Ya moto mkubwa West London, Watanzania tuangalie na tujifunze cha kufanya

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
434
1,000
 • Hili jengo walikuwa wanaishi watu wenye kipato cha kati na chini..
 • Kuna firefighters(wazimamoto) 250 na magari zimamoto 40
 • Wame set up emergency hotline numbers (line ya dharura kwa jamaa na ndugu waliofikiwa majanga)
 • Tahadhari nyingi zatolewa kwa wapita njia na walio karibu
 • Bado kuna watu mle ghorofani
 • Mpaka sasa watu 50 wameumia..
 • Idadi ya watu waliokufa kwa moto haijajulikana mpaka sasa..
 • Ghorofa linawakazi sio chini ya watu 400
 • Hatari inayotegemewa ni ghorofa kudondoka kama Twin towers...Na madhara yake hapo baadaye..
 • Kuna flats zaidi 120...
 • Wakazi jijini London, hasa Chelsea, Kensington, sehemu tajiri kuliko yote jijini London wanashiriki kwa hali na mali kuwasaidia wenzao, kuanzia nguo, chakula, mablanketi, sehemu za kupumzika na kulala, wako bega kwa bega kabisa...hawajali cha dini, rangi wa tamaduni za mtu, wao ni kutoa msaada..
 • Mpaka sasa ni watu 12 wamepoteza maisha
 • Yakadiriwa zaidi ya 100 watakuwa wamepoteza maisha
 • 64 wameumia. 22 mahututi.
 • Bado wakazi wengi wa hapo hatima yao haijulikani
 • Moto ulianza toka saa saba asubuhi ya leo (1am-1:30am) Kama saa tisa au tisa na nusu asubuhi ya leo..
 • Mpaka sasa tukio halijahusishwa na ugaidi
 • Yasemekana, ni fridge iliyolipuka kwenye flat moja moja juu, ukweli utajulikana baadaye baada ya kuzima moto..
 • Jengo lina historia ndefu ya kuonywa kuhusu janga kama hili..ila wadau wakapuuzia kama sisi..
 • Swala la usalama lilikuwa lajulikana na wahusika..
 • Yalikuwa makazi ya kila aina ya watu, hasa wahamiaji..
 • Serikali yaanza kushutumiwa madhara yasingekuwa mabaya kama wasingekata matumizi polisi, zimamoto na manispaa...
 • Yadaiwa usalama na ubora wa wakazi haukuwathaminiwa/hawathaniwi sababu walikuwa watu wa kipato cha chini...
 • Tukio liko twitter na lina trend kwa #GlenfellTower
 • R.I.P. waliopoteza maisha...na pole kwa walioumia...
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,829
2,000
Nimejifunza kuwa ,maghorofa yetu yawe na njia za kuruhusu zimamoto kuzungusha magari pande zote za jengo badala ya vile ilivyo kama pale kariakoo, zile nafasi kati ya jengo na jengo zimebadilishiwa matumizi na kuwa biashara au parking
 

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
434
1,000
Nimejifunza kuwa ,maghorofa yetu yawe na njia za kuruhusu zimamoto kuzungusha magari pande zote za jengo badala ya vile ilivyo kama pale kariakoo, zile nafasi kati ya jengo na jengo zimebadilishiwa matumizi na kuwa biashara au parking
Sawa kabisa. Ila pia fires escapes, extinguishers, sprinklers, mabomba ya fire mtaani (Fire hydrants) za kutosha kabisa...
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,252
2,000
Naona kikosi cha uokoaji wameanza kutafuta kama kuna mabaki yoyote ya miili ya watu ndani ya jengo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom