Yaaaalah! Wandugu! Hali mbaya sana, msaada wa haraka unahitajika

Kuwa verified kwanza ili watu wakuamini. Wasiliana na mods kwa hatua zaidi
 
Kidogo nakushangaa..jamani mm niwe connected na watu kama hao alafu nisitoke..never aisee ..!mie hata leo niunganishwe na Kaijage kwakwel ntatusuaa sasa sijui ww una uzito gan...!hyo circle uloyoisema ni bora ukairudia ikakusaidia mkakati wa kuishi mjini..nawaza tu
Utamponza mwenzako aliwe kiboga buree
 
POLE NDUGU
MWAMINI MUNGU KWANZ BINADMU HUMU NYOKA.
PELEKA FACEBOOK .MSAADAUTAKUWAMKUBWA ZAIDI
HABARI ZENU WAKUBWA!
Naitwa JAMES YUSTAR EBRANIA
Kijana mkakamavu umri 28,

Nimekuwa mfatiliaji wa JF tangu mwaka 2011, kabla ya mwaka Jana kujiunga rasmi.

Wakubwa, Leo naomba niwashirikishe changamoto nazopitia Kama kijana,
Naomba nianze na history fupi ya maisha yangu.

Binafsi ninaamini ya kuwa kila binadamu anaishi kwa Neema za MUNGU tu' kupata na kukosa, maradhi na uzima wetu vinamtegemea huyo MUNGU japo kila mtu anakuwa na imani yake kwa wakati wake.

Binafsi napenda kumshukuru MUNGU kila wakati maana kunasehemu amenitoa na kunamahali ananipeleka, ili aweze kutimiza kusudi la uumbaji wake ktk maisha yangu.
Kwa ufupi tu'nikwamba History YaNGu iko hivi;

Kabla ya kuwa kijana wa leo, nilikuwa mtoto mchanga.
Niliyezaliwa nikafungashwa ndani ya box na kutupwa jalalani
Kwa Neema za MUNGU alipita mama msamaria aitwaye YUSTAR akaniokota toka kwenye midomo ya Mbwa waliokuwa wanaliburuta Lile box nilimokuwa ili wanile Kama mzoga

Huyo mamaangu alinilea kwa UPENDO mkuu, lkn kwa bahati mbaya nilipofikisha miaka 7 mamaangu alifariki dunia Rest in Paradise's my dear Mother Naamini siku moja tutakutana.

Kifo cha mamaangu kilipelekea ndoto zangu kuyeyuka. Mama aliniacha Niko darasa la 3 ktk shule ya Plan intanational Arusha.
Wakati huo tulikuwa tunaishi Njiro.
Baada ya mama kufariki, Ndugu mmoja Mwenye tamaa alinifukuza nyumbani kwa kunitumia watu waje shule waniteke na kunipeleka melerani ili waniuwe.
Neema za MUNGU Tena ziliniokoa ktkt ya watesi hao.
Sitaweza kuelezea hicho kipande vipi niliokoka toka kule melelani, maana naumia saana nikikumbuka
Hapo ndipo ukawa mwanzo wa maisha mapya ktk umri mdogo wa miaka 8.
Ndipo nikawa rasmi mtoto wa Mtaani najipambania mwenyewe kula na kulala. Hapo ndipo nikaanza kudandia magari na kunipeleka sehemu mbali mbali, mpaka mwaka 1999 nikaja Dar es Salaam. Nilipofika Dar es Salaam nikawa nauza mifuko ya Rambo shimoni k/ Koo, nilikuwa na Rafiki yangu tuliyetoka wote anaitwa Bruno, yeye alikuwa anauza sigara pia hivyo tulikuwa tunauza usiku na mchana.
Mwaka 2000 tulipata pesa tukaenda kupanga chumba kule maheneo ya mchikichini jirani na Jangwani.
Tulipopanga tu chumba nikaanza kupata wazo la kurudi shule kuendelea na masomo.

Hivyo nilimshirikisha huyo rafiki yangu aliyekuwa Ni Kama Ndugu wa damu kabisa.
Jamaangu ali-support wazo langu kwa UPENDO mkuu, japo yeye pia aliacha shule darasa la 4 lkn hakuona shida kunitia moyo Mimi kufanikisha kurud shule. Hivyo tulinunua mahitaji ya shule, shule zilipofungua tukaanza kutafuta shule.
Nilibahatika kupata shule ya msingi Uhuru mchanganyiko pale K/Koo.
Sikuingia shule kwa Njia halali, niliingia kwa ujanja-ujanja maana nilikuwa nahitaji kusoma lkn kila shule nayoenda naambiwa wamefunga kupokea wanafunzi wapya
Hivyo nilipoenda shule ya Uhuru mchanganyiko bahati nzuri nilikutana na wanafunzi wa tukutu, watoto wa Dogodogo center, wao walikuwa wanasoma darasa la 4 so baada ya kuwaambia hitaji langu wakaniuliza " Unajua kusoma na kuandika!?" Nikajibu ndio. Wakanambia twende katununulie mihogo afu twende darasani kwetu. Nikafanya walichohitaji, Kisha tukaenda darasani, tuliingia darasani tukaenda kukaa wanapokaa wao.
Walimfukuza mwanafunzi mwingine waliokuwa wanakaanaye ili me nikae.
Mara mwalimu aliingia Darasani hivyo kwa mara ya Kwanza nilianza kusoma Tena, nilifurahi saana baada yakujiona nasoma kwa mara nyingine
Nilihisi Kama naota vile ! Kuna wakati nikawanajifinya ili nijue Kama ni Mimi kweli, nikijifinya nikiumia naanza kucheka moyoni

Sikupata shida saana na masomo ya pale kwa kuwa nilitoka ktk shule ya English medium, hivyo nikawa nafanya vizuri ktk masomo yangu. Baada ya wiki moja ya masomo yangu nikaitwa office kwa mwalimu mkuu.
Uzuri wale rafiki zangu wa Dogodogo center walikuwa pamoja na Mimi, hivyo walikuja kunisaidia kutoa maelezo ya uongo, mwisho tukaambiwa turudi Darasani.
Hivyo tangu siku hiyo nikawa ninaamani kubwa shuleni nikawa Niko huru Zaidi.
Nilisoma kwa utulivu, nikitoka shule napitia K/Koo kusaidiana na Ndugu yangu Bruno kuuza mifuko.

Lkn bahati mbaya mwaka 2002 nikiwa Darasa la 6, Ndugu yangu Bruno aligongwa na gari na kufariki dunia
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi tukiwa tunazunguka kutafuta ridhiki yetu ya kila siku.
Tulikuwa maheneo ya Mnazi mmoja makutano ya Barabara ya Lumumba na Uhuru Road.
Kunamtu alikuwa anaitaji sigara, hivyo Ndugu yangu Bruno Rest in peace my Brother alikuwa anavuka ili akamuuzie, bahati mbaya Kuna gari ya mchanga ilikuwa inatokea uhuru road inaelekea posta hivyo lilimponda Ndugu yangu Bruno na kumsaga
Kilichotokea baada ya kushuhudia ile ajali, ila nilizinduka siku ya 3 nikajikuta Niko Muhimbili hospital.
Baada ya wiki mwili wa Ndugu yangu Bruno ulizikwa na askari wa jiji makaburi ya jiji ilala.

