Elections 2010 Yaelekea ccm inarudi madarakani kwa ridhaa ya mafisadi.........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
NI dhahiri ya kuwa CCM siyo chaguo la wapigakura wengi na wanarejeshwa madarakani na mafisadi kwa minajili ya kuendelea kuvuna ambacho hawajapanda……………………

Mbinu za mafisadi kuiwezesha CCM na haswa JK kurejea madarakani ni hizi hapa:-


  1. NEC kutokuwa na watumishi wa kudumu na hivyo kutegemea waalimu na watendaji wa serikali za mitaa katika kuratibu na kusisimamia wizi wa kura………………NEC walipaswa kuwa na wasimamizi ambao ni watumishi wao wa kudumu na ambao wanawajibika kwao moja kwa moja badala ya hawa mamluki ambao wanawajibika moja kwa moja kwa waajiriwa wao ambao baadhi yao ni wagombea ubunge au Uraisi kupitia serikali ya CCM…….haya ni mazingira ya mgongano wa kimasilahi…….na chaguzi haiwezi kuwa ya huru na haki kwenye mazingira haya………..


a)Kutokana na NEC kutokuwa na watumishi wa kudumu na hivyo kutegemea waalimu na watendaji wa serikalini ilitoa mwanya wa serikali ya CCM kufuta wagombea wa upinzani ambao walikuwa ni tishio kwa CCM na kuiba kura kila ilipowezekana wakati wa uchaguzi.......


b)Serikali ya CCM iliwahonga waalimu kwa kuwaongeza mishahara kabla tu ya uchaguzi na kuwalipa mara moja kinyume na serikali hiyo hiyo ilivyowatendea waajiriwa wake wengine…….


c)NEC ilifumbia macho serikali ya CCM iliponunua shahada za wapigakura na kupiga kura mara kwa mara isivyo halali na kinyume cha sheria.


d)NEC kwa makusudi mazima iliruhusu maboksi yenye kura haramu kuzagaa maeneo mengi na baadhi yake kukamatwa na polisi……..Huu ni uthibitisho ya uvunjaji wa sheria kwa sababu kura tayari zilikuwa zimevuja hata kabla ya uchaguzi kufanyika………..


e)NEC kughairi kuwalipa mawakala wa vyama vya siasa kinyume na makubaliano kwa malengo machafu ya kuvidhoofisha vyama vya upinzani ambavyo vina ukata na hivyo CCM kuutumia mwanya huo kuwarubuni mawakala wa upinzani…


f)NEC kuchelewesha kutangaza matokeo kwenye maeneo ambayo upinzani ilifanya vizuri kwa minajili ya kuchakachua na hivyo kuleta fujo na madhara mengi kwa jamii ambayo hayakuwa ya lazima na kuvisingizia vyama vya upinzani kuwa ndivyo vyenye kuleta rabsha hizo!!!!!!!!!!


  1. Mafisadi waligharimia mabango ya JK nchi nzima kwa kutumia misamaha ya kodi ambayo serikali ya CCM huwapa kila mwaka…NEC ilishindwa kuthibiti matumizi makubwa ya CCM ikiwa ni pamoja ya kuyafuatilia kujua fedha hizo za kampeni zilikuwa zinatoka wapi…..fulana na kofia za ccm zilitengenezwa na mafisadi nje ya nchi na viliingizwa bila ya ushuru wa kodi…..mali na fedha za umma ikiwa ni pamoja na watumishi wa serikali walitumika kuipigia na kufanikisha kampeni za CCM……..



  1. Mafisadi kwa kutumia sms, mitandao ya internet na vyombo vya habari walifanikiwa kumchafua Dr. Slaa kwa kumwita mropokaji, mdini, n.k……na hivyo kumshushia hadhi kwenye jamii na serikali ya CCM iliendelea kuchekelea njama hizo za uvunjaji wa sheria za nchi hii badala ya kuchukua hatua za kukomesha hali hiyo ambayo ingeliweza kuvuruga amani na utulivu..



  1. Mafisadi kwa kuitumia serikali ya CCM walifanikiwa kuvitumia vyombo vya dola kama polisi na JWTZ kutisha wapigakura kuirejesha CCM madarakani…..



  1. Kuhakikisha katika chaguzi hii na nyinginezo zijazo NEC inaendelea kuwa ni kibaraka cha serikali ya CCM kwa kuhakikisha si vyama vya upinzani au hata bunge linashiriki katika uteuzi wake..na hivyo Raisi wa CCM ndiye ataendelea kuwa ndiye mteuzi wake……………..

Kwa mbinu hizi CCM itaendelea kuongoza kwa ridhaa ya mafisadi na kamwe serikali inayowajibika kwa mafisadi haitatuhakikishia "Maisha bora kwa kila Mtanzania" kwa sababu zifuatazo:-

1.Misamaha ya kodi ambayo ndicho kivuno kikubwa cha mafisadi na upewaji wa zabuni za kazi serikalini kwa kukuza madai ya malipo utahakikisha ya kuwa serikali haina fedha za kutoa huduma za jamii kama elimu bure na afya bure……..Hii ndiyo maana JK alipokuwa anahitimisha kampeni zake pale viwanja vya jangwani alikuwa na ubavu wa kutoa kauli chafu ya ….."……absolutely ridiculous" kama ni bezo lake la Dr. Slaa juu ya elimu na afya kuwa bure……………ingawaje Jk hakuona misamaha ya kodi kuwa………"absolutely ridiculous"


2.Kuendela kutegemea wafadhili kuendesha nchi hii na ndiyo maana JK alikiri ya kuwa bila misaada ahadi zake hazitekelezeki…….


3.Kuendelea kubeza mchango wa raia wa nchi hii katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na hivyo kutowawezesha na hivyo kuwategemea wawekezaji uchwara kutoka nje kuendeleza soko la ajira la ndani badala ya sisi wenyewe kufanya hivyo……Hivyo ajira finyu kuendelea kuwa tatizo hapa nchini………….
 
Vox populi, Vox Dei.. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Wagombea wa nafasi zote walioshinda wanastahili pongezi.. hata kama wameshinda kwa kura moja. mshindi anaweza kuonekana kituko machoni pako.. lakini si kwa yule aliyempigia kura.
Kumbuka, asiyekubali kushindwa si mshindani. Kusema CCM itakuwa imerudi madarakani kwa ridhaa ya mafisadi ni kuwakosea adabu watanzania. Matokeo ya uchaguzi huu wa mwaka 2010 ni mazuri kwa afya ya nchi yetu. Ni vema Bunge letu likawa na idadi kubwa ya opposition ili kujenga mfumo mzuri wa "Check and Balance".
Tujifunze kukubali matokeo.. hata kama imekula kwetu. Vinginevyo tutakuwa tuna-exercise DOMOKRASIA badala ya Demokrasia!
 
Ameanza kushikwa na tumbo la kuendesha..... bha ha haaaaaaaa
Huyo Jaji mstaafu NEC sidhani kama atafurahia pention yake maana ana laana toka kwa watz. Unaiba kura za watu kisa kumfurahisha JK??? Nilimwona alienda hata zimbabwe wkt wa mgogoro wa kura na hata kenya alienda. Hata kutumia hiyo computer ni mgogoro. Mtakuja niambia siku moja yatakayo mtokea:cool:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom