Ya msanii Mabeste na mkewe hutokea pale mwanamke anapomzidi akili mumewe

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,743
4,269
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la kuaibishana au kusemana mtandaoni kwa wanandoa ambao wameshafeli kwenye union zao.

Tulishuhudia Mihayo Wilmore na mkewe wakishambuliana mmoja kwenye podcast ya Men Men Men, mwingine akahojiwa na Clouds pamoja na kuvujisha video.

Kisha msanii Stamina akatoa wimbo pamoja na kufanya interview akieleza wazi wazi kuwa kachapiwa na hataki iwe siri ya ndani na akamtaja alommega mkewe kuwa eti ni mchezaji wa Simba.

Wakati bado anga lina vumbi ikaja issue ya Msanii Venance William 'Mabeste' na Mkewe Lisa Karl Fickenscher kuwasuprise fans kuwa wameshatalikiana huku kila mmoja akivuta kamba upande wake kuwa kaonewa.

Niliangalia interview za hawa watu wawili na ninachoweza kusema ni kuwa Mabeste alioa mke asiye level zake especially kiakili.

Sijui yupi ni mkweli kati yao, ila Lisa hata anavyojieleza tu you can tell alimzidi akili Mabeste. Sijasema ana akili saana ila zikiwekwa zake na mabeste kwenye mzani tofauti ni kubwa sana na hapo ndo tatizo lilipoanzia.

Huyu dada anajua kupangilia maneno, ana the right facial expression, hajajichanganya hata kidogo, hajaonesha chuki wala kupiga ngenga, kwa kifupi kamuaibisha Mabeste with class kwa kupitia kwenye weakness zake na kujifanya kama vile hana shida nazo kumbe ndo anatoboa meli.

Mabeste on the other hand, kakimbilia lile lile ambalo wanaume wote hukimbilia, "ooh kaenda kuwa na rafiki yangu, tulikula Christmas kwao". (Kwanza wanaume mtambue tu, ukimuacha mkeo probability ya yeye kuwa na rafiki yako ni kubwa sana hasa akiwa jembe. Kwa sababu wenzio kwani hawana macho? Unadhani hawakuonei wivu unavyofaidi?)

Kisha Lisa kuhusu hilo suala ameclarify, kuwa huyo rafiki alikuwa rafiki yake yeye kwanza na Mabeste ndo akamjua. So Mabeste amebaki hana claim. Alitumia a very weak point.

Mabeste anasema "sijashirikishwa shule anayoenda kusoma mwanangu naambiwa tu kuwa kaenda shule, sijaambiwa natoaje matunzo". Yani amecheza mule mule kwenye story ya Lisa kuwa Mabeste ni Marioo hawajibiki.

Wanaume, tafuta mwanamke unayemmudu kiakili or else utalialia weeh na kusema wamemchukua sababu ya pesa, wamemchukua sababu ya mali kumbe hukutosha kiakili.

Wasalaam




 
Ukidate au kuoa mwanamke mzuri kaa tayari kwa matokeo yoyote iwe umefulia au bado una pesa zao.

Nikki sijui wa pili sijui mbishi awe makini sana na yule pilipili pia(haka kajamaa kanaweza kujinyonga kabisa,kamezama mzima mzima)
 
Hamna sababu ya msingi hapo. Tatizo ni kuchokana tu na mmoja akishamchoka mwenzie basi atatafuta sababu au kuanza visa.

Mitandao imefanya wanawake na mabinti wawe exposed sana so hata kama mwanamke kaolewa anakua bado anajiachia sana na jamaa wengine wakimuona wataanza kuingilia ndoa ya watu

Wanawake zamani hata kutoka tu kwao ilikua ni mpaka awe na ruhusa ya mzazi au mme wake, hii ilisaidia kufanya asionekane sana kwa wasiohusika nae lkn siku hz kama usipomuona mtaani basi utamuona fb, insta au kwenye videos pendwa
 
Ukidate au kuoa mwanamke mzuri kaa tayari kwa matokeo yoyote iwe umefulia au bado una pesa zao.

Nikki sijui wa pili sijui mbishi awe makini sana na yule pilipili pia(haka kajamaa kanaweza kujinyonga kabisa,kamezama mzima mzima)
Ila kweli, kuna siku dogo fln aliniuliza mbona mabilionea kama kina mark na billie wake zao ni wa kawaida mno. Nadhan kuoa mke mwenye mwonekano wa kawaida inasaidia kutunza ndoa. Sio unakua na mke kila mara CHAPUTA wakimuona wanaenda kufanya yao
 
Zurie,
Hat uongo ukiupangilia huwa ukweli, ni kujua tu baada ya attack una revenge vipi kupitia weak points, kuna watu wana akili sana ila ability to express hawawezi but practically they do send message than words, na kuna ambao ni ABIOLA MANENO, anakaba kwa maneno very smart and sweet but practically he is more than Murmuring, Sitaki kujaji kwa migongano ya watu wawili walio tofautiana chumbani wakati wewe unayasikilizia katika social Media.
 
Muuliza maswali hajaitendea haki hadhira.

Kwanza unamuhoji vipi mtu masaa matatu hakuna maji mezani wala tissue?

Pili, uulizaji maswali wa huyu jamaa umekuwa wa kishamba sana. Yani huyu dada ndo anampelekesha mwenye kipindi.

Kuna maswali huyu dada alitakiwa kuulizwa. Muulizaji ameishia kukimbilia kutafuta viewers.

HAKUJIPANGA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona mwanaume kashindwa kulipa mahari basi jua hamna kitu hapo.

Mabeste alipata bonge la mke, ukweni pia walikuwa waelewa sana, lkn kaichezea bahati kwa utoto wa kipumbavu kabisa.

Na asidhani kama atapata mwanamke mwingine kama Lisa, na asipoangalia ndio safari ya kupotea imeanza, sio kimuziki bali maisha yake ndio yanaenda kufa kabisa.

Unforgetable
 
Ukisikiliza zile clip zao utagundua kabisa Mabeste ni muongo wa kutupwa. Sababu alizozisema za yeye kuachwa na mke wake hazina mashiko kabisa, yani ni sababu za kitoto na inaonekana ni mtu ambaye hakuwa tayari kuingia kwenye majukumu ya ndoa.

Hebu imagine mwanaume analalamika eti mama watoto amewapeleka shule bila ya kuniuliza mimi tuwapeleke shule gani? Hivi kati ya mwanaume na mwanamke ni nani wa kuanzisha hii discussion? Halafu watoto kupelekwa shule ya gharama sio tatizo as long as wamelipiwa, kwa nini kama kweli una nia ya kuwalea wanao usichangie chochote?

Katika kitendo ambacho ni cha fedheha ni kile ambapo mke wake alimkopea mahari kwa rafiki yake kwa kuweka bond gari. Akaenda kulipa then wakairudishiwa ili wakakomboe. Hapa mama mkwe na mwanae walifanya hivi ili kuokoa jahazi maana mchizi alishaishiwa mbinu kabisa. Cha kusikitisha mpaka leo mchizi hajapeleka hiyo mahari na anajitetea kwa mama mkwe eti mwanae alimforce kumuoa yeye hakuwa tayari.

Yani Mabeste inabidi aje na utetezi mwingine, lkn kwa huo uharo alioongea hakuna wa kumuamini.


Unforgetable
 
Back
Top Bottom