Uchaguzi 2020 Ya Mwenyekiti wa CCM Tarime kumuita mgombea mwanamke ni malaya, na ukimya wa Chama changu

Mikono yenye Sugu

Senior Member
Jul 1, 2020
133
215
Kitendo cha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime kutumia lugha isiyo ya staha jukwaani kwa kumuita mgombea wa CHADEMA "mwanamke malaya" ni cha kidhalilishaji na hakipaswi kunyamaziwa pasipo kukemea.

Tupo katika mchakato wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu na Tume imekuwa ikisisitiza kila mara wagombea wa vyama vyote kufanya kampeni za kistaarabu pasipo kutumia maneno ya uchochezi na uvunjifu wa amani. Alichokifanya Mwenyekiti huyo ni udhalilishaji dhidi ya mama zetu akiwemo mama yake, dada zake na shangazi zake.

Ni matumaini yangu kuwa CCM, hususan watendaji waandamizi wakiongozwa na Katibu Mkuu Mwl Bashiru, watajitokeza hadharani kukemea kauli hiyo sambamba na kuomba radhi umma wa wanawake wa taifa hili na wapenda amani wote kwa kitendo kilichofanywa na mwenyekiti huyo mwenye nakisi ya maadili.

Nakipenda chama changu, lakini kamwe sitakuwa tayari mapenzi hayo kunifanya nisione yasiyofaa na kuyakemea.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mwanaume anayemuita Mwanamke Malaya tena hadharani ana tatizo la akili
 
Mwanaume anayemuita Mwanamke Malaya tena hadharani ana tatizo la akili

Kwa kweli inabidi tuungane mkono kuandamana humu kwenye mitandao mpaka ajue tumechukia. Tena ingekuwa vema kama Mwenyekiti wa chama kitaifa angeungana nasi kukemea na kulaani kitendo hiki. HAKIKUBALIKI. Hii ni nchi ya kistaarabu na kamwe sio karakana ya matusi.
 
Upo sahihi.hiki kitendo kikemewe
 
Kwasababu ni mwenyekiti wa CCM hakuna shida. Sheria zimewekwa kudhibiti wapinzani tu ndoaana mpaka kamera zimesajiliwa kwa dola. Hata kama akimchoma mtu kisu hadharani na akafa hatachukuliwa hatua maana ni CCM.
 
CCM wapo juu ya sheria
 
Mkuki kwa ngurue apo hiyo kauli ingekuwa imetolewa na wa chama pinzani ungeskia police ishahusika
 
Hapo TUME ya UCHAGUZI toeni ufafanuzi, Mgombea Ubunge wajimbo la Tarime mjini kuitwa MALAYA na Mwenyekiti wa chama tawala , je, KAMPENI ZA KISTAARABU?

Msipochukua HATUA, upande wa pili nao ukajibu kwa maneno ya KASHFA mtasema kosa la mwingine halikuhalalishii kujibu kwa kosa?
 
Back
Top Bottom