Ya Mabina: Tumepata mafunzo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nipende kuchukua nafasi hii kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu Clement Mabina na kusema kuwa Mabina alazwe anapostahili. Pia, nalaani mauaji hayo kwa nguvu zangu zote kwakuwa ni kinyume na Sheria na taratibu za nchi tulizojiwekea. Vitendo vya namna ile si vya kuvifumbia macho wala kuvikumbatia. Ni vya kuvilaani na kuvitokomeza.

Tukio la kuuwawa kwa Mabina pale Kisesa-Mwanza lina sura mbalimbali. Lina sura ya kisiasa;kijamii,kiuchumi na kiutamaduni.Nitajaribu kuelezea sura hizi na mafunzo yake. Mtaniwia radhi kwakuwa mngoni ataelezea tamaduni za wasukuma ingawa ni chembe tu.

Sura ya kisiasa. Marehemu Mabina alikuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Mwanza. Hadi mauti yanamkuta,alikuwa Diwani wa Kisesa(kama niko sahihi). Nafasi hizi za kisiasa zina jambo la kusema.Clement Mabina alikuwa mwanasiasa na kiongozi.Tena ndani na kupitia chama tawala. Hakuwa mtu mdogo. Hadhi hii aliyokuwa nayo ndiyo, kwa maoni yangu, iliyomfanya afanye alivyofanya. Kulikuwa na kiburi cha kisiasa na kiuongozi ndani yake. Kwamba hagusiki wala hatishwi. Yakatokea yaliyotokea.

Sura ya kijamii. Tukio la Kisesa limeonesha matabaka na jinsi matabaka hayo yanavyoweza kupambana. Marehemu Mabina alikuwa na uchumi mzuri ukilinganisha na wanachi wake walio wengi. Ndiyo kusema yeye alikuwa tabaka la juu;wananchi la chini. Kama ilivyo ada, tabaka la juu hutaka mazuri yote na ikiwezekana yote. Au mengi sana. Magari,nyumba,viwanja,biashara na kadhalika. Wa tabaka la chini kinyume chake. Hivyobasi, Kisesa ilikutanisha matabaka mawili ya kijamii yaliyokinzana na kusababisha kilichotokea.

Sura ya kiuchumi. Wananchi wengi ni maskini Kisesa.Tena waliokuwa wakiongozwa na Mabina. Maumivu ya umaskini wao ni makali lakini wanajitahidi kuvumilia. Wanavumilia huku wakijishughulisha kwa bidii kupata ahueni kama wenzao wenye uchumi wenye afadhali. Umaskini wao ni kidonda kibichi lakini kilichopoa maumivu. Njia pekee ya kutotesha maumivu hayo ni ubabe. Ubabe hutafsiriwa kama dharau,kiburi,kutojali,kujiamini na kadhalika. Ubabe ni kama msumari wa moto kwenye kidonda cha maskini. Haufai. Kisesa, ubabe umeripotiwa pia. Mambo yakatokea hivyo.

Sura ya kiutamaduni. Nianze na utamaduni wa kisiasa. Watanzania huwaheshimu sana viongozi wao.Haijalishi kama waliwachagua au la. Huwasikiliza;hufuata ushauri wao kama viongozi na kusonga mbele kuelekea maendeleo ya nchi hii. Watanzania ni wapole;wafuata sheria;watii na wema. Ndiyo mhimili wa amani tuliyonayo. Halafu, wasukuma ni wasikivu na wanyeyekevu mno. Wanastahili sifa.

Lakini, kwanini wamshambulie had kufa kiongozi wao na mmoja wao? Lazima kulikuwa na jambo. Kiutamaduni,wasukuma wa Mwanza na kwingineko, hawana hulka ya kushambulia wala kubishana na viongozi wao. Hii ni hasa pale viongozi hao wanapokuwa wakitimiza majukumu yao. Pale Kisesa,Marehemu Mabina hakuwa kiuongozi.Alikuwa kijamii. Kiutamaduni. Je, alikwenda kinyume na utamaduni wa kisukuma? Sisi tumearifiwa tu yaliyotokea.

Ndugu zangu watanzania, amani tuliyonayo Tanzania ni tunda la mti wetu wenyewe. Mti wa kuheshimiana,kusikilizana,kusaidiana,kutaniana,kusemana,kuonyana,kuongozana na kadhalika. Ni sisi tunaoumwagia maji mti huu kila uchao ili uzidi kutoa matunda ya amani haki na umoja. Hatutachoka kufanya hivyo.

Lakini, kila mmoja wetu ana wajibu wa kuheshimu mwingine. Kumheshimu ni kutambua haki zake na kumsaidia kuzipata.Si kufanya kinyume. Si kunyanyasana. Si kuhitilafiana.Si kugombana.Si kudharauliana.Na si kuleteana ubabe usio na maana.

Amini nawaambia, hakuna siasa au mwanasiasa aliye juu ya watu. Hakuna haki isiyohusu watu. Hakuna wajibu usiotekelezwa na watu. Watu ndiyo kila kitu. Mliopo juu,kati na chini mjue hili. Kwa kila tukio,tuna la kujifunza. Hapa pia kwa Marehemu Clement Mabina lipo la kujifunza.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Juzi Mh. Lema alilalamikia watu wanaomilikishwa silaha kutokufuatiliwa kama bado wana akili timamu. Waziri mkuu Mh. Pinda alisema nadhani ni kwa kejeli kuwa wataanza kufuatilia wamiliki wa silaha katika jimbo la Arusha mjini. Kama Mabina alikuwa anajihami ni kwa nini ampige mtoto?

Kuchukua sheria mkonani ni dalili ya umma kupoteza imani na serikali pamoja na mahakama!
 
Umejiuliza swali la kwa nini wamshambulie kiongozi wao,ina maana hujui kwamba aliua mtu kabla ya kuuawa?sidhani kama upole wa Wasukuma ni wa kuvumilia hadi ndugu yao kuuawa mbele yao.Sidhani kama yangetokea haya kama asingeua
 
Pole yake sana innocent boy aliyeuwawa na MABINA.
Mungu amuweke mahali pema peponi.
 
Nipende kuchukua nafasi hii kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu Clement Mabina na kusema kuwa Mabina alazwe anapostahili. Pia, nalaani mauaji hayo kwa nguvu zangu zote kwakuwa ni kinyume na Sheria na taratibu za nchi tulizojiwekea. Vitendo vya namna ile si vya kuvifumbia macho wala kuvikumbatia. Ni vya kuvilaani na kuvitokomeza.

Tukio la kuuwawa kwa Mabina pale Kisesa-Mwanza lina sura mbalimbali. Lina sura ya kisiasa;kijamii,kiuchumi na kiutamaduni.Nitajaribu kuelezea sura hizi na mafunzo yake. Mtaniwia radhi kwakuwa mngoni ataelezea tamaduni za wasukuma ingawa ni chembe tu.

Sura ya kisiasa. Marehemu Mabina alikuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Mwanza. Hadi mauti yanamkuta,alikuwa Diwani wa Kisesa(kama niko sahihi). Nafasi hizi za kisiasa zina jambo la kusema.Clement Mabina alikuwa mwanasiasa na kiongozi.Tena ndani na kupitia chama tawala. Hakuwa mtu mdogo. Hadhi hii aliyokuwa nayo ndiyo, kwa maoni yangu, iliyomfanya afanye alivyofanya. Kulikuwa na kiburi cha kisiasa na kiuongozi ndani yake. Kwamba hagusiki wala hatishwi. Yakatokea yaliyotokea.

Sura ya kijamii. Tukio la Kisesa limeonesha matabaka na jinsi matabaka hayo yanavyoweza kupambana. Marehemu Mabina alikuwa na uchumi mzuri ukilinganisha na wanachi wake walio wengi. Ndiyo kusema yeye alikuwa tabaka la juu;wananchi la chini. Kama ilivyo ada, tabaka la juu hutaka mazuri yote na ikiwezekana yote. Au mengi sana. Magari,nyumba,viwanja,biashara na kadhalika. Wa tabaka la chini kinyume chake. Hivyobasi, Kisesa ilikutanisha matabaka mawili ya kijamii yaliyokinzana na kusababisha kilichotokea.

Sura ya kiuchumi. Wananchi wengi ni maskini Kisesa.Tena waliokuwa wakiongozwa na Mabina. Maumivu ya umaskini wao ni makali lakini wanajitahidi kuvumilia. Wanavumilia huku wakijishughulisha kwa bidii kupata ahueni kama wenzao wenye uchumi wenye afadhali. Umaskini wao ni kidonda kibichi lakini kilichopoa maumivu. Njia pekee ya kutotesha maumivu hayo ni ubabe. Ubabe hutafsiriwa kama dharau,kiburi,kutojali,kujiamini na kadhalika. Ubabe ni kama msumari wa moto kwenye kidonda cha maskini. Haufai. Kisesa, ubabe umeripotiwa pia. Mambo yakatokea hivyo.

Sura ya kiutamaduni. Nianze na utamaduni wa kisiasa. Watanzania huwaheshimu sana viongozi wao.Haijalishi kama waliwachagua au la. Huwasikiliza;hufuata ushauri wao kama viongozi na kusonga mbele kuelekea maendeleo ya nchi hii. Watanzania ni wapole;wafuata sheria;watii na wema. Ndiyo mhimili wa amani tuliyonayo. Halafu, wasukuma ni wasikivu na wanyeyekevu mno. Wanastahili sifa.

Lakini, kwanini wamshambulie had kufa kiongozi wao na mmoja wao? Lazima kulikuwa na jambo. Kiutamaduni,wasukuma wa Mwanza na kwingineko, hawana hulka ya kushambulia wala kubishana na viongozi wao. Hii ni hasa pale viongozi hao wanapokuwa wakitimiza majukumu yao. Pale Kisesa,Marehemu Mabina hakuwa kiuongozi.Alikuwa kijamii. Kiutamaduni. Je, alikwenda kinyume na utamaduni wa kisukuma? Sisi tumearifiwa tu yaliyotokea.

Ndugu zangu watanzania, amani tuliyonayo Tanzania ni tunda la mti wetu wenyewe. Mti wa kuheshimiana,kusikilizana,kusaidiana,kutaniana,kusemana,kuonyana,kuongozana na kadhalika. Ni sisi tunaoumwagia maji mti huu kila uchao ili uzidi kutoa matunda ya amani haki na umoja. Hatutachoka kufanya hivyo.

Lakini, kila mmoja wetu ana wajibu wa kuheshimu mwingine. Kumheshimu ni kutambua haki zake na kumsaidia kuzipata.Si kufanya kinyume. Si kunyanyasana. Si kuhitilafiana.Si kugombana.Si kudharauliana.Na si kuleteana ubabe usio na maana.

Amini nawaambia, hakuna siasa au mwanasiasa aliye juu ya watu. Hakuna haki isiyohusu watu. Hakuna wajibu usiotekelezwa na watu. Watu ndiyo kila kitu. Mliopo juu,kati na chini mjue hili. Kwa kila tukio,tuna la kujifunza. Hapa pia kwa Marehemu Clement Mabina lipo la kujifunza.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

heko kwa hekima uliyo nayo mkuu
 
Mleta uzi umeangalia upande mmoja wa shillingi na kuuacha upande wa pili. Ni kwanini wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi? Ni kweli wasukuma ni wapole lakini upole wao si kigezo cha mtu kummua mwingine mbele yao halafu eti tulitegemea waendelee na upole wao.

Tiba
 
Back
Top Bottom