Ya Urusi mmeyasikia?

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
207
Rais mpya wa Urusi, Bw Medvedev anakusudia kumteua rais anayemaliza muda wake Vladimir Putin kuwa waziri wake mkuu. Yaani baada ya kuwa rais kwa miaka minane, Putin anarejea serikalini kama waziri mkuu! Hapa wakubwa protokali imekaaje, aliyekuwa bosi atashuka kweli hiyo ngazi, au ndio amebadilishiwa tu jina la cheo lakini bado ni rais?

Pana mafunzo mengi hapa, hebu tuyatizame. Na ninayo hofu fulani, mafisadi ya kwetu yakigundua hii mbinu si ndio yatakaa madarakani milele? Unakuwa rais miaka 10, awamu ijayo unakuwa waziri mkuu 10 years, tena unarudi kama makamu wa rais 10 years nyingine! Hii ya warusi tuitupie macho wakubwa!
 
Rais mpya wa Urusi, Bw Medvedev anakusudia kumteua rais anayemaliza muda wake Vladimir Putin kuwa waziri wake mkuu. Yaani baada ya kuwa rais kwa miaka minane, Putin anarejea serikalini kama waziri mkuu! Hapa wakubwa protokali imekaaje, aliyekuwa bosi atashuka kweli hiyo ngazi, au ndio amebadilishiwa tu jina la cheo lakini bado ni rais?

Pana mafunzo mengi hapa, hebu tuyatizame. Na ninayo hofu fulani, mafisadi ya kwetu yakigundua hii mbinu si ndio yatakaa madarakani milele? Unakuwa rais miaka 10, awamu ijayo unakuwa waziri mkuu 10 years, tena unarudi kama makamu wa rais 10 years nyingine! Hii ya warusi tuitupie macho wakubwa!

Putin amekolea na pesa ya mafuta na sasa hataki kuachia ngazi. Nani aachie ngazi wakati oil imefikia dola 120 kwa pipa? Naona Mugabe watu kama hawa wanampatia push ya nguvu kuendelea na uongozi kule Zimbabwe!
 
putin ndiye aliyemuweka madarakani medvedev kwa sababu alitaka kuendelea kubakia mdarakani. vinginevyo medvedev uraisi angeusikia redioni tu.

hii ni njia nzuri sana ya kbakia madarakani, na si dhani kama ni kinyume na katiba hata hapa tanzania.

huu ni mchakato mzuri kwa mafisadi. na wafanye tuwaone
 
Iam sorry to say, but in the quest for democratization, we third worlders..we have NOTHING to learn from the East..be it China or Russia (with the exception of India maybe). Yaani hapo ndo na undava na unazi wao woooote..nawaheshimu wamarekani! wamejijengea misingi ambayo kwa kweli ni fundisho la kudumu kwa mataifa mengine! Yaani hapo western countries ndo zinatupiga bao la nguvu. wanajua power corrupts-absolutely and as such kila mtu anamchunga mwenzake..kwenye madaraka hakuna utani! ni maslahi ya nchi kwanza mengine yatafuta... Putin ni another corrupt folk tuu..hana jipya...
 
I am trying to imagine things out, with all what folks are now saying about JK et al, suppose after relinquishing the presidency JK remains as Pinda's PM? I'm just thinking aloud because these guys are watching this and it might sound as a sweet lesson for them! Or suppose Mkapa was Kikwete's PM, who would have been the de facto president?

There could be (apparently) nothing wrong with ex-president becoming new PM, actually I think this might taste better than the Eyadema issue of succession through a family lineage, but doesn't it render the whole idea of "fixed term" presidency utterly senseless then?
 
Vladimir Putin anairudisha Russia kwenye neo-communism, complete with a personality cult and a huge difference between the haves and have not.

World is he is waiting for one term as PM then he will legally be able to run for the Kremlin again, the new presidaa is just keeping the seat warm for Mr. Putin.
 
Rais mpya wa Urusi, Bw Medvedev anakusudia kumteua rais anayemaliza muda wake Vladimir Putin kuwa waziri wake mkuu. Yaani baada ya kuwa rais kwa miaka minane, Putin anarejea serikalini kama waziri mkuu! Hapa wakubwa protokali imekaaje, aliyekuwa bosi atashuka kweli hiyo ngazi, au ndio amebadilishiwa tu jina la cheo lakini bado ni rais?

Pana mafunzo mengi hapa, hebu tuyatizame. Na ninayo hofu fulani, mafisadi ya kwetu yakigundua hii mbinu si ndio yatakaa madarakani milele? Unakuwa rais miaka 10, awamu ijayo unakuwa waziri mkuu 10 years, tena unarudi kama makamu wa rais 10 years nyingine! Hii ya warusi tuitupie macho wakubwa!

Mkuu,

Kulifanyika "maneuvers" ya hali ya juu ili Putin awe na mrithi wa kiti chake cha uraisi.

Hii inamaanisha kwamba Putin ataendelea kufanya mambo yote yanayohusu Russia hususan uchumi ambao umekuwa "boosted" na mafuta.

Ila Dmitrii Medvedev alikuwa ni naibu waziri mkuu kwa hio Putin Alikuwa anajua atamnadi pale bungeni Duma.

Lakini kwa mtazamo wangu, mambo haya hufanyika katika nchi ambazo zina harufu za UFISADI na mambo mengine ya uzandiki.
 
Putin ana uroho wa madaraka. Tumekuwa tukisikia tuhuma ambazo zimekuwa zikimlenga yeye moja kwa moja jinsi anavyo wa-deal watu ambao walikuwa wanatishia kitumbua chake. Mie binafsi sijui katiba ya Russia lakini jamaa alivyo Mafia anaweza kum_KOLIMBA Rais wake kisha yeye akarudi tena kwenye kiti chake. Tunajua wazi kuwa nchi itakuwa inaongozwa under his SHADOW, si ajabu tofauti itakuwa ofisi tu.
 
Kinachoniogopesha ni jinsi viongozi wetu (Afrika) wanavyopenda kuiga ya Ulaya, na sisi tujiandae baada ya miaka 3 au 4 ijayo,. Afrika itakuwa na viongozi "type" ya Putin kibao tu!
 
Hayo ya Putin mbona mapya..unatoka Urais unarudi PM?tena PM mwenye madaraka..makubwa kuliko ...Rais sasaa..maana ukisikiliza aliyoahidi ...ni kama yeye ni Pres ........sasa Pres hana kazii ...nafikiriaa wanaogopa na bado wana mawenge ya vita baridi wanajuaa USA watawazidii sana kwenye kila nyanja.......
 
IT is more than that guys. Russia kulikuwa na kina Chenge wengi sana Putin aka-deal nao vizuri sana. Na mali ya Russia imemekwa mikononi mwa viongozi wenye uchungu, na pesa zinabaki Russia na kutumiwa na wa russia.
Putin amekuwa PM kwa sababu katiba haimruhusu kuingia third term mfululizo, kwa hiyo atakuwa PM kwa muda then atakuwa President baada ya Medvedev,
Nawapongeza ni kawaida kwenye baadhi ya nchi mambo kama haya kutokea. Mbona leo Israel Barak ni waziri wa Ulinzi, na Netanyahu yupoyupo tu, possible kwa hali kama hii kutokea.
 
Puttin ni kiboko wa Maekani na ndio mwiba ambao unahitajika kuwepo karibu na Uongozi mkuu na kwa kiasi fulani amefanikiwa kuiendeleza Urusi kutoka kwenye dimbwi la kijeshijeshi na kuingia katika soko huria la utanda wazi ,hivyo kiongozi akiwa bora inafaa kumtumia na kwa kweli hakufanya kasheshe yeyote ya kutaka kubadilisha katiba kuwa Raisi aweze kugombea tena kwa muhula mwingine ,ameondoka Uraisi na amechaguliwa kuwa Waziri Mkuu inaonyesha wazi Warusi wameridhika na utendaji wake ,yaani ni Uongozi mzuri ndio wanahitaji wananchi ,haina maana ukiondoka Uraisi huwezi kushika nafasi nyengine ,nahisi hata mtu baada ya kumaliza muhula wa miaka kumi anaweza kuishi miaka mingi mingine na anaweza kabisa kurejea katika Uraisi ikiwa tu ni kiongozi mchapa kazi ambae alisababisha maisha bora kwa kila raia kitu ambacho walala hoi wengi ni ndoto ,hivyo akitokea mtu atakaewawezesha basi hata akiwepo miaka mia kwenye kiti cha Uraisi hakuna taabu ila mafisadi hili hawalitaki wanataka wapate Uraisi waanze kukoromea mali za Taifa wakimwacha mpiga kura akipiga miiayo.
Kuna nchi viongozi wake ni wezi au mafisadi wa kutupwa lakini ufisadi wao huwezi kuugundua maana nchi inajengwa na raia hana shida ,bara bara hazina mashimo ,maji hayana shida,huduma za afya ni za kuchagua hii naitaka hii siitaki,usafiri kila aina umeme 24hrs unalipa kwa bei poa ,Mwananchi wala hashughuliki nakusaka wizi unaotokea erikalini maana ameridhika na hana dhiki ya aina yeyote.
Lakini Tuchukue hili Taifa letu shida na dhiki kila pembe halafu hawa viongozi tunaowapa kura wakiishika serikali wanaichomoa kila kitu ,kujaza matumbo yao tu hawana habari na raiaalieko kijijini ambae alimtembelea kumwomba kura na kumuahidi maisha bora ,so far yako wapi maisha bora ? Hakuna zaidi ya kuzidi kwa shida kila kukicha.
Kwanza tengenezeni nchi muiondoe katika dimbwi la umasikini na kuhakikisha ahadi mlizozitoa zote mmezitimiza na kumwekea matumaini mwananchi yeye na kizazi chake ,tena hapo itapatikana extra ambayo mtajua namna ya kukatiana bila ya kuathiri maendeleo ya Nchi.Hivyo ndivyo wakuu wanavyokula katika hizo nchi zilizoendelea.
 
Mwanamalundi,

That is what the resourceful international press is asserting.
 
NI mwanasiasa ambaye maisha yake yamegubikwa na usiri mkubwa. Wapinzani zake wamejaribu kuchokonoa ili kupata chochote watakachokitumia kama silaha katika kampeni zao za uchaguzi wa urais nchini Urusi, bila mafanikio.

Hata watu wake wa karibu, wameishia kumfahamu kijuu juu, ingawa wanakiri upole wake, kutokuwa na majivuno, mchukiaji wa rushwa na sifa nyinginezo nzuri tu, achilia mbali ile moja hasi inayotawala hivi sasa wakati akielekea kuikwaa nafasi ya juu zaidi ya Taifa linalojaribu kurudisha heshima na ubabe wake kama ilivyokuwa wakati wa Vita Baridi, lilipokuwa likishindana na Marekani.

Aidha, kwa watu hao wanaomjua Dmitry Medvedev wanamwelezea kuwa mtu mwenye akili na mchapakazi makini katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Lakini je; anayo sifa ya kisiasa ya kuweza kuwa Rais mpya ajaye wa Urusi? Ni swali linalosumbua vichwa vya wengi, huku wadadisi wengi wa mambo wakitabiri chini yake, Urusi itaongozwa kwa ‘remote control' ya Rais wa sasa, Vladimir Putin.

Anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais utakaofanyika Jumapili wiki hii, ubashiri uliotolewa tangu mshirika wake wa karibu na wa muda mrefu wanayetoka eneo moja, Rais Vladimir Putin, alipompitisha awanie kuchukua nafasi yake mwaka jana.

Akiwa ameibuliwa na Putin kutoka kusikojulikana, haiba na sifa binafsi za Medvedev zinaelezwa kuendana na malengo ya Putin, anayehitaji mshirika mtiifu na wa uhakika katika kutimiza dhamira yake ya kuendalea kuiweka Kremlin (Ikulu ya Urusi), katika kiganja chake hata baada ya kumaliza muhula wake wa urais.

Rais Putin pamoja na kuchukiwa na nchi za magharibi, lakini zinakiri kwamba anao umaarufu mkubwa nchini mwake kutokana na sababu kadhaa, zikiwamo kurudisha heshima ya nchi kimataifa, kufanikiwa kufufua uchumi wa nchi hiyo uliokufa baada ya kumeguka kwa uliokuwa Umoja wa Nchi za Kisovieti (USSR) mapema miaka ya 1990 na kadhalika.

Kwa kutumia umaarufu huo, ambao imefikia kiasi cha baadhi ya Warusi kutaka awanie tena urais ili aweze kutimiza azma zake, hususan heshima na ushawishi wake wa huko nyuma, Rais Putin badala ya kuwania mwenyewe, ameamua kuheshimu Katiba ya nchi yake, akitegemea kutumia mlango wa nyuma kuliongoza Taifa hilo, ikiwamo kutarajia cheo cha uwaziri mkuu.

Aidha, Putin anaelezwa kulenga kurudia urais baada ya muhula wa Medvedev utakapoisha miaka minne ijayo kutokana na Katiba ya Urusi kuruhusu.

Baadhi ya washirika wa zamani wa Medvedev waliohojiwa na kuomba kutotajwa majina yao, pamoja na kukiri juu ya uwezo, umahiri, uadilifu na ujanja alionao Medvedev, uwezo wa kujijengea mamlaka yake mwenyewe, bado una utata.

"Dima ni mjanja. Mjanja vya kutosha kuwa Rais, na ni imara, imara vya kutosha kuwa Rais," anasema mmoja wa washirika wake wa enzi za miaka ya 1990, wakati akiliambia Reuters kwa masharti ya kutotajwa.

Anaendelea: "Lakini uwezo, hisia za kikachero, uwezo wa kutoa maamuzi pale Kremlin, Rais Putin alibarikiwa nayo, kama ilivyokuwa kwa Rais wa zamani, Boris Yeltsin. Je; Dima? Hilo sijui lakini wacha tuone." Dima ni kifupi cha jina Dmitry Medvedev.

Iwapo atashinda uchaguzi huo, Medvedev mwenye umri wa miaka 42, atakuwa kiongozi kijana zaidi wa Urusi tangu mtawala wa mwisho wa nchi hiyo, Tsar Nikolai II.

Aidha, atakuwa kiongozi wa kwanza wa Urusi anayetoka katika sekta binafsi ya biashara.

Kulinganisha na Rais Putin, kachero wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Urusi (KGB), ambaye anatuhumiwa kurudisha nyuma demokrasia, Medvedev, mwanasheria wa zamani wa nchi hiyo, anasisitiza umuhimu wa uhuru na sheria.

Aidha, ameifurahisha sekta ya masoko wakati aliposema anataka kuweka ukomo kwa Kremlin kujishughulisha katika makampuni makubwa.

Lakini zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya uchaguzi wa urais, maisha binafsi ya Medvedev yamebakia kuwa siri.

Mtu ambaye mwenyewe binafsi husema anajiweka wazi kwa umma, ndiye huyo ambaye upande wa pili wa kampeni hauna kitu chochote cha kumhusisha juu ya tabia na historia yake.

Amekataa kushiriki katika mijadala ya televisheni, na ni mara moja tu alifanya mahojiano ya moja kwa moja kama sehemu ya kampeni zake.

Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi, Mikhail Kasyanov, enzi zile Medvedev akifanya kazi katika ofisi ya Putin, Kremlin, alijalibu kujitutumua kumshambulia Medvedev akisema:

"Hana lolote. Ni mmoja wa wale wafanyabiashara warasimu tulio nao." Kasyanov, ambaye ameondokea kuwa mkosoaji mkali wa Kremlin baada ya kufukuzwa uwaziri mkuu mwaka 2004, anajitutumua akisema hoja ambayo haina uzito wowote mbele ya wengi.

Hata wafuasi wa Medvedev, hawana mengi ya kumhusu. "Ni mtu mzuri, mtu mzuri tu," kilisema chanzo kimoja cha habari kilichopo karibu na Kremlin na kuongeza: "Hufanya kila anachoona chema kwa uangalifu."

"Ni mpenda utamaduni mno. Unaweza kumzungumzia kuhusu maonyesho ya sanaa za utamaduni na muziki," anasema Nataliya Rasskazova, ambaye alisoma na Medvedev katika kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Petersburg, ambacho pia alisomea Putin.

"Hajabadilika. Nilimuona mwaka mmoja uliopita, na hana majivuno, hana ubwana mkubwa wala fahari," alimwagia sifa.

Medvedev alifundisha sheria baada ya kuhitimu masomo yake, kabla ya kwenda kufanya kazi kwa Putin, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya masuala ya Nje, chini ya Meya wa Mji wa Mtakatifu Petersburg.

Ni katika kipindi hicho pia Medvedev aliingia rasmi katika anga za biashara. Alifanya kazi kama mwanasheria muhimu wa Kampuni ya Ilim Pulp, akisaidia wakati wa mchakato wa uanzishaji wa kampuni hiyo, ingawa wafanyakazi wenzake wa wakati huo wanasema, hakuwahi kutendewa sawa sawa na wamiliki wa kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ya mbao, kwa sasa imeibukia kuwa moja ya makampuni makubwa yanayoongoza katika sekta hiyo ya biashara nchini Urusi, ikiwa na imewekeza mabilioni ya dola za Kimarekani.

"Alipata mshahara na wakati huo, akawa mfanyabishara kamili katika miaka 1990," anasema mmoja wa wafanyakazi wenzake wa zamani.

Wafanyakazi wake wa zamani wanasema Medvedev, hakuwa mtu wa kawaida linapokuja suala la uadilifu. Aliepuka kutoa rushwa, na alikuwa tayari kuona kampuni yake inapoteza kesi mahamani hata kama itaigharimu kampuni, kwa sababu hakuwa tayari kumpatia hongo hakimu.

Maisha ya awali ya Medvedev. Dmitry Anatolyevich Medvedevlisten, alizaliwa Septemba 14, 1965 katika kitongoji cha Leningrad, akitoka katika familia ya walimu wa chuo kikuu, na alikulia katika kitongoji hicho hicho, kilichoko mjini Kupchino.

Alimaliza masomo yake ya sheria katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Leningrad mwaka 1987, akiwa na kina Ilya Yeliseyev, Anton Ivanov, Nikolay Vinnichenko na Konstantin Chuychenko, kabla ya kujipatia Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sheria mwaka 1990, katika chuo hicho hicho.

Anatoly Sobchak, aliyekuwa mmoja wa wanasiasa wana demokrasia wa mwanzo nchini humo, na hasa katika miaka ya 1980 na 1990, alikuwa mmoja wa maprofesa wake, kabla ya Medvedev baadaye kushiriki katika kampeni zilizofanikiwa, za Sobchak, kwa kuukwaa Umeya wa Mji wa Jiji la Saint Petersburg.

Mwaka 1990, alifanya kazi katika Manispaa ya Leningrad, kabla ya mwaka kati ya 1991 na 1999, kufanya kazi katika Chuo Kikuu cha Leningrad, sasa Chuo Kikuu cha Taifa cha Saint Petersburg kama mwalimu wa sheria.

Aidha, kati ya mwaka 1991 na 1996, alifanya kazi kama mtaalamu wa sheria katika Kamati ya Uhusiano wa Kigeni, katika Ofisi ya Meya wa Mji wa Saint Petersburg, iliyokuwa chini ya Putin.

Novemba 1993, Medvedev alifanywa kuwa Mkurugenzi wa masuala ya Sheria wa Kampuni ya Ilim Pulp Enterprise, kampuni inayojishughulisha na ununuzi na uuzaji wa mbao katika jiji la St. Petersburg.

Mwaka 1998, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kiwanda cha Karatasi cha Bratskiy LPK.

Kuiingia katika siasa Novemba 1999, Rais huyo mtarajiwa wa Urusi, alikuwa mmoja wa watu kutoka St. Petersburgers, walioletwa na Putin kushika nafasi za juu serikalini.

Desemba mwaka huo huo, aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Watumishi wa Rais, Ikulu, kabla ya kuwa mmoja wa wanasiasa walio karibu na Rais Putin, na hata wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000, alikuwa Mratibu Mkuu wa Kampeni za Rais, akiwa makao makuu.

Kuanzia mwaka 2000 hadi 2001, Medvedev alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Gazprom, kabla ya kufanywa Naibu Mwenyekiti, kati ya mwaka 2001 na 2002.

Juni 2002, Medvedev alifanywa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Gazprom kwa mara ya pili, kabla ya Oktoba 2003, kuchukua nafasi ya Alexander Voloshin, kuwa Mnadhimu Mkuu wa Watumishi Ikulu.

Novemba 2005, aliteuliwa na Rais Putin kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu, Naibu Mwenyejkiti wa Kwanza wa Kamati ya Utekelezaji wa Miradi ya Kipaumbele ya Taifa ya Shirikisho la Urusi, na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utendaji.

Akiwa mtu mtaratibu, Medvedev anahesdabiwa kuwa Mliberali wa kisasa, mwenye nadharia ya vitendo, mtendaji mahiri na mfuasi mtiifu wa Putin.

Aliteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Urusi, Novemba 14, 2005, kabla ya Desemba 10, mwaka jana, kupitishwa kuwa mgombea urais wa Chama Tawala cha Urusi, cha United Russian, na uteuzi wake rasmi ulifanywa wiki moja baadaye, Desemba 17.

Kugombea kwa Medvedev katika nafasi hiyo ya urais kunaungwa mkono na Putin mwenyewe pamoja na vyama vingine washirika.

Taasisi Huru ya Urusi, ya Levada Center, iliendesha kura ya maoni kati ya Desemba 21 na 24, mwaka jana, maoni ambayo yameonyesha kwamba asilimia 79 ya Warusia, wako tayari kumpigia kura Medvedev, iwapo uchaguzi ungefanyika wakati huo.

Zaidi ya kuwa mwanasiasa mteule, mfanyabiashara na mwanasheria, Medvedev hajawahi kushiriki na kuchaguliwa katika madaraka yanayohitaji uchaguzi.

Akiwa tayari kushiriki, anatarajia kuachia ngazi uenyekiti wa Gazprom, kwa sababu katika sheria ya sasa nchini humo, Rais haruhusiwi kushika wadhifa mwingine katika taasisi yoyote ile.

Vyanzo vilivyo karibu na kampuni ya Gazprom na Medvedev, vililiambia gazeti la Vedomosti kwamba nafasi ya Medvedev, huenda ikashikwa na Putin katika kampuni hiyo.

Aidha, Medvedev, alipitishwa rasmi kuwa mgombea halali wa urais na Tume ya Uchaguzi ya Urusi, Januari 21, mwaka huu.

Kama ilivyovumishwa kwa muda mrefu, mara baada ya kupitishwa kuwania urais, Medvedev alitangaza kwamba akiwa Rais wa Urusi, atamteua Putin katika wadhifa wa uwaziri mkuu.

Ingawa anazuiwa na Katiba kuwania urais kwa muhula wa tatu mfululizo, wadhifa kama huo wa uwaziri mkuu, utamruhusu Putin kuendelea kuwa Rais wa kitaifa, na Katiba pia itamruhusu kurudi katika urais iwapo atapenda hapo baadaye.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kwamba kauli ya Medvedev, ya kumteua Putin kuwa Waziri Mkuu, inaonyesha namna atakavyokuwa kama ‘Rais pambo tu.'

Ingawa Putin ameahidi kutobadilisha mamlaka kati ya Rais na Waziri Mkuu, wachambuzi wengi wanategemea madaraka mengi kuinuliwa kutoka urais kwenda uwaziri mkuu, iwapo Putin atapewa wadhifa huo chini ya urais wa Medvedev.

Jambo jingine muhimu kwa Medvedev, ni kwamba Desemba 2005, aliteuliwa na Expert Magazine, kuwa Mfanyabiashara Bora wa Mwaka. Hilo ni gazeti maarufu linaloheshimika kibiashara nchini humo, linalochapishwa kila mwezi.

Alitwaa Tuzo hiyo sambamba na Alexei Miller, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Gazprom.

Medvedev ni baba wa familia yenye motto mmoja wa kiume, Ilya, aliyezaliwa mwaka 1996 kwa mkewe Svetlana Vladimirovna Medvedev. Kabla ya kuoana wawili hawa walikuwa marafiki wakati wa utotoni, wakiwa shuleni.

Walioana miaka kadhaa baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1982.

Medvedev ni mmoja wa waandishi wa kitabu kinachoelezea masuala ya sheria ya kiraia kwa vyuo vikuu, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1991, na ambacho kinaheshimika vyuoni na wanafunzi wengi wa kiraia.

Aidha, ni mwandishi wa kitabu cha vyuo vikuu kijulikanacho kama Questions of Russia's National Development, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, kuhusiana na jukumu la Taifa la Urusi katika sera za maendeleo ya uchumi na jamii. Aidha, ameshiriki kuandika vitabu vingi vingine vya sheria.

Huyo ndiye Dmitry Medvedev
 
kwani jamani hamkumbuki zamani zile kulikuwa na USSR kabla ya kuvunjika na kugawanywa vipande vipande mpaka leo urusi si taifa kubwa kama lilivyokuwa awali?

je mmesahau nini kilisababishha yote hayo?

na mnakumbuka hotuba ya kwanza ya putin alivyoingia madarakani alisemaje?

na mnakumbuka kuwa kuna manuwali iliyokuwa imesheheni wanajeshi wa ngazi za juu katika jeshi la urusi ilzama na wanajeshi hao kupoteza maisha?

sasa mkiyajuwa hayo hamtamdharau tena kamanda huyo kutoka st persbrough vladimir putin.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom