Tetesi: Yadaiwa rais wa Marekani Donald Trump akubali kupimwa usalama wa akili yake

kwinyo

JF-Expert Member
May 2, 2017
281
230
TRUMP KUPIMWA AKILI ?

Yadaiwa rais wa Marekani Donald Trump akubali kupimwa usalama wa akili yake.

Baada ya kuongezeka mashinikizo ya wananchi na vyombo vya habari vya Marekani, rais wa nchi hiyo, Donald Trump hatimaye amekubali kupimwa akili ili iweze kujulikana iwapo yuko salama kiakili au la.

Gazeti la Daily Telegraph limeripoti habari hiyo na kusema, baada ya Trump kukubali kupimwa akili, zoezi hilo sasa litafanyika Ijumaa ijayo katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC. Walter Reed ni hospitali kubwa zaidi ya kijeshi nchini Marekani.
Donald Trump

Imepangwa kuwa matokeo ya uchunguzi huo wa akili ya Trump yatawekwa hadharani ili watu wote waweze kuyaona. Kwa mujibu wa Telegraph, Trump amekubali kupimwa akili ili kupunguza wimbi la uvumi ulioenea katika kila kona ya dunia kwamba rais huyo wa Marekani hana akili timamu.

Suala la usalama wa kiakili wa Trump limepata nguvu zaidi siku chache zilizopita baada ya kusambazwa kitabu cha "Moto na Ghadhabu ndani ya White House ya Trump" kilichoandikwa na mtunzi wa vitabu wa Kimarekani, Michael Wolff. Sehemu ya kwanza ya maelezo ya kina ya kitabu hicho inayoakisi hofu na wasiwasi walionao wasaidizi waandamizi katika Ikulu ya White House kuhusu uzima wa kiakili wa rais wa Marekani ilichapishwa Jumatano iliyopita na gazeti la The Guardian.

Katika sehemu moja ya kitabu hicho, Michael Wolff anasimulia matukio ya kipindi cha mwaka mmoja wa urais wa Donald Trump na kusema kuwa, rais huyo wa Marekani hata hawezi kuwakumbuka marafiki zake wa zamani bali hata anasahau sana mambo yaliyomtokea.

Vile vile kitabu hicho kinachora picha inayoonesha udhalili wa rais wa Marekani Donald Trump na ukosefu wake mkubwa wa heshima alioudhihirisha zaidi baada ya kuingia katika Ikulu ya nchi hiyo. Kitabu hicho kinamuonesha Trump kuwa mtu mwenye fikra za kitoto ambaye hakutarajia kabisa kushinda urais na kuingia katika Ikulu ya White House.

d21f8a962baf4ddfbf7cef87b52164ff.jpg
 
Mimi kama mtanzania makini,mwenye akili timamu na ninayejitambua naunga mkono hatua hiyo ya marekani.But napenda na mimi nimuombe magufuli aweze kukubali kupima akili zake kwani nina wasiwasi kuwa na za kwake haziko timamu kutokana na matendo yake na maneno anayoongea.
 
Mwe... mwe...
 
wazungu ni wanafiki sana; kwani si ndio wao wenyewe waliompigia kura na kumweka madarakani??

Naomba na wewe upimwe akili mkuu, maandamano yote ya kipindi kile na mivutani ile hukuisikiaga?
 
TRUMP KUPIMWA AKILI ?

Yadaiwa rais wa Marekani Donald Trump akubali kupimwa usalama wa akili yake.

Baada ya kuongezeka mashinikizo ya wananchi na vyombo vya habari vya Marekani, rais wa nchi hiyo, Donald Trump hatimaye amekubali kupimwa akili ili iweze kujulikana iwapo yuko salama kiakili au la.

Gazeti la Daily Telegraph limeripoti habari hiyo na kusema, baada ya Trump kukubali kupimwa akili, zoezi hilo sasa litafanyika Ijumaa ijayo katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC. Walter Reed ni hospitali kubwa zaidi ya kijeshi nchini Marekani.
Donald Trump

Imepangwa kuwa matokeo ya uchunguzi huo wa akili ya Trump yatawekwa hadharani ili watu wote waweze kuyaona. Kwa mujibu wa Telegraph, Trump amekubali kupimwa akili ili kupunguza wimbi la uvumi ulioenea katika kila kona ya dunia kwamba rais huyo wa Marekani hana akili timamu.

Suala la usalama wa kiakili wa Trump limepata nguvu zaidi siku chache zilizopita baada ya kusambazwa kitabu cha "Moto na Ghadhabu ndani ya White House ya Trump" kilichoandikwa na mtunzi wa vitabu wa Kimarekani, Michael Wolff. Sehemu ya kwanza ya maelezo ya kina ya kitabu hicho inayoakisi hofu na wasiwasi walionao wasaidizi waandamizi katika Ikulu ya White House kuhusu uzima wa kiakili wa rais wa Marekani ilichapishwa Jumatano iliyopita na gazeti la The Guardian.

Katika sehemu moja ya kitabu hicho, Michael Wolff anasimulia matukio ya kipindi cha mwaka mmoja wa urais wa Donald Trump na kusema kuwa, rais huyo wa Marekani hata hawezi kuwakumbuka marafiki zake wa zamani bali hata anasahau sana mambo yaliyomtokea.

Vile vile kitabu hicho kinachora picha inayoonesha udhalili wa rais wa Marekani Donald Trump na ukosefu wake mkubwa wa heshima alioudhihirisha zaidi baada ya kuingia katika Ikulu ya nchi hiyo. Kitabu hicho kinamuonesha Trump kuwa mtu mwenye fikra za kitoto ambaye hakutarajia kabisa kushinda urais na kuingia katika Ikulu ya White House.

d21f8a962baf4ddfbf7cef87b52164ff.jpg
3
Huyu mwandishi haruhusiwi kutembelea tz na serikali imeamuru akamatwe popote atapoonekana tz kwa uchochezi kuwa rais wetu hamnazo
 
Back
Top Bottom