Yabainika magufuli anatumia sheria feki katika hifadhi ya barabara ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yabainika magufuli anatumia sheria feki katika hifadhi ya barabara ubungo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by darnessta, Mar 11, 2011.

 1. d

  darnessta Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Licha ya Waziri wa Ujenzi Mhe John Pombe Magufuli kujigamba kuwa ni muumini mzuri wa utawala wa sheria, na ameapa kulinda sheria kwa kutamka "Mungu Nisaidie" hivyo hawezi kusita kutekeleza sheria. Imebainika kuwa katika hoja ya hifadhi ya barabara Ubungo anatumia sheria feki.

  Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheia ya barabara-Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05/05 1967 inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) utakuwa ni Futi 75 kila upande. Na Ibara ya 4 ikaweka upana maalmu kwa barabara ya Morogoro kuwa ni kati ya Futi 300 hadi 400 kati ya Ubungo hadi Kibaha.

  Mara baada ya kukamilika barabara iliyokusudiwa na ibara ya 4 hapo juu mwanzoni mwa 1970s, Serikali ya awamu ya kwanza ilianzisha vijiji vya ujamaa na kuwagawia ardhi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia.

  Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya ya 1999 inatamka kuwa "Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya tarehe 01 Januari 1970 na tarehe 31 Desemba 1977, kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu kwa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo......

  Kifungu cha 16 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 kinatamka kuwa"Kwa madhumuni ya kuepusha mashaka na ili kuwezesha kuwapo kwa usalama wa miliki ya ardhi na hivyo kuchangia maendeleo ya ardhi ya kijiji, masharti ya Kifungu cha 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na Halmashauri ya Kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya tarehe 01 Januari 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii na kwamba badala ya tarehe zilizotajwa katika kifungu cha 15, kumewekwa tarehe kati ya tarehe 01 Januari 1978 na tarehe ya sheria hii kuanza kutumika".


  Vijiji vyote 52 vya Mkoa wa Dar es Salaam vilifutiwa hadhi ya vijiji mwaka 1985 kutokana na mahitaji makubwa ya ardhi kwa ajili ya upangaji wa Jiji hivyo kuingizwa katika Mipango Miji. Hivyo Mtu au watu waliogawiwa ardhi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia kufikia mwaka 1985 wananufaika na vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya 1999 ambayo iliwekwa sahihi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benajmin Mkapa tarehe 15 Mei 1999 ili kuanza kutumika kama sheria.

  Kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi Serikali ya Tanzania huchukua muda mrefu kuchapisha, kusambaza na kutoa elimu ya sheria mbali mbali kwa wananchi zinazopitishwa na Bunge . Hivyo Mhe John Magufuli aliposhika wadhifa wa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza mwaka 2000, akatumia mapungufu hayo ya serikali kusigina haki za wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vilivyotajwa hapo juu kwa kuagiza kupandwa kwa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi hao bila ya uchambuzi wowote kufanyika kubaini ni akina nai wanapaswa kunufaika na Sheria ya Ardhi ya Vijiji.

  Kuanzia tarehe 15 Mei 1999 Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya ya 1999 ilipoanza kutumiaka kama Sheria (Lwa) Ibara ya 4 Kanuni za Sheria ya Barabara za 1967 ilyoweka upana wa kati ya Futi 300 hadi 400 katika eneo kati ya Ubungo hadi Kibaha ilipoteza uhai kwa watu wote waliokuwa wakiishi katika vijiji hadi mwaka 1985. Hivyo Kanuni ya hifadhi ya Barabara iliyobaki na uhai na ibara ya 2 inayotamka kuwa Hifadhi ya barabara zote kuu hap nchini ni Futi 75 kila upande. Hata Master Plan ya Jiji la Dar es Salaam ndiyo iliadopt ibara hiyo wakati inatengenezwa mwaka 1979.

  Kwa mantiki hiyo lilikuwa kosa kubwa kwa Mhe John Magufuli kuagiza mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara kupandwa Mita 120 ndani ya ardhi na makazi ya wananchi kati ya Ubungo hadi Kiruvia kiholela pasipo kufanyika uchambuzi wa ain ayoyote kuwatamnbua wale wanaopaswa kunufaika na sheria ya 1999.

  Kwa kuwa Mhe John Magufuli alikuwa mbunge wakati Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 inapitishwa na Bunge mwaka 1999, ni dhahiri alikuwa akitambua maudhui ya vifungu 15 na 16 kuwa vinawapa haki wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia n.k ndio maana akakwepa kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa, Tarafa, Kata na Seriklai za Mitaa katika zoezi hilo la kikandamizaji. Vile vile amekataa majadiliano ya aina yoyote kuhusu suala hilo mapaka sasa na anaendeleza ukandamizaji kwa kutumia ulaghai kuhus msongamano wa magari na mradi wa mabasi yaendayo kasi.

  Ni kwa kuzingatia ukwei huu, ukarabati wa barabara ya Morogoro kati ya Dar-Mandizi uliofanyika mwaka 2001 uliwagusa tu wale waliojenga ndani ya hifadhi ya barabara ya Futi 75 kila upande, hata hivyo busara kubwa ilitumika kwa zile nyumba zilizoko katika eneo lililohitajikwa kwa upanuzi wa barabara wakati huo ndizo tu zilizobomolewa, zipo zilizobomolewa zote, nusu, robo zingine uzio tu n.k.


  Ibara ya 29 (1a, b) ya Kanuni za Sheria mpya ya Barabara namba 13 ya 2007-Tangazo la Serikali Na 21 la Tar 23 Januari 2009, inatamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) ziwe za njia moja (single carriageway), au njia mbili (dual carriage ways) utakuwa ni Mita 60 tu, yaani Mita 30 kila upande wa barabara. Ikizingatiwa kuwa hata sheria ya zamani ilitamka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu ya nchini (Trunk Roads) ni Futi 75 kila upande. Na kwa kuzingatia kuwa Ibara ya 27 Kanuni ya mpya inatamka kuwa upana wa chini kabisa wa njia moja ya barabara (lane) katika barabara kuu (Trunk Roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25.

  Hivyo upana wa hifadhi ya barabara uliowekwa na Kanuni za sheria mpya ya barabara ya 2007 wa Mita 60 unao uwezo wa kuzalisha njia za 18 (lanes) yaani 9 za kuelekea Kibaha na njia 9 (lanes) za kuja Dar. Hivyo madai ya Mhe John Magufuli kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro unasababishwa na watu waliojenga nje ya Mita 60 ndio maana akaagiza nyumba hizo kuwekewa alama ya X hayama ukweli wowote. Aidha hana uhalalai wowote wa kisheria kushinikiza nyumba zilizoko nje ya Mita 30 kila upande wa barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia kubomolewa kwa kuwa hazina uhusiano wowote na msongamano wa magari na hazizuii kwa namna yoyote ile upanuzi wa barabara hiyo.

  Kutokana na matendo yasiyo halali ya Mhe John Magufuli, mwaka 2009 wakati Wizara ya Ujenzi inatengenza Kanuni za Sheria mpya ya barabara ilijichanganya pale Waziri mwenye dhamana ya barabara aliponakiri Ibara ya 4 ya Kanuni za Sheria ya barabara-Tangazo la Serikali namba 161 la Tar 05/05 1967, kama ilivyokuwa ikisomeka mwaka 1967 (miaka 43 iliyopita) na hivyo kufanya ibara 29 (2) kuendelea kusomeka kuwa "upana wa hifadhi ya barabara kati ya Ubungo hadi Kiruvia ni Mita 120 sawa na Futi 300 hadi 400"; na hivyo kuwepo mgongano kati ya Ibara hiyo ya Kanuni (Regulation) na maudhui ya vifungu 15 na 16 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 (Law enacted by the Parliament) katika maeneo yaliyokuwa yakiitwa vijiji vya Kimara, Mbezi, Kibamba na Kiruvia.

  Licha ya mgonagno huo kati ya Kanuni na Sheria Ibara ya 29 (2) inapingana na Ibara 29 (1 a,b) inayosemeka kuwa upana wa hifadhi ya barabara kwa barabara zote kuu hapa nchini (Trunk roads) ziwe za njia moja (single carriageway), au njia mbili (dual carriage ways) utakuwa ni Mita 60 tu, yaani Mita 30 kila upande wa barabara.

