Ya Leo Kali: Kiingereza Ni Lugha Tu, Hata Watoto Wanaongea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Leo Kali: Kiingereza Ni Lugha Tu, Hata Watoto Wanaongea!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mbea, Oct 20, 2010.

 1. m

  mbea Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya Leo Kali: Kiingereza Ni Lugha Tu, Hata Watoto Wanaongea!

  [​IMG]

  ( Mjadala unaposhika kasi, mjumbe hapa chini kaamua kumfungia mtu kazi. Mwenyekiti nasema tuendelee tu!)

  Narudia tena bwana Mhango na wenzio wote mliokosa malezi mlikotoka, matusi yenu yote mnayoelekeza kwangu na kwa wengineo, kidole kimoja tu ndio chanielekea mimi, vitatu vyakutazama mwenyewe!

  Na hiyo style yenu ya kunyamazisha watu kwa kuwaita mafisadi haisadii, hiyo style yenu ya kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kutukana watu kinaonyesha kuwa mmeishiwa kifikra na kimtazamo, inaonyesha sononi mlizo nazo. Maana kama si sononi ni nini sasa kinachokufanya ukimbilie matusi yote hayo? Huna majibu yenye mashiko?

  Na nakuhurumia kweli kama kipimo cha elimu kwako wewe ni kujua kiingereza! Hala baba sikujua kama wewe bado hujajikomboa na ni mtumwa wa kimawazo, kifikra na kitamaduni. Kiingereza ni lugha kama kimasai, kimatumbi na kiswahili na sio kiashiria cha usomi. Ingekuwa ni usomi basi waingereza wote wasingekwenda shule wangekaa majumbani mwao kwa kuwa wanajua kiingereza. Na watu wengine wote wangejifunza kiingereza kama lugha kisha tayari wakawa wasomi wa fani mbali mbali badala ya kwenda darasani kwa kutumia lugha zao za kichina, kifaransa, kilatini na nyinginezo.

  Pamoja na kujifaragua kote bado hujajibu hoja yangu ya kuonyesha scientific/empirical evidence ya madai yako, zaidi ya kumwaga propaganda zisizo na mashiko na kukimbilia kubadili mada, jibu hoja, leta evidence hapa kijiweni, onyesha usomi wako kwa kutupa data zinazosupport claim yako. Nadhani hilo huna ndio maana nikasema wewe sio Greatthinker, ni mbabaishaji tu unayetafuta umaarufu mgongoni mwa Greatthinking, eti unabii! Kwenye Greatthinking hakuna unabii kwa sababu hakuna imani, sasa inawezekana uliona tu hilo neno ukaamulia kulitumia ili uonekane ni mwanafalsafa, labda mwanafalsafa wa matusi lakini sioni mpaka sasa falsafa yoyote inayotoka kwako. Na tena mwanafalsafa haogopi criticism na wala hajibu critics zozote kwa matusi bali kwa logical reasoning.

  Mwisho unataka kujua kuwa mimi ni mwanamke au mwanaume ili iweje? Gender yangu itakusaidia nini kwenye majadiliano? Unataka kujua jina langu ndio litakupa majibu ya maswali yangu? Au kwa jinsi ulivyo wala huamini kuwa Msafiri ni jina langu au Msafiri laweza kuwa jina la mtu? Au nyie ndio wale majina mpaka yawe ya kizungu ndio yanaweza kuwa majina ya watu?

  Heri yangu mimi sijasoma kama usomi wenyewe ndio huo.

  Msafiri Kafiri!
  Kiingereza ni lugha tu hata watoto wanaongea!!!!
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!ni kweli kabisa!
   
Loading...