Elections 2010 Yaelekea JK arudi ofisini lakini kwa ridhaa ya nani?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,427
911,172
JK mkakati wake wa kurudi kazini yaelekea umefanikiwa kutokana na matokeo ya awali yanayosomwa na NEC ambayo yeye mwenyewe ndiye mteule wake lakini anaelewa fika siyo chaguo la wengi na ndiyo maana ili kuyapaka mafuta ushindi wake bandia anahangaika kuhakikisha mawaziri wake tuliowakataa wanarudi.........

Tatizo kwa JK ni kudai yeye ndiye mtaji wa CCM hivyo mawaziri wake aliowachagua yeye mwenyewe hayupo tayari kuona wakidondoka kwa sababu itazua maswali mengi........hivi inakuwaje majemedari wake wameanguka na yeye amebaki beneti....................

Hii inaelezea ni kwa nini NEC imekwama kutangaza matokeo ambayo Chadema imeshinda kama Dar, Arusha, Mwanza na maeneo mengine ili kuangalia uwezekano wa kucheza mchezo mchafu............

Hii siyo demokrasia mpaka pale NEC kitakapokuwa chombo huria.......yaani hata kesho siamini JK kumshinda Dr. Slaa babati Mjini ........something must have happened there....................something despicable................
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom