Ya Sankara, Compaore, Kikwete na Lowassa

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
YA COMPAORE , SANKARA, KIKWETE NA LOWASA!

Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas sankara na blasius compaore, walipindua serikali ya rais wa wakati huo katika nchi iliyojulikana kama upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo.

Vijana hawa wakiwa katika fikra za kimax, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, manake nchi ya watu, country of honorable citizen. Uchapa kazi wa vijana hawa , Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa ari mpya, kasi mpya, kabla haujachuja. Haiyumkini sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake compaore wakiwa kama pete na kidole.

Urafiki wa makapteni hawa ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia sankara kuwa compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu mwingine, akaongeza kuwa hata kama compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia. Ni wazi kuwa sankara alikuwa mno karibu na compaore,kwa kiasi kuwa compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya sankara. kama ilivyotabiriwa, compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha sankara mwaka 1987, na yeye mwenyewe huku akishuhudia rafiki yake kipenzi sankara akiuuwa, Akawa ndo rais.

Kwa kikwete na lowasa, wengi mnaweza kupuuza mfano huu, lakini ukweli ni kuwa katika kuwania madaraka, siyo mara ya kwanza ndugu kwa ndugu kugeukana, licha ya marafiki kwa marafiki kuuana. Ni nani asingependa kupigiwa saluti na mizinga? Hata hivyo binadamu huwa hawatosheki na hatua aliyo nayo kihali na mali bali, angependa ajulikane, aabuduwe nk.

Siku za karibuni, imeskika minongono kuwa, wale wanaoitwa mafisadi, walikuwa wanasuka mipango ili kikwete awe Rais wa kipindi kimoja. . Hata hivyo tetesi hizi zimekuwa zikipata upinzani mkubwa toka serikalini, kana kwamba ni kitu kisichowezekana, wanaodhani kuwa genge la akina lowasa na watuhumiwa wenzake wa ufisadi hawakitamani kiti cha urais, wamesahau kuwa mwaka 1995, lowasa alienda dodoma kuchukua fomu ya kugombea urais, na wala si uwaziri mkuu. Wamesahau kuwa licha ya mwalimu Nyerere kumkataa, alikuwa nyuma ya pazia kwenye mbio hizo 2005, akitegemea kuwa baada ya kikwete itakuwa zamu yake.

Kama alivyowahi kusema zitto kabwe, kuwa lowasa akiwa bungeni kama waziri mkuu, alikuwa anafanya kazi kama vile yuko kwenye kampeni za urais. Hata kuukosa uwaziri mkuu, bado tunaona jitihada zake kupitia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na rafiki zake vikijaribu kumbeba na kumsafisha, wanaosikiliza bunge au kuangalia televisheni walishuhudia, mbunge wa kyela akilalamika wazi kwa swala hili.

Tulio makini na kufuatilia mustakabali wa taifa letu ,tunadhani mienendo ya akina lowasa ni ya kutilia wasiwasi, kwamba kila kashafa inayohusu kupotea kwa mabilioni ya pesa za walala hoi wako, linatutia wasiwasi zaidi. Kama kweli wapo kwenye kashfa hizi, hayo mabilioni wanapeleka wapi? Si kwamba ni maandalizi ya kuchukua madaraka kwa kuiba kura, au kushawishi wapiga kura?

Ni kwa ajili hiyo tunamwomba kikwete asipuuze kabisa habari zilizoandkikwa na gazeti moja wiki hii, kuwa kuna mbinu chafu za kuhakikisha hapiti kipindi cha pili. Rais anaweza kujinasua tu, kwa kutangaza mapambano na mafisadi kwa kuwa wanaotuhumiwa ni wale wale waliohusika na kashfa za kifisadi.

Tunamkumbusha Rais kikwete, kama alivyowahi kutamka mwenyewe kuwa urais wake hauna ubia na mtu isipokuwa makamu wake Dr Shein kuwa ni wakati wa yeye kuonyesha wazi kuwa, urais wake hauna ubia na marafiki zake, au hata familia yake, kwa kuwa tunaambiwa mwanawe wa kumzaa yuko bega kwa bega akiwasaidia mafisadi labda kwa kutumiwa bila kufahamu.

La sivyo! Endapo yatamkuta ya blasius compaore hana wa kumlaumu.



MWIKIMBI M. MWITORI
EMAIL mwikimbi@gamil.com
 
Haya uliyoandika hayana nafasi sasa na bila shaka ni uchochezi tu.
 
Hivi Blaise Compaore bado tu hajanyongwa? Alichomfanyia Capt. Thomas Sankara ni kitendo ambacho hakiwezi kusamehewa.

Haki ya Compaore ni kunyongwa hadharani.

Yanayotokea Burkina Faso ni funzo zuri kwa viongozi wetu wa Afrika Mashari ambao kuna minong'ono kwamba wanataka kubadili katiba zao ili waendelee kukalia madaraka. Wanasema ati waliingia kwa nyundo na wao watatolewa kwa nyundo!!

Gen. Museveni, Gen. Kagame na Pierre Nkurunzinza kuweni makini.
 
Back
Top Bottom