Ya Nishati Na Madini Ni Kioja Kingine! ( Makala, Raia Mwema) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Nishati Na Madini Ni Kioja Kingine! ( Makala, Raia Mwema)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 30, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,
  PTOLEMY, mwanafalsafa wa Kiyunani alipata kuandika: ”Ex Africa simper aliquid novi". Maana yake: "Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika."

  Naandika makala haya nikiwa nchini Sweden. Katika kufuatilia yanayoandikwa na kusemwa na wanahabari wa Sweden kutuhusu sisi, basi, nimekutana na kashfa ambayo kimsingi ni kioja chenye kutuhusu.
  Hapa Sweden kuna Shirika la Misaada limeishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.
  Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey, inavuna gesi ya Songosongo nchini Tanzania; huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli , TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.
  Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid, iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.
  Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 10. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabini na tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.
  Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi uliotamalaki unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Unatuacha tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.
  Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na mkataba wa kifisadi usiotanguliza maslahi ya Taifa. Taarifa hii niliweka mtandaoni majuma mawili yaliyopita na hakika wengi wameshiriki kuitolea maoni yao.
  Ni jambo la faraja na kutia moyo kuwa hata waheshimiwa wabunge, bila kujali itikadi zao za vyama, wameanza kuamka na kuwa wakali kutetea rasilimali zetu. Na hakika, huu ni wakati wa waheshimimiwa wabunge wetu kumweka kikaangoni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na Waziri Ngeleja atwambie ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii, na hivyo basi kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.
  Naamini kuwa nchi yetu ni nchi tajiri sana, lakini wananchi wake wengi wamo katika lindi la umasikini unaotokana na ufisadi wa wachache tuliowapa dhamana za uongozi.
  Haiyumkini mtu mwenye akili zake na anayeipenda nchi yake akakubali kuingia mkataba wa miaka 25, kwa maana ya robo karne, na kampuni ya kigeni kuruhusu wageni hao wavune gesi yetu asilia iliyo kwenye visima vyetu kule Songo Songo.
  Na kioja katika mkataba huo ni mgeni mwekezaji anayevuna gesi yetu tunakubali asitozwe kodi kwa faida anayopata kwa kutuuzia umeme unaotokana na gesi ya kwetu wenyewe! Kwa mwanadamu, ni heri uwe mwendawazimu kuliko kuwa limbukeni. Watanzania tumefanywa kuwa malimbukeni.
  Na majuzi hapa tumemsikia Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo, akimtuhumu Bungeni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia Shiolingi bilioni moja kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge. Nacho ni kioja kingine kwa wizara ya serikali kutumia fedha kuwahonga wawakilishi wa wananchi ili bajeti ipite, na wawakilishi hao wakapokea hongo hiyo.
  Ni jambo jema kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufikia busara ya kuondoa bungeni hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini. Na itakaporudi tena bungeni, ni wakati wa wabunge wetu kusimammia maslahi ya umma na kuibana Wizara kufafanua baadhi ya mikataba yenye kashfa kama huu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli, TANESCO na kampuni ya Pan African Energy.
  Na kauli ifuatayo ya Mbunge wa Nzega, Mheshimiwa Hamisi Kingwangwalah inatia matumaini kuwa bado tuna wabunge walio tayari kupambana kutetea maslahi ya umma.
  Mbunge Kingwangwalah aliyasema haya bungeni:
  "Nataka nianze kwa kusema siungi mkono hoja ya kupitishwa kwa bajeti hii na nawaomba wabunge wenzangu msipitishe bajeti hii kwa sababu tupo gizani". Mbali na tatizo la umeme, alitaja sababu nyingine za kutaka bajeti hiyo isipitishwe kuwa ni mikataba mibovu ya sekta ya madini na nishati ambayo imesababisha rasilimali za nchi kuibwa na wageni huku Watanzania walio wengi wakiendelea kuogelea kwenye umasikini.
  Mbunge Kingwangwala anasema: "Waliosababisha hayo wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua. Wengine wapo hapa bungeni na wengine wako serikalini. Hii ni mikataba kandamizi. Watu hao wapo kwenye 'system' (mfumo wa Serikali). Nchi inauzwa, wachache wanashibisha matumbo yao. Watu hawa wamelifikisha taifa kwenye mazingira haya ya kifisadi kwa sababu ya kutumia nafasi zao kujinufaisha na kuweka kando maslahi ya umma wa Watanzania...Hawa watu kama hawafikirii kwa matumbo wanafikiria kwa kutumia 'spinal cord' (uti wa mgongo) badala ya ubongo."

  Mbunge huyo akaongeza kusema; “ Watendaji walioliingiza taifa kwenye mikataba hiyo mibovu wanapokwenda kuisaini wanajali kile watakachopata ili kufanikisha malengo yao binafsi kama vile kujenga majumba ya kifahari. Wanaruhusu ardhi ya Watanzania kuuzwa nao wanafaidi kwa kwenda kujenga Mbezi Beach (Dar es Salaam),"

  Akaongeza kusema: “Miongoni mwa mikataba ya kifisadi ni kati ya Pan African na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusiana na uzalishaji na usafirishaji wa gesi asilia.” Mwisho wa kumnukuu.
  Ndio, kuna baadhi ya viongozi wetu wameigeuza nchi yetu kuwa Banana Republic. Katika Banana Republic, wanasiasa wachache hutumia siasa kufanya biashara na uchumi wa nchi. Wako tayari kuuza rasilimali za nchi kwa faida yao.
  Watanzania tuna lazima ya kukataa kugeuzwa malimbukeni na kuruhusu nchi yetu kuwa Banana Republic’- Jamhuri ya Migomba. Nahitimisha.
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kuna tofauti gani kati ya mikataba aliyoingia chifu mangungo wa msovero na hii ya serikali yetu? ukicheki vizuri utaona hamna kabisa hivyo naconclude kuwa hawa wasomi wetu wa havard ni mbumbumbu kama mangungo
   
 3. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mikataba mingine ya kifisadi katika sekta ya nishati ni: TANESCO na Songas, TANESCO na IPTL, TANESCO na Richmond, TANESCO na Dowans, TANESCO na Agreko jumla yake ni nchi iko gizani bila umeme kwa ubiinafsi wa viongozi wetu hawa.
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mjengwa kwa kweli kuna ugumu sana kukuelewa wewe ndugu yangu kwa maana juzi tu umemuita JK kuwa ni mwanasiasa mahiri, mwanasiasa mahiri na haya yote yanaendelea chini yake bila yeye kuchukua hatua . kuhusu Tanzania kugeuka Banana republic, inabidi nikushangae wewe kuwa ndio umejua leo kuwa Tanzania inataka kugeuzwa kuwa banana republic wakati Tanzania is and has been a Banana republic for a while. viongozi wamekuwa wakiiba mabilioni kila kukicha huku wakitukana hadharani kwa kudai kuwa hivyo ni vijisenti tu na rais anasikia na hafanyi lolote. sasa hivi ufisadi ndani ya TZ umeshakuwa institutionalized kwa maana mtu anaiba haulizwi tena kama kaiba isipokuwa anaulizwa kiasi gani kaiba??
   
 5. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Post yako ya mfalme IHSAN na hii hapa yaani zinapingana, sasa sijui wewe unatetea nini hasa; kotekote unataka, yaani kutetea maslahi ya nchi na kutetea chama tawala. Chagua kimoja basi tukuelewe. Katika posti ya IHASN umetoa lawama za kuyumba nchi kwa watu wasio na shukrani kwa maendeleo makubwa yaliyoletwa na serikali ikiongozwa na mfalme/rais hodari. Pots hii unaonesha utawala legelege unavyoruhusu maliasili ya nchi kuvunwa bure na kupelekea wananchi kukosa hata huduma muhimu kama elimu. Jaribu kukumbuka uliyoandika jana kabla ya kuandika tena siku inayofuata make wasomaji tunakumbuka hata kama wewe unasahau. Au una sera ya kuuma na kupuliza kama panya?
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa haeleweki anataka nini. Ni kibaraka mkubwa na mlamba vidonda wa mafisadi halafu anajifanya kujigeuza ati ni mzalendo. Watu wa dizaini hii Marehemu Samora alikuwa anawaita ofisini na kuwatwanga shaba ya kichwa kwa mkono wake.
   
 7. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,262
  Likes Received: 3,095
  Trophy Points: 280
  '' JK ni raisi dhaifu" - Prof I Lipumba
  '' Serikali ni dhaifu" - E Lowassa
  " Bunge limekosa nidhamu" - J Warioba
   
 8. m

  maggid Verified User

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Silent,
  Ahsante sana. Hiyo simulizi ya Mfamle Ihsan kwenye nchi yenye giza unapaswa uisome kwa makini kabla ya kuharakisha kutoa hukumu.
  Maggid
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  maggid mjengwa ni ndumila kuwili? Nadhani muadhirika wa ufisadi ambaye dhamira yake inamsuta.
   
 10. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Politiki,
  Nakubaliana na wewe, lakini huyu jamaa (Mjengwa) haiyumukini kabaini kuwa alichosema jana hakikuwa sahihi ndiyo maana kaja na hoja hii, ambayo kimsingi inasikitisha na inaumiza sana. Nakumbuka Tido Muhando (wakati huo alikuwa BBC) alimuhoji Prof I. Lipumba mara-tu JK alipounda baraza lake la mawaziri la kwanza kuona mstakabali wa TZ. Prof. Lipumba alisema JK kaweka baraza la kishikaji ili kufyonza maliza za Taifa na kufisilisi hazina iliyo jaa fedha zilizokusanywa na mtangulizi wake mzee Mkapa. Kwamba, Lipumba (Prof) aliyaona haya ya Tanzania kugeuzwa kuwa banana republic zamanii sana. Zaidi ya yote Prof. Lipumba alisema "TUNAMATATZO MAKUBWA". Kwahiyo Mjengwa ndugu yangu na wana jf wote mkae mkijuwa kuwa: Ni nguvu ya umma tu ndiyo itamaliza yote haya.
   
 11. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,807
  Likes Received: 2,581
  Trophy Points: 280
  Mikataba mibovu ya aina hii imechangia pakubwa Zanzibar kutoa petroli na gesi kutoka mambo ya muungano.
   
 12. wende

  wende JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 715
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nawasifu sana wazanzibari kwa kuliona hilo mapema! Big up TZ zanzibar.
   
Loading...