Uchaguzi 2020 Yaani CCM ni SGR, Ndege na Stieglers. Ndiyo sera yao kila mahali

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Yaani kila mahali wimbo wao Ndege, SGR na STIGLERS kila mahali kwenye mabrasha yao wanatembea na hayo mambo 3. Yaani huwezi kumkuta mtu anaimba nje ya hayo. Hivi hayo mmefanya kwa pesa zenu?

Hawa jamaa hawana jipya hadi wanatia huruma. Haya mambo matatu utafikiri ndio ilani yao. Hawana mapya wimbo mmoja kila siku. Huu wimbo wenu umechukua tafuteni mwingine.

Hivi hamna watu wabunifu CCM?
 
Hata Mimi nawashangaa hawa CCM.
BORA KULE KWA JAMAA WA KIKI ZA MIUJIZA HUKU IRANI YAKE IKIWA ENDAPO AKISHINDA ATANZISHA KIWANDA CHA MATUSI NA KUPAYUKA PAYUKA HOVYO NA KUWA ITA WATUMISHI WA UMA NI TAKATAKA.
 
Kama Akili yako ni nzuri Huwezi kubeza Mafanikio hayo. Jiulize kwa nini Huko nyuma haikuwezekana? Mpaka Awamu ya Magufuli?

Tafuteni Kazi za kufanya. Hadithi za Halimbaya ya maisha ya watanzania zipotu kwa wale wavivu wa kufikiri na waliokua wanategemea ujanja ujanja uliokuwepo.

Kila Mbuzi Atakula kwa Urefu wa Kamba YAKE.
 
Mafanikio yenyewe ni work in progress, SGR bado haijaisha na Stiglers Gorge bado kabisa. Ndege zimeegeshwa hapo Kipawa na ATCL haijiendeshi kwa faida. Hayati sio mafanikio.
 
Mkuu ulitegemea Reli na Stiglers Gorge Zishuke kutoka Mbinguni ndio chama cha mapinduzi kijivunie?

Wakati tunakodisha ndege Mbovu kutoka ufaransa kwa Mabilioni ya PESA na huku shirika likiwa hoi bin taabani Na wabunge wa upinzani wakiitukana serikali ya chama cha mapinduzi bungeni kwamba imeshindwa hata kununua ndege 1 Ndio Ulikua unapenda?

Siku zote Wapinga maendeleo hawatakosekana lakini Serikali ya CCM imejipanga kutuletea maendeleo hata kama mtabeza baadae mtatuelewa.
Mafanikio yenyewe ni work in progress, SGR bado haijaisha na Stiglers gorge bado kabisa. Ndege zimeegeshwa hapo Kipawa na ATCL haijiendeshi kwa faida. Hayati sio mafanikio.
 
Halafu sijui hizo Ndege, SGR na STIGLER sisi tulioko huku Mtanana zinatusaidia nini!!!

1599499379599.png

muulize huyu apa znamsaidia nn!
 
Yule dingi wa chato kachoka mnoo kisera.

Zile hadithi zake za Tanzania ya viwanda za 2015 zimebakia kuwa zilipendwa, anaogopa hata kuzisema, maana wananchi wanajua zilikuwa ni full fix.

Sasa ndege alizozipaki pale airport ndio imekuwa sera zake mpya.
 
Wajinga hawataona Impact ya hii miradi inayowekezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Ila nikwambie. Miradi hii PESA zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kuhudumia wananchi.

Huwezi kusema ndege hainisaidii wakati kuna Utalii unaotegemea Usafiri wa Anga. Hao wageni watakuja na Bodaboda? Utapataje PESA za kigeni kama huwekezi?

Huwezi kubeza SGR kwamba huta panda Tren hivyo haina Msaada kwako una sahau kwamba Kuna wakulima wanategema usafirishaji wa mazao na mizigo wakipata usafiri wa uhakika na nafuu utapunguza Mfumuko wa bei na kusaidia kupunguza Gharama za maisha.

Huwezi kubeza Mradi wa Bwawa la Nyerere kwamba Hauna tija wakati Viwanda vina hitaji Umeme wa uhakika na wagharama nafuu ili kuongeza uzalishaji na Ajira.

Ndio maana nasema wafuasi wengi wa upinzani Akili zenu ni ndogo sana. Mnawaza kuwa na PESA Mfukoni kuliko kuangalia Vitu vya msingi ambavyo ndio vitakua mkombozi wa watu wengi wa taifa hili.

Hivi umeshajiuliza ukawa na fedha mfukoni Alafu hakuna Miundo mbinu mizuri ikapelekea Mfumuko mkubwa wa bei hivi hiyo hela itakusaidia nini?

Umeshajiuliza Congo ya Mobutu ilikua unaenda kununua mkate na sanduku la Pesa Kutokana na serikali kutokuwekeza kwenye Miundombinu ila iliruhusu watu wawe na PESA Ambazo mwisho wa siku hazikuwasaidia wakamtoa madarakani.

Hivyo wanadamu hawana jema. Hiyo Ndio nature yao. Mimi naipongeza CCM kwa misimamo YAKE chini ya Rais Magufuli. Nchi haiendeshwi kwa kusikiliza watu nchi inaendeshwa kwa kufuata vipaumbele vya msingi na sio kuwanufaisha wachache Bali kwa manufaa ya wengi.
Halafu sijui hizo Ndege, SGR na STIGLER sisi tulioko huku Mtanana zinatusaidia nini!!!
 
Wajinga hawataona Impact ya hii miradi inayowekezwa na Serikali ya chama cha mapinduzi.

Ila nikwambie. Miradi hii PESA zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kuhudumia wananchi.

Huwezi kusema ndege hainisaidii wakati kuna Utalii unaotegemea Usafiri wa Anga. Hao wageni watakuja na Bodaboda? Utapataje PESA za kigeni kama huwekezi?

Huwezi kubeza SGR kwamba huta panda Tren hivyo haina Msaada kwako una sahau kwamba Kuna wakulima wanategema usafirishaji wa mazao na mizigo wakipata usafiri wa uhakika na nafuu utapunguza Mfumuko wa bei na kusaidia kupunguza Gharama za maisha.

Huwezi kubeza Mradi wa Bwawa la Nyerere kwamba Hauna tija wakati Viwanda vina hitaji Umeme wa uhakika na wagharama nafuu ili kuongeza uzalishaji na Ajira.

Ndio maana nasema wafuasi wengi wa upinzani Akili zenu ni ndogo sana. Mnawaza kuwa na PESA Mfukoni kuliko kuangalia Vitu vya msingi ambavyo ndio vitakua mkombozi wa watu wengi wa taifa hili.

Hivi umeshajiuliza ukawa na fedha mfukoni Alafu hakuna Miundo mbinu mizuri ikapelekea Mfumuko mkubwa wa bei hivi hiyo hela itakusaidia nini?

Umeshajiuliza Congo ya Mobutu ilikua unaenda kununua mkate na sanduku la Pesa Kutokana na serikali kutokuwekeza kwenye Miundombinu ila iliruhusu watu wawe na PESA Ambazo mwisho wa siku hazikuwasaidia wakamtoa madarakani.

Hivyo wanadamu hawana jema. Hiyo Ndio nature yao. Mimi naipongeza CCM kwa misimamo YAKE chini ya Rais Magufuli. Nchi haiendeshwi kwa kusikiliza watu nchi inaendeshwa kwa kufuata vipaumbele vya msingi na sio kuwanufaisha wachache Bali kwa manufaa ya wengi.
Umemamaliza kuandika au unaendelea?
 
Mkuu tangaza sera zako, za wengine waache wenyewe kama wananchi hawapendi si hawatamchagua
 
Back
Top Bottom