wawazike wafu wao.

Ukiiba Iba sana ukiiba kidogo unaminywa mbavu.
 
Hata hivyo siwezi kusahau kwamba hata Sita naye ni fisadi mdogo.​

Ufisadi mdogo wa Mhe. Sitta ni upi? Uwe ule ambao umethibitishwa siyo ule ambao ni gumzo huko mitaani........
 
Mi naona CCM hawajakosea Kumpa MH. Anna Makinda uspika kwa sababu wamefanya hivi ili kuua makundi ambayo yalikuwa tayali yameshajitokeza kati Mh 6 na Mh Vijisent hapo Mjini Dodoma maana kila mtu alikuwa na kundi lake ndani ya bunge. Hivyo CC wakaona wawapige chini wote halafu wapitishe watu ambao hawana makundi kabisa ndani ya bunge, hivyo hii imewasaidia kutopoteza kiti hicho kwa CHADEMA kwani kama angesimama Mh 6 au Chenge basi kuna kura ambazo ziingepotea kutoka kwa wabunge wa CCM na kwenda kwa CHADEMA kutokana na makundi ambayo tayali yalikuwa yameundwa ndani wakati wa kampeini za uspika.
 
Hivi kweli tumesahau alivyokuwa anatetea posho mbili mbili za wabunge? Maboresho ya malipo ya wabunge? Hata kama mnampenda alipojisahau tuseme, alikuwa fisadi tangu zamani, tatizo kwenye Richmond walimnyima 10% yake, Mbona kashfa ya EPA alimkejeli Slaa, mbona alibisha eti Elimu bure haiwezekani wakati yeye alisoma bure? mmesahau malumbano yake na Slaa wakati wa kampeni, Sitta alisema Tanzania bila JK haiwezekani
 
Juzi jiono huko Dom, Rostam Azizi aligawa 2.5 milion kwa kila mwanachama wa ccm, ili wamchague Ana, Hii inaamanisha nini?
 
Hivi kumbe CCM wizi na utapeli ni jadi yao? Sasa kama wanaume hawakutaliwa kugombea hela za form walichukua za nini? Kwa nini wasitangaze tokea mwanzo, kuwa uspika mwaka huu ni wa akinamama ili wanaume wasijihangaishe kuchukua form??
 
Hivi kweli tumesahau alivyokuwa anatetea posho mbili mbili za wabunge? Maboresho ya malipo ya wabunge? Hata kama mnampenda alipojisahau tuseme, alikuwa fisadi tangu zamani, tatizo kwenye Richmond walimnyima 10% yake, Mbona kashfa ya EPA alimkejeli Slaa, mbona alibisha eti Elimu bure haiwezekani wakati yeye alisoma bure? mmesahau malumbano yake na Slaa wakati wa kampeni, Sitta alisema Tanzania bila JK haiwezekani

Katika yote hayo yaliyotajwa sijaona ufisadi wa 6 uliothibitika.
 
Hebu tujiulize sakata la Mhe. Samweli Sitta na jinsi CC ya CCM ilivyojikanyaga hapo................Sasa tuna ushahidi ya kuwa CC ilikuwa na donge zito dhidi ya Mhe. Sitta na kauli za Makamba, Chenge, Kingunge na makada wa CCM wengineo wengi zathibitisha hayo..................hawa wote na wenziwao wamekuwa wakimlaumu Mhe. Sitta kwa jinsi alivyoruhusu mijadala bungeni ya ufisadi ambayo sasa CCM ndiyo imemshika mchawi wa kusababisha wananchi kwa ujumla kukichukia chama chao..........na kwa mantiki hiyo hiyo kuijenga Chadema..........wako ambao wamechukia Mhe. Sitta kwa kuhamasisha na kufadhili chama cha CCJ pamoja ya kuwa hapo hatuna ushahidi wa kuwa kweli alifanya hivyo.........lakini siasa always is a game of perceptions.......................

Wapo ambao donge lao dhidi ya Mhe. Sitta ni kuhusu mjadala wa Richmond na jinsi ulivyositisha malengo ya kisiasa ya baadhi ya vinara ndani ya CCM...................

Kundi hili lina chuki dhidi ya Sitta kwa kukataa mitambo ya Dowans isinunuliwe na Tanesco....Sitta alisisitiza ya kuwa utaratibu wa kununua mitumba na bila ya ushindani ni ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ambayo Bunge hilo lilipitisha..........

Kama mtandao wa kifisadi ungelikuwa na mratibu ungelijipanga kumshinikiza Mhe. Sitta asigombee ili kumnyima nafasi ya kujipatia simanzi tele ambayo hivi sasa amejinyakulia kutoka kwenye jamii..........

Sababu hizo hizo za kuwainua akina mama ingawaje kwa kubeza demokrasia wangelimpa Mhe. Sitta au hata kutangaza ya kuwa wanaoruhusiwa kuchukua fomu za kugombea uspika au wenye sifa safari hii ni wanawake tu ili kuondoa utapeli uliojitokeza wa CCM kuchukua hela za wanaume kumbe safari hii hawana hata sifa za kugombea Uspika!!!!!!!!!!!!...............

Kila mgombea alilipia fomu shs laki tano na hiyo siyo hela ya mchezo.......Mwishowe kumweleza kumbe alikuwa hana sifa na hela humrudishii ni utapeli wa kimataifa huo....na ni dhuluma za waziwazi kabisa...

Kwa kumdhalilisha Mhe. Sitta kumemletea kizaazaa hata Mhe. Anne Makinda sasa aonekana ni zao la mafisadi kwa sababu yeye pamoja na kuwa alikuwa ni Naibu Spika wa Mhe. Sitta haonekani kuwa alikuwa ni kikwazo kwa mafisadi ambao wamekuwa mstari wa mbele hata kutoficha ghadhabu zao dhidi ya Mhe. Sitta hadharani.....................Ama kweli mafisadi ni bora liende tu.................hawana hata mratibu wa shughuli zao na hata kama wanaye basi anapwaya ile mbaya............Hivyo basi hawa mafisadi tusiwaogope ni saizi yetu tupambane nao mpaka watakaposalimu amri wao wenyewe.....

Ndani ya ccm hakuna mwenye ujasiri wa kujisafisha na kinyesi cha ufisadi, kila aliye ndani ya chama hicho ni fisadi tuuu. Kuanzia mwenyekiti wa Jakaya Kikwete mpaka mjumbe wa nyumba kumi. Nasema mjumbe kwa kuwa hawa huchukua pesa ili kukupa barua ya kwenda serikali za mitaa kupata utambulisho lakini hawatoi stakabadhi kwa ajili ya malipo hayo. Mafisadi hatuna muda wa kulumbana nao tunasubiri muda ufike na utafika tu tuwaburuze mahakamani na mwisho tuwasweke kwenye magereza waliyowajengea vijana wetu waliochoshwa na ugumu wa maisha uliosababishwa na kina Lowasa hivyo nao wakaamua kujisaidia kwa kuiba simu na hereni.
 
Katika yote hayo yaliyotajwa sijaona ufisadi wa 6 uliothibitika.

Unaweza usiuone ufisadi wa Sita kama unavyoonekana ufisadi wa watu kama akina Lowasa na RA ambao wao wamepitiliza.
Utakumbuka mara baada ya Sita kuwa Spika 2005 yeye ndiye aliyepigania kwa hali na mali ili posho na mishahara ya wabunge iongezeke(tena mara dufu).
Sita ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM kamati ambayo huratibu wizi wa kura na kutumia mbinu yeyote inayowezekana kuwarudisha madarakani mafisadi.
Ukweli unabaki pale pale Sita ni fisadi mdogo na wapo mafisadi wakubwa ambao wamemfix Sita.
 
Mi naona CCM hawajakosea Kumpa MH. Anna Makinda uspika kwa sababu wamefanya hivi ili kuua makundi ambayo yalikuwa tayali yameshajitokeza kati Mh 6 na Mh Vijisent hapo Mjini Dodoma maana kila mtu alikuwa na kundi lake ndani ya bunge. Hivyo CC wakaona wawapige chini wote halafu wapitishe watu ambao hawana makundi kabisa ndani ya bunge, hivyo hii imewasaidia kutopoteza kiti hicho kwa CHADEMA kwani kama angesimama Mh 6 au Chenge basi kuna kura ambazo ziingepotea kutoka kwa wabunge wa CCM na kwenda kwa CHADEMA kutokana na makundi ambayo tayali yalikuwa yameundwa ndani wakati wa kampeini za uspika.

Tatizo la mtazamo huu ni kuwa CC hupeleka majina matatu na wala siyo moja................isingewezekana kwa wabunge wa CCm wawe wamechagua mmoja wao kati ya hayo majina matatu halafu wamtelekeze.............
 
Juzi jiono huko Dom, Rostam Azizi aligawa 2.5 milion kwa kila mwanachama wa ccm, ili wamchague Ana, Hii inaamanisha nini?

ulikuwepo au ndio ile mambo ya unaa. thibitisha kama una data kuliko kukurupuka.
 
It is too early for me to say anything as my conclusion.
Hata hivyo siwezi kusahau kwamba hata Sita naye ni fisadi mdogo.
Sasa anaminywa na Mafisai Wakubwa sisi tulofisadiwa eti tunatakiwa kumwonea Huruma??
Waacheni wafu wawazike wafu wao.

Ukiiba Iba sana ukiiba kidogo unaminywa mbavu.
mkuu umekata tamaa kama nini duu pole sana!!
 
Back
Top Bottom