Baada ya kifo cha Bruno, nikajikuta nimeacha shule, na kwenda kushinda mtaani.
Nikaanza kushinda na watoto wa Dogodogo center kule maheneo ya feri.
Nami nikawa kama chokoraa.
Kule Feri nilikutana na Brother super star wakipindi kile kwa Sasa Ni marehemu John Mjema, pamoja na Eribarick Minja- Ney wa Mitego.
Maisha Yale ya niliyazoea na kuyachukulia Ni sehemu yangu,
Ila nilikuwa namuomba MUNGU kila siku aweze kutimiza kusudi la uumbaji wake ktk maisha yangu
Sikutamani kujiingiza ktk makundi ya uovu japo ninakaa ktkt ya uovu na uharibifu.
Sikupenda kujiingiza ktk ulevi wa kitu cho chote.
Nilikuwa nakumbuka saana maneno ya marehemu mamaangu Yustar,
Alikuwa anasema "mtu yeyote anayevuta sigara na kutumia vilevi Ni mfuasi wa shetani, hivyo upendo wa MUNGU haupo ndani yake"
So nilikuwa naogopa saana kujiingiza ktk mambo hayo, nikawa najitahidi kuyaepuka kwa NGUVU zangu zote.
Na kwa msaada wa MUNGU nimefanikiwa kutoka maisha ya mtaani bila kutumia ulevi wa ainayeyotee

Nilitoka maisha ya Mtaani mwaka 2013 baada ya kukutana na waandishi wa Habari wa Cloud's fm, wa kipindi cha Njia Panda.
Shukrani nyingi ziwafikie kaka mkubwa Dr Isaac Maro, kaka Amani Siri & my Brother Douglas Pius aliyekuwa anakesha usiku na mchana kunirecord na ku-edit kwa sababu ya kigugumizi Changu nilichokipata kutokana na matatizo ya dunia
Huo ndo ulikuwa mwanzo wa maisha mapya ya kuifikia ndoto yangu kwa upya
Wasikilizaji na wadau wa Cloud's Media walinichangia nikapata kupanga nyumba, na hapo ndipo nikapewa wazo la kuandika kitabu ili kiwe funzo kwa wengine.
Namshukuru saana MUNGU alinifanikisha kunitutanisha na watu sahihi wakati sahihi.
Kwa mara ya Kwanza mwaka 2014 nilikutana na Boss Ruge.
Alinitia moyo na kuahidi kunisaidia kila napokwama. Pia alinikutanisha na Madam Miriam Mahanyu, aliyekuwa mkurugenzi msaidizi wa Ewura, pamoja na Madam Professor Agnes Godfrey Mwikaje wa UDSM. MUNGU hakuishia hapo, mwaka 2015 mwishoni alinikutanisha na Madam Selina Koka, aliyenisaidia mambo mengi.
Mwaka 2016 alinikutanisha na kaka mkubwa Mr Mahesh Bollisha.

Wote walifanyika Baraka kubwa ktk maisha yangu.
Hapo ukawa mwanzo wa kuandikwa kitabu Changu kinachoitwa MAISHA HALISI ya MTOTO wa MTAANI..
Kitabu kilikamilika mwaka 2017 hivyo tukaanza kujiandaa na uzinduzi ambao haukufanikiwa kufanyika kwa sababu wakati tunaendelea na uhandishi wa kitabu kunamtu alinifata kunishawishi tufungue taasisi ya kijamii.
Hii yote ilitokana na alivutiwa na simulizi ya maisha yangu hivyo akawa ananionea Huruma akisema tukianzisha taasisi utakuwa umetoa elimu kwa watu wengi zaidi, kumbe bila kujua huyu mtu alikuwa na kusudi la kisiasa, hivyo alikuwa anahitaji mlango wa kutokea.

Nilimshirikisha Boss Ruge lkn alikataa akasema "Yustar, Achana kukaa na matapeli, hao wanataka tu kukutumia badae watakudump wakishafanikisha malengo yao".
Najuta sikuusikia ushahuri wake, alichoongea ndicho kimetokea.

Tulianzisha taasisi ya (James Foundation) na bwana Leonard Tungalaza Manyama akiwa Kama mwenyekiti wetu. Lengo la taasisi Ni kutoa Elimu ya Malezi Bora ktk Family.
Kauli mbiu ilikuwa Ni ( Usitoe Mimba ;Usitupe Mtoto.) Ili kupunguza ongezeko la watoto wa MTAANI. Mara ya Kwanza tulianza vizuri kufanya mikutano, tukawa tunaharikwa kwa vyombo vya Habari.
Baada ya kuona mafanikio hayo mwenyekiti akaamua kubadilisha muhelekeo na kuanza kufanya mikutano ya kisiasa. Sasa kila tukipanga kufanya uzinduzi mwenyekiti analeta Habari tofauti.
Mwisho siasa zikakolea kwa mwenyekiti hivyo niliamua kujitoa rasmi kwenye taasisi hiyo.

Boss Ruge aliniita na kunipanga kuhusu uzinduzi wa Kitabu.
Lkn kwa bahati mbaya alianza kuumwa mwisho wa siku yametokea yaliyotokea Rest in peace Boss Ruge. Tutaonana baadae

Baada ya msiba wa Boss Ruge mipango iliharibika, maana tulipanga kufanya tamasha ktk msimu wa kuazimisha miaka 20 ya Cloud's Media.

Hii Ni sehemu ndogo tu'ya simulizi ya maisha yangu.
Lengo la kueleza hayo yoote, Ninashida nahitaji kazi ya kufanya.

Wakuu mdogo wenu Sina kazi, nimechoka kuishi maisha ya kuunga-unga.
Hali yangu kiuchumi sio nzuri kabisaa
Nahitaji msaada wenu ili niweze ku-move mbele kuifikia ndoto yangu.
Kielimu nimesoma mpaka form 5,
Maana nilipokuwa mtaani nilikutana na dada mmoja wa kizungu aliyekuwa anafanya kazi British council, huyo dada nilikuwa namuoshea gari lake kijiweni kwetu mtaa wa Shaban Robert na Garden Avenue, hivyo alinisaidia kujiunga na British council kusoma computer na English course.
Nilifanya vizuri ktk masomo na hivyo nilimfurahisha yule dada wa kizungu, akanilipia kwenda kusoma QT.
Hivyo nilisoma QT kinondoni vijana nilibahatika kufaulu kidato cha 4 yule mzungu alizidi kufurahi alinilipia Tena kwenda kusoma kidato 5 jitegemee.
Wakati wote nikiwa nasoma nilikuwa nalala nje Kama vijana wenzangu wa mtaani.
Lkn ikatokea matatizo yule mzungu aliondoka kwao na hivyo ilinilazimu kuacha shule.

Hivyo wangugu mdogo wenu natafuta kazi yeyote halali ya kufanya, ili niweze kufikia ndo yangu.

Kwa Sasa naishi kinondoni B , Dar es Salaam.
Sina kazi, ila Ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili.
Nimefanikiwa kurecord Album 1, natafuta pesa ya kufanya videos ya Nyimbo zangu ili nifanye tamasha la uzinduzi wa Album hiyo.
Nahitaji kupata kazi yeyote wapendwa WaNgU.
Nahitaji kazi yakujishikiza kwa muda mchache tu' maana ninategemea mwezi wa kumi na 12 nitaingia mkataba na wazungu flani wa kijerumani mkataba wa matangazo ya Billboard & Mabango ya barabarani.

Yoote ktk yoote Ndugu zangu napitia ktk kipindi kigumu saana kwa Sasa, nadaiwa Kodi ya nyumba, na Sina hata pesa ya kula.
Nimechoka kuwa ombaomba, Hali ilivyo ngumu hata mtu wa kumuomba hayupo kwa Sasa
Nawaomba saana Ndugu mnisaidie mdogo wanu.

Kwa yeyote aliyetayari kunisaidia
Mawasiliano yangu Ni 0657 579 300
0757 698 500.

Natarajia kupata mrejesho mwema toka kwenu Ndugu ZaNgU.
Kiasili me Ni mcheshi napenda story. View attachment 1162125
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom