Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,240
- 9,527
WWF (World Wide Fund for Nature) walitoa report mbili tofauti moja ikiandikwa na Barnaby Dye na Nyingine ikiandikwa na Joerg Hartmann juu ya athari zitakazopatikana kutokana na ujenzi wa bwawa la kufulia umeme ndani ya Selous Game Reserve.
Selous game reserve ni world heritage site ambayo serikali yetu iliingia mkataba juu ya namna inavyopaswa kulindwa. Hivyo ujenzi wa mradi wa umeme kwanza kabisa utakuwa kinyume na mkataba huu kitu kitakacholeta hatari ya Selous kufutwa kwenye list ya 'world heritage sites' ambako kutakuwa na athari zake!
WWF wakapendekeza kuwa hili halina lazima kwakuwa kwenye 'Tanzania Power Master plan' kuna miradi mbadala mingine yenye uwezo wa kuzalisha kiasi hichohicho cha umeme kitakachozalishwa na Stiegler's.
Shida ni ile dhana kuwa 'mimi sipangiwi' na dhana ya kutokujali ndio inayofanya tupush huu mradi.
Tujifunze jamani, dereva wetu ameshatuingiza chaka mara kibao tena akiwa na confidence ya kufa mtu;
1.Sukari
2.Mbaazi
3.Makinikia
4.Korosho
N.k
Na kote huko anachomokaga na gia nyepesi ya 'UZALENDO'.
Mradi huu wa Stiegler's utaathiri utalii ndani ya Selous unaotegemewa na raia zaidi ya laki mbili na athari nyingine kedekede kwenye ecosystem!
Sasa badala ya kumuita Gwajima Ikulu ili aongelee habari ya mayai ya kuku na chipsi za viazi mviringo nadhani tungewapa kazi wataalamu wetu kuandaa research itakayoonyesha kuwa au hayo WWF wanayotushauri ni uongo au faida za mradi wa Stiegler's zitakuwa kubwa mno kulinganisha na athari zinazotajwa na WWF.
Tuache siasa za bei rahisi kwenye masuala ya msingi!