Ya Mwisho Wa Wiki:Mgombea ubunge Chadema ahamia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Mwisho Wa Wiki:Mgombea ubunge Chadema ahamia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TandaleOne, Sep 6, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Mgombea ubunge Chadema ahamia CCM
  Saturday, 04 September 2010


  Julieth Ngarabali, Kibaha


  MGOMBEA wa Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, kwa tiketi ya Chadema, Nkhambaku Elisha amesitisha kugombea nafasi hiyo na kurudi CCM.

  Elisha alihamia Chadema kwa hasira akitokea CCM baada ya kuenguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) licha ya kuongoza katika kura za maoni.


  Tukio hilo la mgombea ubunge kusitisha kampeni zake na kuhamia chama kingine ni la kwanza kutokea mwaka huu.


  Uamuzi huo wa Elisha unampa mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Mohamed Misanga kushinda uchaguzi huo bila kutumia nguvu nyingi.


  Elisha aliongoza kwenye kura za maoni kwa tiketi ya CCM, lakini jina lake lilitupwa na Nec kupewa aliyeshika nafasi ya pili.


  Mgombea huyo alifikia hatua hiyo jana, wilayani Kibaha, ilikofanyika mikutano miwili ya kampeni ya CCM katika Wilaya za Kibaha na Bagamoyo.


  Katika kura za hizo za maoni, Elisha aliongoza kwa kura 3,499 akifuatiwa na Mohamed Misanga kwa kura 3,433, lakini Nec ilimwengua.


  Hatua hiyo inadaiwa kuwa ndiyo iliyomfanya mgombea huyo apate jazba na kuamua kujiunga na Chadema ambao nao walimpitisha kugombea jimbo.


  Akizungumza katika mkutano huo wa CCM mkoani Pwani, alisema alichanganyikiwa jina lake lilipoenguliwa na Nec wakati alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni.


  Alisema hasira ndizo zilizomfanya ahamie Chadema kwa kuwa alitamani kuwaongoza wananchi kupitia ubunge, lakini aligundua kuwa nafasi yake ya baadaye kisiasa itakuwa ndani ya CCM na si chama kingine.


  Alisema alianza kupeperusha bendera ya Chadema kwa kishindo lakini hasira zilipoisha

  akagundua kuwa alikosea na aliposhauriana na ndugu na marafiki aliamua kurudi CCM.

  Kuhusu usaliti, Elisha alisema kuwa yeye si msaliti lakini hawezi kuzuia watu wengine kumwona kuwa ni msaliti kwa kuwa suala hilo lipo katika vyama vyote, bali jambo la msingi kwake ni kuwa ndani ya CCM.


  Mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alisema chama kinatambua umuhimu wa Elisha na ndiyo maana waliamua kumshauri na akakubali kurudi CCM.


  Naye Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba aliwataka wanachama wenzake waliokimbilia upinzani kwa hasira warudi nyumbani ili wajiandae na chaguzi zijazo.


  Kampeni za Dk Slaa

  Mwandishi wetu, Salim Said anaripoti kuwa siku sita za mwanzo za msafara wa kampeni za mgombea urais Chadema, Dk Wilibrod Slaa ziliambatana na matukio kadhaa, huku ummati mkubwa watu ukijitokeza katika mikutano aliyofanya katika mikoa ya Manyara na baadhi ya majimbo ya Dodoma na Morogoro.

  Katika siku hizo sita, Dk Slaa akiwa ameongozana na mchumba wake Josephine, alionyesha kukubalika kwake katika wilaya za Kiteto, Babati, Hanang, Mbulu zote za mkoani Manyara na Mikumi mkoani Morogoro pamoja na Singida Vijijini.


  Mwanzo wa msafara


  Baada ya ufunguzi wa Agosti 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alianza msafara wa kampeni Agosti 30 mwaka huu katika majimbo mbalimbali ya Morogoro pamoja na Mikumi.


  Wakati Dk Slaa akiwa jukwaani anahutubia katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro alasiri, alipita mwendesha baiskeli ya matairi matatu (Guta), na kumwambia, "Freeman Mbowe usiwadanganye wananchi…Freeman Mbowe usiwadanganye wananchi."


