Ya Mtikila: Rostam aburutwa kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Mtikila: Rostam aburutwa kortini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Oct 27, 2008.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  * Atakiwa kulipa mamilioni
  * Chanzo ni kanisa, ufisadi
  * Ahusishwa pia na utumwa

  Na Mwandishi Wetu - Majira

  MWANASIASA mashuhuri nchini ambaye pia ni Mbunge wa Igunga (CCM), Bw. Rostam Aziz ameburutwa kortini akitakiwa kulipa mamilioni ya fedha na pia kuomba radhi kwa kile kilichoelezwa kuwa wazazi wake kujihusisha na biashara ya utumwa, limebaini gazeti hili.

  Rostam ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa za CCM, kwa hatua hizo sasa atalazimika kufika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Jaji Kalegeya Novemba 11 mwaka huu kujitetea kutokana na mashitaka hayo.

  Katika kesi ya madai namba 131 ya mwaka huu iliyofuinguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila na Majira kupata nakala yake, Rostam pamoja aliyeunganishwa na magazeti kadhaa nchini yaliyiripoti haba ri hiyo, anadaiwa kumkashifu kiongozi huyo na kutakiwa kulipa sh. bilioni 3.

  Kwa mujibu wa hati ya mashitaka yenye kurasa 10, vipengele 37 na vielelezo lukuki, Mtikila anadai kuwa Bw. Rostam alimchafulia jina na hadhi yake mbele ya jamii kwa maneno aliyoyasema kwenye mkutano wake na waandishi wa habari wa Julai 13 mwaka huu, ambao pia uliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo tovuti na kuibua mijadala kwenye intaneti.

  "Julai 13 mwaka huu mdaiwa wa kwanza (Rostam) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski alitoa kauli iliyonidhalilisha," inaeleza sehemu ya hati hiyo.

  Maneno ambayo Mtikila anadai kuwa yalimkashifu, yameanza kubainishwa katika katika kipengele cha 12 cha hati hiyo ya mashitaka ikimkariri Bw. Rostam akisema:

  "Matamshi yaliyotolewa wiki hii na Mtikila ni kinyaa, yananuka harufu ya chuki, wivu,ubaguzi,unafiki na ufisadi."

  Chanzo cha sakata hili hadi kutua mahakamani ni tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazomkabili Bw. Rostam ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu nchini ambazo baada ya kimya kirefu, alizizungumzia kwa kwa mara ya kwanza alipoalikwa kwenye uzinduzi wa kwaya ya Kanisa la KKT Kinondoni, ambapo mbali na kutoa msaada wa sh. milioni saba, pia alikanusha kuhusika na tuhuma zote hizo na kusisitiza kuwa yeye ni mtu safi mbele ya jamii.

  Siku kadhaa baada ya Rostam kutoa kauli hiyo,Mtikila aliibuka na kulaani kitendo cha Rostam kutoa mchango kanisani na 'kujisafisha' akisema Kanisa halikustahili kupokea fedha za Mbunge huyo.

  Akionekana kukerwa na kitendo hicho, Rostam ndipo alipoitisha mkutano wa Julai 13 ambapo pamoja na kauli iliyoonekana kumuudhi Mtikila alitoa siri kuwa Mchungaji huyo naye aliwahi kumwomba mchango kwa ajili ya kanisa lake na akampa sh. milioni 3. Mtikila hakukana dai ila alihoji uhalali wa risiti ya mchango huo ambayo Rostam aliitoa kwa wanahabari akisema ilighushiwa.

  Katika kesi hiyo, pamoja na kutaka alipwe mamilioni hayo ya fedha Mtikila amembana zaidi Rostam kwa kuiomba Mahakama imwamuru awaombe radhi Watanzania kwa kile Mchungaji huyo alichokisema kuwa ni wazee wa mbunge huyo kujihusisha na biashara ya utumwa.

  Mtikila ameomba katika hati hiyo: "Zaidi (Mahakama) imuamuru mdaiwa wa kwanza (Rostam) aombe radhi kwa maandishi kwa watanzania kwa niaba ya familia yake au mababu zake, kwa kuwafanyia biashara ya utumwa wazee wetu kwa kuwafanyisha kazi za kubeba dhahabu na pembe za ndovu."

  Uchunguzi wa Majira umebaini kuwa dai hilo la Mtikila limetokana na Bw. Rostam kukiri alipozungumza Julai 13 na waandishi wa habari kuwa biashara zake amerithi kwa wazee wake waliokuwa wakifanyabiashara tangu mwaka 1852 ingawa hakutaja aina ya biashara hizo.

  Rostam alisema:"Fedha zangu ni pato halali linalotokana na jasho langu kupitia biashara ambayo imekuwa ikiendeshwa na familia yangu tokea mwaka 1852."

  Kwa mujibu wa Sheria ya Mwqenendo wa Madai na Kanuni za Mahakama Kuu, Rostam halazimiki kufika mwenyewe mahakamani hapo kujitete, iwapo ataamua kuweka wakili au mtu wa kumwakilisha lakini anaweza kulazimika kufika kortini iwapo kuna ushahidi utakaokuwa muhimu yeye mwenyewe kuutoa.


  Imekaa kinamna
   
 2. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  ......Kuchamba kwingi mwisho utoka na mavi......
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuendelea kusisitiza Mchungaji Mtikila sio timamu ila pia nakiri kuwa sio kichaa. Ni political fanatic mwenye hobby kubwa ya kuendesha kesi.

  Kuna baadhi ya kesi zake zinasaidia jamii kama ile ya mgombea binafsi.

  Hii ya Rostam haina merit in the face of it. Kwa vile anadai alikopa ile M.3 kwa Rostam, kumfungulia kesi ya madai mdeni wako ni moja ya njia za kukwepa kulipa deni.
  Dai la biashara ya utumwa ni ngumu kulithibitisha before the court of law japo sio siri waarabu walifika Tabora wakati wa biashara ya watumwa,
  Natamani kumfahamu wakili wa Mtikila I doubt kama analipwa!.
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Ukisikia kufilisika kisiasa ndiko huko? Hivi huyu mtikila wananasheria wake wanafurahia kulipwa fees tu au ni kitu gani? Mbona hawamshauri katika baadhi ya kesi zake? Au pengine anatumia msaada wa kisheria katika hivyo vituo husika Tz? Vinginevyo sielewi kama kesi za Tanzania ni deal kwa wadai ukizingati gharama kubwa za uawakili au tu kuandikwa legal document. Pole Mtikila mpenda kesi. Tutakuita mzee wa Vyesi!!!!
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kuna watu wanampandisha munkari Mtikira ili ampigishe kwata Rostam na kumpotezea apetite ya siasa si unajua wenyewe wanasema siasa ni mchezo wa kuchafuana...
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,687
  Likes Received: 21,953
  Trophy Points: 280
  Vipi yule aliyempiga jiwe kule tarime hajamtambua ili naye amfungulie kesi? Au anasubiri mbunge aapishwe kesho amdai fidia bil.5 kwa vile wapigakura wake walimuumiza? kwi kwi kwi1!
   
 7. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  the sooner MTIKILA leaves tanzanian politics behind,the better.he has become a laughing stock,and sorry to say this,but he has now assumed the title of a pain in the a----.he is at most a brake in the fight for proper democracy in tanzania.At every opportunity he just deviates our attention towards silly nothings.
   
 8. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mbona baadhi ya 'wakuu' hapa JF walisema kuwa wanauthibitisho kuwa Mtikila alitumwa na CCM (Makamba na Rostam) kule Tarime kwenda kuichafua CHADEMA?

  Macho na masikio yetu !!!
   
 9. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Believe me my dear huyu is a real fanatic but you can never know the contribution he has made on the Tanzanian Legal System unless you are a lawyer with his everyday's cases!
  Mtikila has to know one thing that Tanzanians are fed up with him and they actually want him to retire politics unless he is being paid handomely for what he is doing!
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ningependa kujua kama suala la Uraia wa Rostam limo kwenye hii kesi au la. Nadhani Mtikila aliahidi kwamba na hili litakuwa addressed mahakamani maana ana vithibiti vya U-irani wa Rostam.

  Kama halimo basi hizo issue za utumwa ni smokecreen za Mtikila tu. By the way, kutoomba msamaha kwa utumwa ni uvunjaji wa sheria gani ? I wish we had competent court reporters. Or, we had just the press period.
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  .....tangu agundue namna ya kufungua kesi basi game yake ni kuburuza yeyote on his way na sijui huko kanisani kwake kuko vipi? mwenye hint atupe!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Koba,
  Hivi unaamini Mtikila ana kanisa kweli? Huo uchungaji alijipachika mwenyewe. Hajausomea au kuwekewa mikono kama ilivyo kwenye madhehebu mengi ya Kikristo.
   
 13. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Niliambiwa kuwa, kuna siku moja aliulizwa na mwandishi fulani wa habari ataje chuo alichosomea Uchungaji, akajibu alisomea chuo cha Uchungaji alichosomea Yesu Kristo na wale mitume wake 12.
   
 14. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,230
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Wengi mnaweza mkadhani akili za mtikila hazina akili, lakini the Guy si very smart. na ninakuelezeni hiyo kesi itazua mengi na nyote hapa mtageuza semi zenu na kumuunga mkono. mwenye kumbukumbu za kesi za mtikila atushushie hapa tuone ameshindwa ngapi na ameshinda ngapi.

  Ila nijuavyo mie keshi ni gharama na kama atashindwa basi inakula kwake. kwa uzoefu wake huko mahakamani kila kukicha lazima atakuwa anajua anachokifanya. Kimsingi yeye anatumika tu kama mshitaki lakini nyuma yake lazima kuna wanasheria anaodili nao ambao ni ma opportunists ambao wanajua kesi ikishinda bilioni 3 si ndogo.

  Serikali ishamlipa huyo mara nyingi tu kila anapoishinda huko mahakamani, Kwa mtikila kesi ni project kama project zingine za kawaida ambazo wewe na mimi tunafanya kupata mkate wa kila siku. Ndo maana kila anapoona opportunity ya kuweza kuburuza mtu mahakamani anaitumia effectively.

  Sasa wewe ukimuona mtu kachizika wakati ndo kwanza yuko kwenye miradi yake utajiju.
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Endeleaaa,

  Mtikila huwa yuko Mahakamani kwa kesi za Kikatiba au kujitetea kwa "mihadhara ya kichochezi." Sidhani kama utatengeneza hela ukishinda kesi ya ku overturn constitutional provision.

  Na angekuwa anapata hayo mabilioni asingekuwa anaenda kumpiga mzinga Rostam Aziz!!!

  Mtikila ana passion na social issues na ana ma lawyer wenye ujuzi na balls za kushitaki Serikali kutangua katiba. Sidhani kama ni mradi unaompatia faida.

  Hata hivyo wengi tutakubali kwamba jamaa ni kinyonga na ni erratic. Kuchukua hela za unaemshutumu ni fisadi sio tabia za mtu responsible na mkweli.

  Lakini ndio huyo huyo ana shinda ma kesi makubwa makubwa ya kikatiba. Kwa hiyo kama jamaa ni kichaa, basi that says a lot more about the rest of us Tanzanians as it does him, kwa sababu ni yeye tu ndio anaona ma pitfalls ya Katiba. Sisi ambao sio vichaa hatushtukii!

  Katika maswala ya Katiba tunahitaji Mtikila wengine kwenye mahakama za Tanzania. Kichaa ama sio kichaa.
   
 16. M

  Masatu JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwanini tusiamini kuwa Rostam kamtuma amfungulie kesi isiyo na nguvu ili itupiliwe mbali na Mahakama na mwisho wa siku kuficha makubwa ya Rostam

  Mbuzi kwenye gunia.......
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pamoja na uzoefu wa Mtikila hii kesi haina cha ziada zaidi ya kutaka kutupotezea muda na akili zetu kufikiria mambo yao badala ya kuendelea kuweka nguvu kwenye ukombozi wa pilia wa taifa letu. Hata kama atashinda au kuzua mengi ila kwa sasa hii siyo agenda muhimu ya Watz. Angepeleka kesi kuishitaki serikali kwa kula na wezi wa EPA au yenyewe kutuibia (in the EPA scam) na kutuzuga ningemwona wa maana. For now we can trash him and continue with our main (sweeet) story/agenda....TANZANIA's RENAISSANCE.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Competant court reporter inabidi awe na angalau ODL ama LL.B besides Journalism qualifications. Thank kuna baadhi ya waandishi wa habari wana LL.B ila ni mabosi. Tena nawapongeza sana kuendelea kufanyakazi newsroom. Hawa ni waandishi wa wito.
  Ili kupata proffessionalism lazima usome ama upate uzoefu wa muda mrefu. Nakiri court reporters wetu wengi ni wa uzoefu tuu.

  Kwa wasiojua Prof. Palamagamba Kabudi, Dr. Harison Mwakyembe na Dr. Sengodo Mvungi hawa wote walikuwa waandishi wa habari wakasomea sheria chuo kikuu. Wakafanya vizuri kwenye sheria, wakaajiriwa kuwa wahadhiri. Nani anaweza kukubali kulia juani baada ya kufika kivulini?.
   
 19. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi wanahulka ya kushabikia wanayoyapenda tu. Mtikila sio kichaa wala hana ugonjwa wa akili. mnanitia kichefuchefu kutaka kumwona huyu mtu ni kichaa. Ameona anahaki ya msingi kufungua kesi, mahakama imeona Rostam anakesi ya kujibu Mtikila ametumia haki yake ya msingi.

  Unafiki wenu ndio unaotupelekea kuibiwa na woga ndio kina Rostam na genge lao wanutumia. Tutoe matongotongo kwenye vichwa na kuacha uvivu wa kufikiri tutee nchi yetu na tuunge mkono wale wote wanaojitahidi kufanya hivyo.

  Mahakamani ni sehemu nzuri sana ya kuibua mambo na sheria kufuata mkondo. Rostam ni mwizi na siwezi kumwonea huruma kuburuzwa mahakamani. Anayemwona Mtikila kichaa lazima awaone na majaji wote walihukumu kesi za mtikila akashinda ni vichaa.
   
 20. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2008
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Masatu, kwa mistari yako miwili uliyoandika, nadhani umesema yote na kweli tupu. mtikila ameamua kucheza mchezo hatari kwa malipo!
   
Loading...