Ya WAMA na EOTF

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
1,225
Tujadili hizi taasisi zinazosimamiwa na wake za marais. .....

Mama Anna Mkapa alianzisha
EQUAL OPPORTUNITY FOR ALL TRUST FUND (EOTF)

Mama Salma Kikwete kaanzisha
WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA).

Ni taasisi ipi unadhani ili saidia kupambana na changamoto za kina mama hp nchini km ilivyokusudiwa ...

Karibuni kwa mjadala.....
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,524
2,000
Mimi nadhani huko tunakoelekea hizi taasisi zinapaswa kuunganishwa na kuwa moja na mke wa rais awe kama mdhamini wake tu. Tumeshuhudia Mama Mkapa akitumia taasisi yake kujitajirisha kwa kukusanya michango isiyojulikan idadi yake in rhe sense kwamba hakun taarifa alikusanya au kupewa kiasi gani na nchi za nje. Vivyo hivyo Salma Kikwete. Kuna watu wanafikiri kuwa hii inawapa first ladies nafasi ya kujitajirisha. Otherwise akija first lady mwingine naye ataona dili la kuanzisha taasisi yake na hakutakuwa na mwisho wake.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,193
2,000
Taasisi hizo ni mali ya WAKE WA VIONGOZI NA NDUGU ZAO , tafuta mwanamke yoyote kijijini kwako aliyewahi kufaidika na mifuko hii , huwezi kumpata !
 

Vitaimana

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
3,542
2,000
Taasisi hizi za kikuda tu! Mbona wanawake wengi bado wapo kwenye wimbi la shida na mateso na hawajasaidika? Kwanza zinzvyooperate kimjini mjini tuu vijijini sijaona utekelezaji wa aina yeyote utamkuta mwanamke ana mzigo mkubwa sana kimaisha na mapito mengi sihjaona huruma ya hawa wataasisi kifupi wanajisaidia wenyewe tu.
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Huyu mama no 2 huwa nikimwona anaongea kwenye tv nashindwa kabisa kumsikiliza kama vile yupo darasani anafundisha vile
 

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,903
2,000
Huyu mama no 2 huwa nikimwona anaongea kwenye tv nashindwa kabisa kumsikiliza kama vile yupo darasani anafundisha vile

Kuna haja ya kuwa na majukumu maalum yanayomhusu mams wa kwanza kwa mujibu wa sheria. Ofisi ya mama wa kwanza iundwe kuratibu shughuli zake na rasilimali watu wawe sehemu ya utumishi wa umma.

CAG awe na wajibu wa kuikagua ofisi hii....marufuku kuanzisha haya ma mifuko labda baada ya mumewe au mkewe kufika ukomo wa kushika ofisi ya uraisi.

Mama wa kwanza awe ni kiongozo wa heshima wa hii ofisi ....asiwe na mamlaka ya kuratibu shughuli za kila siku za ofisi hii.
 

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
1,195
Taasisi ya mama mdogo naona inawajali sasa kina mama wa upande ule...........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom