Ya mjomba mjomba: Adela ni Anne Makinda?

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
wimbo niliousikia hivi karibuni wa msanii huyo uitwao 'adela' unanifanya nifikirie pamoja wa watanzania wengine (pengine!) kwamba ni nani hasa anayetajwa kama adela?

ikumbukwe mpoto ni selebu aliyetokea kupendwa sana kwa mtindo wake wa kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya mafumbo ( kama yesu alivyokuwa akitumia mifano [parrables] ili kufikisha ujumbe bila shaka bila ya kulazimika kumkwaza anayehusika.

katika wimbo wa 'mjomba' watu wakajaribu kubashiri nani hasa huyo mjomba; jk? mkapa? spika sitta? (as he then was), wilbroad slaa? nk ambapo wengi walitabiri huenda huyo anko akawa ni mkulu mkuu wa sasa.
sasa kwa vile kwenye wimbo huu wa 'adela' anayetajwa ni mwanamke (kwa mazingira ya kawaida ya kitanzania ambapo mara nyingi wenye jina hilo ni akina mama, dada, wasichana na vichanga vya kike), swali likaja ni mwanamke gani huyo ambaye ana ukaribu na mjomba?

katika kibwagizo adela anatahadharishwa kwamba lengo la kuombwa anyooshe mkono si kurudishwa darasani bali kuwekana sawa.

kwenye lyrics zake mjomba anaendelea 'kumlaumu' mjomba kwa ukaidi licha ya kutumiwa ujumbe kwa vile huyo mpwa hakuwa na nauli...




my take:

je, huyo adela anaweza akawakilisha viongozi gani wa kike hapa nchini? akina makinda na wenye sifa kama hizo za kushikilia ofisi za juu?
 
atakayefanikiwa kupata lyrics za wimbo huo atupatie.
 
Bahati nzuri tunaye huyu kama msanii halisi wa kitanzania anayejua matatizo ya jamii (nchi) yake, si kama wale wa kwenye kampeni za fiesta, na kila wakiimba lazima mkono mmoja ushike sehemu zao za siri (nyeti),suruali oversized chini ya makalio huku muziki wao ukianikizwa kwa makelele yaitwayo mistari isiyo na vina!
 
Adela ni Anne!!!!! asante sana sana sikua nime-observe hii kitu, nilijiuliza sana huyo adela ni nani kwa kweli sikupata kumjua! thanks
 
duuuuuhhhhh!!!!Mpoto ni kichwa!! anamaktaba kubwa sana ya vitabu!! hutumia mda wake mwingi kusoma!! na kila wimbo wake ukiusikiliza hutamani uishe!! ila kuhusu hilo la Adela duh no comment!!
 
ule wimbo una mashairi mazuri sana ila kuna tatizo moja kwenye chorus ambalo ni " Nyosha kidole Adelaaaaa, sina nia mbaya ya kukurudisha darasani" nianavyo mimi kumrudisha mtu darasani si nia mbaya kwani elimu ni ufunguo wa maisha hivyo kusema sina nia mbaya ya kukurudisha darasani wakati darasani ni sehemu muhimu sana ktk maisha ya binadamu, nadhani hapo ametumia neno ambalo si sahihi ingekuwa sina nia mbaya ya kukurudisha gerezani ingekuwa sawa kwani gereza si sehemu nzuri lakini kuhusu darasani nadhani amekosea au mnaonaje wenzangu?
 
naomba mnisaidie, mashairi ya ASANTENI NA KUJA YANA MAANISHA NINI imenikwaza wakubwa
 
Lazima nikiri kuwa kila ninapousikiliza wimbo wa Adela najikuta napata maana tofauti kila siku, maisha yanamuhitaji kila mtu kujifunza na hakuna anayeweza kukosea muda wote wala kusahau si mwisho wa matatizo. Nafurahi Mpoto anavyokitumia kiswahili katika majukwaa makubwa ya kimataifa
 
ule wimbo una mashairi mazuri sana ila kuna tatizo moja kwenye chorus ambalo ni " Nyosha kidole Adelaaaaa, sina nia mbaya ya kukurudisha darasani" nianavyo mimi kumrudisha mtu darasani si nia mbaya kwani elimu ni ufunguo wa maisha hivyo kusema sina nia mbaya ya kukurudisha darasani wakati darasani ni sehemu muhimu sana ktk maisha ya binadamu, nadhani hapo ametumia neno ambalo si sahihi ingekuwa sina nia mbaya ya kukurudisha gerezani ingekuwa sawa kwani gereza si sehemu nzuri lakini kuhusu darasani nadhani amekosea au mnaonaje wenzangu?

Hapana yuko sawa kulingana muktadha wa stori yenyewe ukimwambia mtu anyooshe kidole wengine wanahisi umewadharau , umewashushia heshima hawajui, utaka kufundisha wakati yeye amesoma au unamfanya mwanafunzi wa shule, so mimi naona yuko sawasawa.
 
Back
Top Bottom