  Lakini Dk Slaa alimjibu, "Msikilizeni huyo hajui hata anayoyasema kwa sababu kutokana na hali yake hapaswi kusema maneno haya, kwani hafanani hata na sisi, lakini mwacheni msimfanye chochote."


  Kulia jukwaani

  Baada ya hapo, Agosti 31, Dk Slaa alihamishia msafara wake mkoa Dodoma ambapo alianzia mikutano yake katika Jimbo la Mtera, ambalo lilikuwa linaongozwa na John Malecela kwa miaka zaidi ya 30 sasa.

  Akiwa hapo Dk Slaa alimwaga mchozi jukwaani baada ya kuelezwa hali ngumu ya maisha inayowakumba asilimia kubwa ya wananchi wa Mtera.


  "Nimelia kwa sababu ya hali ngumu ya maisha yenu ambayo mmenieleza, lakini pia nimekumbuka wenzenu 50, waliofukiwa wakiwa hai katika machombo ya madini ya Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambayo mkataba wake ulisainiwa na na Jakaya Kikwete," alisema Dk Slaa.


  Ufafanuzi wa ndoa yake


  Baada ya makombora mengi kutupwa katika baadhi ya magazeti kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM kuhusu ndoa mpya ya Dk Slaa, ikidaiwa kuwa ina utata, inamtesa na kwamba amepora mke wa mtu, aliamua kuvunja ukimya.


  Septemba 2, mwaka huu, akiwa katika mkutano wa hadhara, Babati Mjini Dk Slaa kwa mara ya kwanza aliamua kutoa ufafanuzi juu ya ndoa yake hiyo, na kumtambulisha kwa mara ya pili mchumba wake mbele ya umati wa watu.


  Utambulisho wa kwanza wa Josephine Mushumbusi ulifanyika siku ya uzinduzi wa kampeni za Chadema katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Slaam Agosti 28 mwaka huu.


  "Ni kweli niliishi na mwanamke nje ya ndoa na kuzaa naye watoto wawili, lakini nilipotaka kufunga ndoa sikutaka kufunga naye niliamua kufunga na huyu. Hebu mama Slaa nyanyuka wakuone," alisema Dk Slaa katika uwanja wa Kibaya Babati Mjini.


  Kumnadi Rose Kamili


  Katika mkutano wa kwanza wa Septemba 3, uliofanyika katika uwanja wa Endasaki, Dk Slaa alisimama jukwaani na Kamili ambaye aliishi naye na kuzaa naye kabla hawajatengana na kumnadi kwa wananchi huku akitaka wamchague kwa kura nyingi.


  Wakati hayo yakiendelea jukwaani, Josephine alikuwa amekaa katika meza kuu iliyokuwa katika hema lililojengwa kwa ajili ya wageni hao.


  Dk Slaa alimsifia Kamili ambaye alikuwa diwani wa CCM kwamba ni kiongozi makini na anaweza kumaliza ufisadi ndani ya halmashauri ikiwa atafanikiwa kupata ubunge wa jimbo hilo, ambalo sasa linaloongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Mary Nagu.


  Akiwa katika kijiji cha Rose Kamili cha Basutu, Dk Slaa aliahidiwa kura zote za wananchi wa hapo kwa kuwa ni kwake, kwa watoto, shemeji na wake zake.


  "Dk Slaa usiwe na wasiwasi, hapa ni kwako, kwa watoto wako, shemeji na wake zako, hivyo nakuahidi kuwa utapata kura zote za watoto, wakwe na shemeji zako," aliahidi Rose Kamili.


  Basuto wanajua bado Dk Slaa na Kamili ni mke na mume


  ya waliohudhuria ambao ni wa asili ya kimasai wakirukaruka na mishale kana kwamba wamepandisha mori, katika kushangilia.


  Katika hali ya isiyo ya kawaida baadhi ya wagombea hao akiwamo Dk Slaa walilazimika kujinadi kwa kutumia lugha za makabila, baada ya kudaiwa kuwa wananchi wengi wa Babati, Hanang na Mbulu ambao ni Wairaq, Wamasai, Wambulu na Wabarbei hawaelewi Kiswahili vizuri.


  Dk Slaa alisema lengo lake la kutaka kuingia Ikulu ni kuwakomboa Watanzania na sio kwenda kula mayai na kujilimbikizia mali


  Source: Mwananchi Jumamosi
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kumbe wewe al shabab
   
 3. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  No,The Mosad
   
 4. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Au Scotland Yard kabisa.That sounds better.Ila tujivunie vya hapa kwetu Tanzania.No special name but they work.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kumbe Slaa ni mtu wa maskandali kibau ,afu mnampigia debe hapa ,jamani tunahitaji raisi msafi kabisa ,huyu Slaa hadi hapa ambapo hatujafika hata robo ya kampeni tayari anakandamizwa kwa mabalaa ya ndoa ,sijui watoto ,kuzaa nje ya ndoa, yaani amemdhalilisha huyo mwanamama kwa kumuweka au kukaa nae na kumzalisha bila ya kupita uhalali wa kufanya hayo ,sijui ni dini gani au kabila gani linaruhusu tabia hiyo

  Halafu mnafumbia macho kana kwamba ni halali kwake kuyafanya hayo, wandugu kusema ukweli Slaa hafai kabisa ,tena muwe na tahadhari sana maana inaonyesha wazi huko atokako anahistoria mbaya isiyolingana na cheo anachogombea ,je akiukwaa Uraisi itakuwaje na mtamlaumu nani ? He must be ruled out ndani ya Chadema ,ni bora mungeliweka ,wengine yeyote yule ,kuliko huyu ambae inaonekana wazi ana problem.
  Tutasikia na kuona mengi ni bora akajitoa kabla mambu hayajamuendea vibaya.
   
 6. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Sipati picha wakigundua one day kwamba Slaa ni CCM au bado padri!!Unajua tatizo la ushabiki wa ghafla ni kuwa huwa unashindwa kufikiri vizuri.Ila ukiamka unaweza mtia mtu makofi.
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Mwamadi alikuwa anapora vitani na anafundisha watu namna ya kujilipua ... mbona usianze kuhimiza watu wamkatae kwanza???
   
 8. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Kazi unayo kaka.
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Angalieni upupu huu wakuu - yaani inakera hata kusoma, njaa bado ni adui mkubwa wa demokrasia kwa nchi maskini kama Tanzania.
   
 10. m

  mtiwadawa Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alisema hasira ndizo zilizomfanya ahamie Chadema kwa kuwa alitamani kuwaongoza wananchi kupitia ubunge, lakini aligundua kuwa nafasi yake ya baadaye kisiasa itakuwa ndani ya CCM na si chama kingine.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Halafu watu kama Mwiba na msula gani sijui wanaona jamaa amefanya jambo la maana.

  Ngoja Slaa ashinde na kama alifikiri atapata Ukuu wa Wilaya, basi ameula wa Chuya.

  Jamaa atajuta kuzaliwa maana CCM watamuacha kwa kujua kuwa siku nyingine akichukia ........

  Chadema ndiyo kabisa maana ni MSALITI. Kusema kweli hata CCM wameshajua kuwa ni MSALITI.

  Kashajikaanga mwenyewe Msingida huyu jirani yangu.
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Signature yako ina upupu ulioexpire kaka.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Na kweli imeshiwa, Aiseeee..............


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. asam.thegunner

  asam.thegunner Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman maon yanayotolewa humu mengi yanaonyesha dhahiri dalili za chuki . Imefikia hadi watu wanakashifu dini za wengine. Nilidhani tuko pamoja katika kupambana kumbe inawezekana kabisa kuna kusudio maalum. Kwa mwendo hamtafika popote na mtaishia kuwa losers daima.  Mpenda siasa asiye na chama
   
 16. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135


  naam hivi kumbe alikuwa akivunja amri ya sita ya dini aliokuwa akiitumikia, na bado anafaaa kuwa mfano wetu mwema kuwa rais ?

  tena bila aibu anasema jukwaani kuwa yeye ni mzinifu, na sasa ananendeleza uzinifu kwa mke wa mwengine ati atamuoa.

  na nyinyi mnaona anakufaeni awe rais.

  huyu hafai hata kuwa mwanachama wa chama chenye kujiamini na kufata maadili
   
 17. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
Loading...