  MY TAKE: WAZIRI MKUU MIZENO PINDA BEING A LAWYER BY PROFESSION AMESHAGUNDUA MGONGANO ULIOPO AMBAO UMESABABISHWA NA UBABE WA MHE JOHN MAGUFULI WA MWAKA 2001 ALIPOVAMIA SECRETLY ARDHI NA MAKAZI YA WANANCHI NA HIVI SASA CLANDESTINELY KUTAKA KOBOMOA NYUMBA ZA WANANCHI KWA KUTUMIA KWA TATIZO LA MSONGOMANO WA MAGARI NA UJENZI WA BARABARA ZA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI AMBAYO HAYANA UHUSIANO WOWOTE NA NYUMBA ZILIZOKO NJE YA MITA 30 KILA UANDE WA BARABARA.

  kWA KUWA MWAKA 2008 MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (DART) ULIWALIPA FIDIA HANDSOMELY WAATHRIKA WOTE WA MRADI HUO BILA YA KUJALI POROJO ZA KUWEPO KATIKA HIFADHI YA BARABARA. HIVYO MAGUFULI ANADANGANYA UMMA ANAPODAI KUWA ANATAKA KUBOMOA NYUMBA ZA WATU 120 METRES FROM THE ROAD KWA AJILI YA MRADI HUO.

  ILI KUMALIZA MGOGORO HUU ULIOZAA BOMOA BOMOA HOLELA IITWAYO MAGUFULI, AMBAO PIA ULISABABISHA CCM KUPOTEZA JIMBO LA UBUNGO NA VITI KADHAA VYA UDIWANI, KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2010. WAZIRI MKUU PINDA ANATAKIWA KUMWAGIZA MAGUFULI KUONDOA (TO OFFCIALLY DELETE) IBARA YA 29 (2) YA KANUNI MPYA ZA SHERIA YA BARABARA ILIYONAKILIWA KAMA ILIVYO KUTOKA KANUNI ZA 1967 BILA KUZINGATIA MAUDHUI YA VIFUNGU 15 NA 16 VYA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NAMBA 5 YA 1999.

  HIYO ITAONDOA MGONGANO ULIOPO KATI YA KANUNI ZILIZOTUNGWA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA (REGULATIONS) NA SHERIA ZILIZOTUNGWA NA BUNGE (LAWS ENACTED BY THE PARLIAMENT); THEREFORE SECTION 29 (1) OF THE REGULATIONS WILL PREVAIL WHICH REAFFIRMS THAT THE ROAD RESERVE IN ALL TRUNK ROADS EITHER SINGLE AND DUAL CARRIAGE WAYS IN TANZANIA IS ONLY 60 METRES.

  KATIKA HILI HAMNA HAJA YA KUSUMBUA BARAZA LA MAWAZIRI FOR SUCH MINOR ISSUES OF FEW PEOPLE LOOKING FOR CHEAP POPULARITY THROUGH THE SUFFERINGS OF OTHERS, IT IS JUST KNOWING HOW TO TAME THE ERRANT HORSE.
   
 2. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pole sana Darnessta, nahisi unapigania kutobomolewa nyumba yako, maana umechimbuka sheria karibu uniambukize na mimi interest ya kusoma sheria.

  Darnessta, matatizo ya nchi yetu ni mengi sana, ikiwa ni pamoja na Dowans (ila hilo najua hujawahi kujitokeza kulalamika), EPA, na Ufisadi mwingi mwingine tunaoujua na ule ambao bado ni siri.

  Dawa ya kuondokana na matatizo ya viongozi wetu kama Dr Magufuri, ni kuwaunga mkono vyama pinzani..unaonaje? Kwasababu kutegemea Pinda kumdhibiti Mh Magufuri ni kupoteza wakati bure, kwani Pinda huyo huyo ameshindwa kudhibiti matatizo mengine kwa kutoa majibu dhaifu tu na wakati mwingine anaishia kulia mbele wanawake na wanaume, mbele ya watoto na wageni! Hakuna kitu cha kutegemea hapo.
   
 3. d

  darnessta Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vyama vya Upinzani sio Mwarobaini wa kila kitu, unaweza kuwa na vyama, wabunge, madiwani and everything lakini kama mind set ya wananchi haijabadilika hata viongozi wa vyama watachoka na hatmaye kurithishwa mabaya. Charity begins at home, if you cant fight for your yr right at household level how do you expect to fight for it at the National level? Hayo ndio mawazo ya kusubiri abowe, Slaam Zitto Mnyika n.k waseme na sisi wengine kuungo mkono, hayana tofauti na mawzo yaliyotalamaki huko CCM pia na branch of this Tanzania nad thata is the breding ground of DOWANS and the kind.

  Ndio maana ni lazima katika kero zinzotuzungka tuzionyeshe ili decdision makers wafanye sustainabale decisions. Big Up Pinda!!!!!!!!!!
   
 4. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimeshindwa kukuelewa! Huenda wewe ni shabiki wa Pinda na ni mpinzani wa Dr Magufuri. Unaposema vyama vingi sio mwarobaini, niambie ni nani aliyeibua madudu yote ya ufisadi tunayoyafahamu hivi sasa? Nani anayeyakemea kwa bidii zaidi kama sio vyama vya upinzani? Nani anayejaribu kuyatetea na kuyafunika kama siyo CCM?

  Kuhusu kubadili mind set up ya watu, nadhani CDM na baadhi ya vyama pinzani wanaifanya hiyo kazi vizuri. CCM wanazuia uamusho wa watu kwa kuwaambia, tulieni msichafue amani!! Msiwasikilize hao vyama vya msimu!! Je unadhani mind set up ya watu inaweza kurekebishwa na hoja za namna hiyo kama chama tawala wanavyotaka?

  Sawa, ni kweli charity begins at home, lakini charity at home isigeuke kuwa mtaji wa ubinafsi. Unapoguswa wewe una react spontaneously na wengine wakiumia wewe unashangilia tu. Tunahitaji mfumo mzima wa kutenda haki uwe overhauled na tuanze na system tunayoitaka kutuletea maendeleo ya haraka.

  Pinda hawezi kutupa matumaini tunayohitaji, na pia CCM, pamoja na ukweli kwamba hicho ndio chama changu.
   
 5. d

  darnessta Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Moja ya athari mbaya ya ulaghai wa Mhe John Magufuli kuhusu utata katika uoana wa hifadhi za barabara ni majirani kujengeana chuki kutokana na kuamini kuwa wenzao ambao wanadaiwa kujenga katika hifadhi ya barabara wakati sio kweli hata kidogo ndio chanzo cha kuteseka kwao kwa tatizo la msongamano wa magari hivyo kila kukicha wanakesha wakiomba wabomolewe nyumba hizo wakiamini kuwa hilo ndilo suluhisho la tatizo la msongamano wa magari.

  Kwa mujibu wa tovuti ya TANROAD hakuna mpango wowote wa kuifanyia upanuzi barabara ya Morogoro kati ya Kimara hadi Mlandizi kwa sasa na taarifa kutoka baadhi ya viongozi waandamizi labda upanuzi huo utafanyika baada ya miaka mitano. Ujenzi unaotarajiwa ni wa barabara za mabasi yaendayo kasi kati ya Kimara hadi Mjini ambapo mradi huo ulikwishawalipa fidia waathrika wa mradi huo tokea 2008.Kutokana na hali hiyo Mhe John Magufuli alipaswa kuwa muangalifu kutoa kauli zinazoweza kuwachonganisha majirani bila ya kupima athari zake kwa umma
  .
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  bwana we pole sana kaka, sheria iko pale pale wewe tu ndo hujaelewa na ukijifanya kujua sana sheria ndo hutalipwa hata kifuta machozi
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huna lolote wewe tatizo lako ni kujiingiza katika ushabiki wa siasa za kijinga za CCM
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakuna lolote wabongo tumezoea njia za mkato. Na tatizo lingine ni ukiritimba uliokithiri pale wizara ya ardhi lakini tusimlaumu Dr. Magufuli kwani ni mchapa kazi hodari.
   
 9. d

  darnessta Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nahisi wewe ni mmoja wa mamangi meza mnaosubiri Dr Slaa, Mbowe, Zitto n.k.wakuamsh. Unaweza kuniambia wewe binafsi umeshafanya nini kupinga maovu katika eneo lako linalokuzunguka? Umeshirikia vipi katika kupambana na maovu kama haya ya Mhe John Magufuli kutumia madaraka yaake vibaya kudanganya taifa kuhusu upana wa hifadhi ya barabara?

  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Hata hao unaofikiri ni miungu watu wana madhaifu yao pia, mbona unafunga macho na hutaki kuyaona. Pinda akifanya jambo jema anastahili kupongezwa husuana kama ili la kupinga matumizi mabaya ya madaraka.

  kwa mtazamao wako wa kungoja kuongozwa badala ya raia kuonyesha the way, hata CDM wakichukua madaraka wananchi wakiendelea kulala kama hivi watafanya ufisadi? Au CDM hakuna watu wenye magari kama VUGUE? unafikiri kwa kuwa CDM they are immune to ufisadi. Ufisadi ni ya tabia ya mtu na unachipua na kumea pale watu kama ninyi mnapongoja viongozi wawaonyesha njia badala ya raia kuonyesha njia tunataka kuongozwa kwenda wapi.

  Kwangu mimi naona CDM na CUF should have been a product of watu waliondokana na uvivu wa kufikiri na wakatambua haki zao and not the opposite kama unavyotaka wewe Kusubiri Dr Slaa, Mbowe n.k wawaamshe. CCM haiwezi kushindwa kabala ya wananchma wake kushindwa, kwa kuwa umekiri ni chama chako udhaifu wako kama mwanachama uliosababisha ishindwe umehama nao kuja nao CDM anayo itashindwa tu kutokana na udhaifu wako.
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa maana hiyo bandiko lake, limeegemea vitu viwili vikuu:
  1. Chuki dhidi ya Magufuli, na wala sio chuki dhidi ya wananchi waliotendewa ndivyo sivyo
  2. Kupoteza jimbo na kata za Ubungo, kulikosababishwa na Magufuli baada ya kutwatendea wananchi ncdivyo sivyo.

  Mimi nadhani kwa hayo mambo 2 umeonyesha udhaifu mkubwa: Kwanza kutokuwa na mapenzi ya kweli kwa wananchi, haswa pale ambapo nyie matakwa yenu ya kiutawala yanatimia. Pili, yote yanayofanyika sio kwa nia ya kuikwamua nchi katika lindi la umaskini, ila ni njia tu ya kuwahadaa wananchi ili wawe katika mkao wa kutawaliwa kwa vitu vyepesi vyepesi.

  Labda nikuulize: Je, huko ccm ilikoshindwa, nako pia Magufuli pia alikuwa na miradi? Nini impact ya Magufuli ndani ya nchi hii akiwa kama Mbunge na waziri? Je, Magufuli amechangia kwa kiasi gani kuporomoka kwa umaarufu wa ccm?

  Kwanini msiite tu chepe/beleshi kwa jina lake na sio "kijiko kikubwa".
   
 11. d

  darnessta Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeuliza swali zuri sana. Impact ya Magufuli katika CCM kuchuliwa ni pale alipotumia ubabe kama huu kuuza nyumba za Serikali kwa bei chee, hakika wananchi wengi sana wankerwa na hili mpaka leo. Hivyo ninamini kuwa utakubalina na mimi amechangia sana kuporomosha umaarugu wa CCM kwa kuuza nyumba za Serikali kw abei chee. Usisahau kitendo cha kuwagawia watu ambao hawakustahili kwa mujibu alivyokuwa ameviweka na wakafanikiwa kupata nyumba za serikali. Kwanini mnaficha mamabo amabayo yametokea. Huu sio Ufisadi Pia?
   
 12. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35

  Tatizo lako unaongea mambo ya kuhisi, sasa unataka nipoteze muda wangu kujadili hisia zako?
  Mimi nimetoa constructive crical views kwenye bandiko lako, sasa unataka kugeuza uwe mahakama nijieleze kama ninasitahili kuchangia kwenye bandiko lako. Je ni lazima mimi niwe nimefanya jambo fulani ndio nipate uhalalai wa kuzungumza maswala yanayohusu nchi yangu? Basi nakushauri utoe sifa za watu wanaotakiwa kuchangia kwenye hoja yako. Mimi nimefanya mambo mema mengi sana na mengine yapo kwenye CV yangu na mengine yapo katika ufahamu wa watu wengi wanaonifahamu.  Naomba usiniwekee maneno yako mdomoni mwangu. Mawazo yako naomba yabaki ya kwako..usiyahamishie kwa wenziyo kwa lazima. Wewe endelea kumpongeza Pinda kila anapokufurahisha kumpinga adui yako Dr Magufuri  Kila mtu ni kiongozi mahala pake na kwa wakati wake. Hata hivyo ni vizuri kukubali kuongozwa, ukikataa kuongozwa unaweza kuwa chanzo cha uasi. Wakati huohuo unapokuwa na viongozi bado unayo fursa ya kuwa pima na kuona mapungufu yao kama W/M PK Pinda anavyopindisha mambo.

  Mimi si mtetezi wa CDM, bali ninafurahishwa na mtu yeyote ama chama chochote kinachojitokeza kupigania wanyonge wa nchi hii kama alivyofanya hayati baba wa taifa. Kama kwa bahati CDM wakatupokonya madaraka 2015 na wakageuka kuwa fisadi, mimi (God willing) nitatoa sauti yangu kuwalaumu kama ninavyofanya sasa  Kijana, naona umejaa assumptions nyingi mu kichwa chako kweli! Mimi sijasema nimehamia CDM katika majibu yangu. Uwe unasoma/kusikiliza na kuelewa vizuri ili kujiepusha na kuandika assumptions.

  Mimi ninasuport kazi ya Dr Slaa na Mh Mbowe na sio kungoja tu peke yake
   
 13. K

  Kaisikii Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  we mwanzisha madaa unachuki binafsi umejipanga wazi wazi tena kweupe kujaribu kumchafulia maghufuli.binafsi naona thread yako imekaa kisiasa zaidi ndani yake..itakuwa ni mwakilishi wa watu waliokumbana na marekebisho yaliyofanywa ndani ya wizara.
   
 14. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  we ni shenzi tuu kwani wapinzani wao hawafati sheria zilizowekwa kihalali na bunge?? i hate magufuli sana coz ana ubabe sana,my dady alisoma nae na alishawahi kuniambia kuna siku magufuli aliwafungia mlango wa bweni kwa ubabe wake kisa tuu alikuwa ni kiongozi shuleni,magufuli acha ubabe watu hawatafuti uraisi kwa jinsi hiyo
   
 15. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nampa pole sana huyu ndugu maana anaonyesha ushabiki na kujidai anajua sheria wakati hajaelewa muktadha wa maagizo ya magufuli. Mh. Magufuli hajawahi kuweka mawe mita 120 kuonyesha hifadhi ya barabara, bali mawe yote yaliyowekwa ni mita 20 kwa kila upande ambayo ni karibia sawa na futi 70 unazozungumzia wewe mtoa mada. Jiridhishe kwanza na uelewa wa sheria kabla ya kurusha mada kwenye jukwaa hili.

  Unajua eneo la mita 120 linalingana na urefu wa uwanja wa mpira wa miguu. Je ni wapi kuna mawe ya hifadhi ya barabara yaliyochukua eneo linalolingana na uwanja wa mpira wa miguu kwa kila upande wa barabara? Acha propaganda za ki-Mizengo Pinda hapa.
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kweli magufuli hafai unasema alimfungia mzee wako wakati anataka kwenda pombeni? hakufanya vizuri kwani kila mwanafunzi ana haki ya kunywa pombe na kucheza pasipo kufata sharia.pia hongera kwa kuwa kijana mwema mwenye kufanyia kazi kauli za wazazi bila kuzipinga nadhani hii ndio siri ya mafanikio yako ........namimi nafanya hivo hivo pia...pili kwa tanzania kwani mabara bara mapana ya nini wakati hatuna magari mengi na hatuna mpango wa kuogopa msongamano wa magari wa baada ya miaka 10.

  ha ha ha mjumbe nadhani wewe mlalamikaji na magufuli wote ni watu wema sana
   
 17. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Thanks Kashaga, habari za huko bondeni?
   
 18. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Du! kaka na wewe upo nini kwenye hifadhi ya barabara maanake unahasira
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Mimi namuunga mkono mtoa mada, naomba mtembelee kati ya Ubungo na Kiruvia mpakani na KIbaha mawe na mbango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara yaliwekwa Mita 120 ndani ya kutoka katikati ya barabara. Mimi naishi eneo la Kibamba mawea, mabanago na miti ya miarobaini ilipandwa pasipo taarifa yoyote. Hivyo haifaia kuamteeta Magufuli tu hata katika jambo msilolifahamua vyema. Najua watu wengi ni mashabiki wa Magufuli kutokana na kujua kucheza na madia lakini sasa ukwlei unaanza kutokeza. Magufuli ni dikteta.
   
 20. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mimi ni mmoja ya watu wanaoheshimu na kuthamini sana mchango wa Mhe Magufuli. Hata hivyo hilo la nyumba za serikali kuuzwa kwa bei ya bure kwa watu walionacho silifagilii kabisa. Na hili lilinifanya niwenatafakari sana hatua zake. Mfano, kuagiza kuvunja jengo la Tanesco Ubungo sidhani ni busara. Two wrongs do not make it right. Hivi namna pekee ya kurekebisha kosa hilo ni kubomoa jengao hilo?
  Huko Mwanza alilazimisha mambo kuhusu kubomolewa mtu fulani. Ni kweli mtu huyo alibomolewa lakini serikali ilikuja kulipa fidia ya kutosha.
  Nilitafakari sana pale Magufuli alipopewa Naibu waziri Dr. Mwakyembe ambaye ni mwanasheria kwa taaluma. Mwanzoni nilifikiri ilikuwa ni kutomtumia sawasawa rasilimali watu ila sasa naamini Dr. Magufuli anamuhitaji sana Mwakyembe kwa ushauri. Sina hakika kama anamtumia iwezekanavyo.
   
Loading...