Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Hebu tujiulize sakata la Mhe. Samweli Sitta na jinsi CC ya CCM ilivyojikanyaga hapo................Sasa tuna ushahidi ya kuwa CC ilikuwa na donge zito dhidi ya Mhe. Sitta na kauli za Makamba, Chenge, Kingunge na makada wa CCM wengineo wengi zathibitisha hayo..................hawa wote na wenziwao wamekuwa wakimlaumu Mhe. Sitta kwa jinsi alivyoruhusu mijadala bungeni ya ufisadi ambayo sasa CCM ndiyo imemshika mchawi wa kusababisha wananchi kwa ujumla kukichukia chama chao..........na kwa mantiki hiyo hiyo kuijenga Chadema..........wako ambao wamechukia Mhe. Sitta kwa kuhamasisha na kufadhili chama cha CCJ pamoja ya kuwa hapo hatuna ushahidi wa kuwa kweli alifanya hivyo.........lakini siasa always is a game of perceptions.......................
Wapo ambao donge lao dhidi ya Mhe. Sitta ni kuhusu mjadala wa Richmond na jinsi ulivyositisha malengo ya kisiasa ya baadhi ya vinara ndani ya CCM...................
Kundi hili lina chuki dhidi ya Sitta kwa kukataa mitambo ya Dowans isinunuliwe na Tanesco....Sitta alisisitiza ya kuwa utaratibu wa kununua mitumba na bila ya ushindani ni ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ambayo Bunge hilo lilipitisha..........
Kama mtandao wa kifisadi ungelikuwa na mratibu ungelijipanga kumshinikiza Mhe. Sitta asigombee ili kumnyima nafasi ya kujipatia simanzi tele ambayo hivi sasa amejinyakulia kutoka kwenye jamii..........
Sababu hizo hizo za kuwainua akina mama ingawaje kwa kubeza demokrasia wangelimpa Mhe. Sitta au hata kutangaza ya kuwa wanaoruhusiwa kuchukua fomu za kugombea uspika au wenye sifa safari hii ni wanawake tu ili kuondoa utapeli uliojitokeza wa CCM kuchukua hela za wanaume kumbe safari hii hawana hata sifa za kugombea Uspika!!!!!!!!!!!!...............
Kila mgombea alilipia fomu shs laki tano na hiyo siyo hela ya mchezo.......Mwishowe kumweleza kumbe alikuwa hana sifa na hela humrudishii ni utapeli wa kimataifa huo....na ni dhuluma za waziwazi kabisa...
Kwa kumdhalilisha Mhe. Sitta kumemletea kizaazaa hata Mhe. Anne Makinda sasa aonekana ni zao la mafisadi kwa sababu yeye pamoja na kuwa alikuwa ni Naibu Spika wa Mhe. Sitta haonekani kuwa alikuwa ni kikwazo kwa mafisadi ambao wamekuwa mstari wa mbele hata kutoficha ghadhabu zao dhidi ya Mhe. Sitta hadharani.....................Ama kweli mafisadi ni bora liende tu.................hawana hata mratibu wa shughuli zao na hata kama wanaye basi anapwaya ile mbaya............Hivyo basi hawa mafisadi tusiwaogope ni saizi yetu tupambane nao mpaka watakaposalimu amri wao wenyewe.....