Ya Samatta na Victor Wanyama: A missed opportunity?

VeronicaAmadu

JF-Expert Member
May 4, 2011
310
379
Heshima kwenu wana jukwaa!
Mimi ni mpenda michezo karibu yote, na kama kawa football ni mchezo niupendao sana tangu utotoni, nina upenzi na timu mojawapo kati ya Simba na Yanga kwa hapa bongo, na nina timu EPL, pia nina team huko Spain
Wiki hii nimeshuhudia jambo ambalo ndio limepepelekea mimi kuandika thread yangu ya kwanza tangu nijiunge na JF miaka zaidi 10.
Tumeshuhudia mwanasoka wa kulipwa kutoka Kenya anayechezea Tottenham akija likizo Tanzania. Kiukweli sikua najua mengi kuhusu mwanasoka huyu zaidi ya kuwa ni Mkenya anayechezea England! Lakini baada ya ujio wake, ambao ulifuatia ujio wa wanasoka kadhaa wakubwa duniani ambao wengine walikuja kimya kimya mwezi huu huu, na kutotaka wajulikane wako huku, wengine walionyesha uwepo wao kidogo, na wengine bado wako mbugani kwenye fungate. Cha tofauti ni kwamba huyu Wanyama alikuja moja kwa moja na kuanza kuhojiwa tangu alipotua JKN. Alionekana ni mtu aliyetulia sana hasa kwenye kuongea na kujibu maswali, hata alipoulizwa kuhusu Samata alisema maneno mazuri juu yake na hata kuhusu muziki alisema anasikiliza miziki yetu na haswa anasikiliza nyimbo mpya ya mwanamama Saida Karoli, Orugambo!
Haikuishia hapo, Wanyama aliendelea kuonekana akiwa sehemu tofauti na wadau mbalimbali wa soka, wengine wakimpeleka vijiwe vyao maarufu vya makange, na baada ya hapo kuonekana akiwa Ndondo Cup! Uwepo na ushiriki wake Ndondo Cup kwenye uwanja mmoja huku kwetu Uswazi , na ni mashindano ya level ya mtaani sana, kwangu ilikua ni jambo la kushangaza na kufumbua macho sana! A player of his caliber to participate in such local event Uswazini is something to be commended! He could have been in Zanzibar or Serengeti or Brazil or anywhere in the world, yet here he was somewhere in Manzese watching Ndondo Cup!
Samatta anaingiaje hapa?:
Samatta kama mchezaji wetu ambaye anacheza Ulaya pia na tunamtegemea kufuata nyayo za Wanyama siku moja awepo huko ligi ya England, kiasi nilishangazwa kutomuona wala kumsikia akiwa na Wanyama popote hapa Dar. Kama mwenyeji, just as a good gesture, i was hoping to see them together somehow, i was hoping Samatta would extend a hand and may be invite Wanyama, have a meet up, hang out, which would be more beneficial for Samatta. Wanyama amekuwa akiandikwa na magazeti ya Uingereza kuhusu uwepo wake hapa bongo, na magazeti hayo yangeweza kuposti hizo meetings za Wanyama na Samatta, which would be more exposure for Samagoal, hata huwezi jua washika dau gani wa Ligi ya England wangetaka kujua who Samatta is, na kumfuatilia na who knows kingetokea nini.... Dunia ya sasa ni dunia ya networking. As someone ambae yuko kwenye fani moja nae na amemtangulia mbali, huyo angekua mtu sahihi kwake kutaka kuonana nae. Na kwa jinsi Wanyama alivyo very humble, asingesita kuonana na Samatta! Hata kujenga urafiki.
Mimi binafsi ni shabiki sana wa Samatta na ninamuombea kwa Mungu afike mbali sana, lakini nimeshangaa kwa kutoitumia fursa hii adimu. Narudia tena, networking is the key. Mdogo wangu au mwanangu Samatta, jaribu kujisogeza kwa watu kama hao, hasa inapotokea mtu yupo kwenye mitaa yako, tena ni Mkenya wala sio wa mbali, tunaongea nae lugha moja, nae alianzia Belgium kama wewe, there was so much for you to gain dogo. Nafasi bado ipo, jaribu kumfahamu huyu kijana mwenzio.
Samahani kwa uzi mrefu wana jamvi, karibuni kwa maoni yenye kujenga.
Kila la heri Samatta na pia Jirani yetu Wanyama.
 
"Wiki hii nimeshuhudia jambo ambalo ndio limepepelekea mimi kuandika thread yangu ya kwanza tangu nijiunge na JF miaka zaidi 10"

Mbona umejiunga 2011 halafu unasema una miaka zaidi ya kumi?? wale wa 2007 watasemaje

Back to the topic; Samatta anapambana kiukweli na one day atatoboa tutamuona ligi pendwa ya Uingereza, akazane tu!
 
Nilipoteza my first ID niliyodumu nayo miaka kama miaka minne, baada ya siku moja kunigomea ku log in, ndio nikafungua ID mpya. Asante.
 
Tatizo la Samatta anaringa mnoooo yaani kajikuta Ronaldo vile ,hajichanganyi na watu yeye ni kujifungia tu huko Mbagala kwao .
Nadhani tunamsifu kupitiliza.Hata mimi nilitegemea ataenda kumsalimia hata Sakho kule Zanzibar au Erickson au Wanyama lakini kajifungia tu sijui anawaogopa walina Gigymoney?

Samatta changamka lasivyo Genk watakutoa vietnam kwa mkopo maana sioni jitihada zozote au ukali wowote ulionao hadi team kubwa hata kukuzungumzia kwa bahati mbaya wakati huu wa usajili
 
Katika ubora wako japo tume miss ID yako ya zamani...huyu Samatta ana sifa ya kujiona ni big player kuliko wenzie.
Halafu kuna waongea ujinga kama kina Manara ndo wanaharibu soka letu na hata kuchonganisha watu kwa kudhani watapata sifa fulani kumbe wanajishushia hadhi
 
Mkuu yaweza kuwa kweli tunamsifia sana au kutokua na competition hapa nyumbani ya kumfanya aone bado hajafika kwa vile yeye hapa ndio top player. This was a missed opportunity kiukweli.
 
Huyo Manara nae amekera sana! Ndio maana tuko nyuma sana. Aliyoropoka juzi ni aibu sana!
 
Tatizo la Samatta anaringa mnoooo yaani kajikuta Ronaldo vile ,hajichanganyi na watu yeye ni kujifungia tu huko Mbagala kwao .
Nadhani tunamsifu kupitiliza.Hata mimi nilitegemea ataenda kumsalimia hata Sakho kule Zanzibar au Erickson au Wanyama lakini kajifungia tu sijui anawaogopa walina Gigymoney?

Samatta changamka lasivyo Genk watakutoa vietnam kwa mkopo maana sioni jitihada zozote au ukali wowote ulionao hadi team kubwa hata kukuzungumzia kwa bahati mbaya wakati huu wa usajili
Ni bahati mbaya sana kwa kijana wetu Samatta kuwa na tabia ya upole asiyetaka makuu hata yale yanayomstahili. Wanaomfahamu kiundani tangu akiwa mtoto mdogo wataelewa nisemacho. Ni bora kujitokeza na ushauri wa kumjenga kuliko kumponda.
 
Mkuu yaweza kuwa kweli tunamsifia sana au kutokua na competition hapa nyumbani ya kumfanya aone bado hajafika kwa vile yeye hapa ndio top player. This was a missed opportunity kiukweli.

Kweli mkuu kwasasa hana anachojivunia kwamba kasaidia kitu fulani kwa taifa, Ronaldo anajulikana ni one man show awe madrid au awe timu yake ya taifa lazima tu atafunga magoli muhimu ya kuibeba timu yake...

Samatta bado sana hujafikia level ya sisi kukupa barabara au mtaa maana you have nothing to show tukikuringanisha na hata Rayvanny maana kwa Diamond humgusi kabisa katika suala la kuitangaza nchi kimataifa
 
Mkuu ulichoandika kina ukweli sana....kuna mdau nilikuwa naongea naye nilimwambia kama Mimi ningekuwa samatta ningeitumia nafasi ya Wanyama kuwa bongo kujenga urafiki hata wa kujipendekeza ila wenye manufaa zaidi....Ila Samatta haonekani ndondo,haonekani kitaa nasikia anajifungia ndani anacheza Play station!
 
Back
Top Bottom