Ya Kweli Haya? Amua Mwenyewe

Jan 1, 2008
23
0
Sijui kama habari hizi ni kweli, lakini kama ni kweli Watanzania tuna hali mbaya.

Yasemekena kuwa kwenye kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichochagua uongozi mpya kilichomalizika Dodoma hivi karibuni Waziri Mkuu Edward Lowassa, na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba hawakupata zile kura ambazo zilitangazwa na vyombo vya habari baada ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari, katika kundi la wagombea 20 kura za Lowassa zilikuwa 1,681, akifuatiwa na Andrew Chenge (1,530), na Yusuph Makamba (1,510).

Kwa mujibu wa habari hizo hizo, wengine walioshinda kwenye kundi hilo ni Bernard Membe (1,281), Jaka Mwambi (1,239), Profesa Juma Kapuya (1,216), Abdulrahman Kinana (1,204), Christopher Gachuma (1,181), Aggrey Mwanri (1,068), Stephen Wassira (1,107), Makongoro Mahanga (1,067), Frederick Sumaye (1,065), John Komba (1,056), Kingunge Ngombale Miwiru (1,023), William Lukuvi (943), John Chiligati (910), Amos Makala (871), Profesa Samwel Wangwe (817), Profesa David Mwakyusa (754), na Jackson Msome (747).

Habari zisizo rasmi zinasema kuwa uwkeli ni kuwa Lowassa na Makamba hawakupata kura za kutosha kushinda nafasi zao na kulichotokea ni kuwa waliondolewa wagombea wawili waliyoshika nafasi ya 19 na 20 ili kutoa nafasi kwa washindwa hao. Aidha, ili kuwapa hadhi inayofanana na nyadhifa zao, walipachikwa ushindi wa namba moja (Lowassa), na namba tatu (Makamba).

Habari zisizo rasmi zinaendelea kusema kuwa aliyeshika nafasi ya kwanza kwenye kundi la 20 alikuwa Andrew Chenge, na ya pili ilichukuliwa na Christopher Gachuma.

Hali mbaya kwa Watanzania inakuja kwa namna mbili. Kwanza, kama haya ni ya kweli ina maana Waziri Mkuu Lowassa na Katibu Mkuu Makamba hawaungwi mkono na chama chao wenyewe kwa sababu ambazo ingekuwa vizuri kwa Watanzania kuzifahamu. Na kama Lowassa hakubaliki kwenye chama chake, Watanzania wengine tuna sababu gani ya kumkubali? Katibu Mkuu wa CCM ni wa wana CCM pekee, lakini Waziri Mkuu anaongoza Watanzania wote, wenye vyama na wasiyo na vyama, hivyo ni haki ya kila Mtanzania kufahamu kwa nini Lowassa hakupata kura za kutosha kushika nafasi muhimu katika uongozi wa juu wa chama chake?

Pili, kama Andrew Chenge ndiyo kweli aliongoza kundi la 20, na Christopher Gachuma alikuwa wa pili, na baadae taarifa rasmi zinatueleza kuwa Chenge kashika nafasi ya pili, na Gachuma kashika nafasi ya saba tuna uhakika gani na ukweli wa hayo majina mengine kwenye orodha hiyo na kura zao? Tunaweza kuuliza: tuna hakika gani na matokeo yote ya uchaguzi huo muhimu kwa CCM na kwa Tanzania?

NA MENGINE HAYA, SIJU NAYO KWELI?

Inasemekana kuwa Waziri Mkuu Lowassa ananuwia kugombea urais 2010. Ndiyo, 2010, siyo 2015 kama ambavyo imekuwa desturi ya CCM kumuacha rais aliye madarakani kuongoza kwa vipindi viwili vya miaka mitano. Sasa hizi zinaweza kuwa ni porojo tu za washindani wenzake wanaowania urais mwaka 2015. Lakini kuna muelekeo kuwa atawania urais mwaka 2015.

Matarajio ni kuwa atakapochukuwa fomu kuwania urais mwaka 2015 hawa CCM wenzake ambao wanasemekana walimbwaga chini Dodoma hivi karibuni hawatakuwepo kwenye Mkutano Mkuu utakaochagua mgomeba rais wa CCM, na kama wakiwepo basi Watanzania tutatarajia kuwa watambwaga tena chini au wakimpitisha watueleze imekuwaje mwaka 2007 alikuwa hafai, na mwaka 2015 mpaka 2025 anafaa?

Kama haya yote ni kweli, siku Edward Lowassa anaapishwa kuwa Rais wa Tanzania kwa kipindi cha 2015 mpaka 2025 Watanzania itabidi tucheke sana. Au sijui itabidi tulie?

Somo la leo: Tumewachagua sisi wenyewe, wewe na mimi

Foti Mwarobaini
 
Viongozi wa CCM wamekuwa hawasemi ukweli hasa ukitilia maanani kashfa za hivi karibuni kuhusiana na kusaini mkataba wa Buzwagi ambapo walikataa kata kata kwamba mkataba huo umesainiwa UK mpaka pale ukweli ulipodhihiri, na pia kashfa ya BOT ambapo walikataa kata kata kuhusiana na kashfa mbali mbali ndani ya chombo hicho. Hivyo hili pia linaweza kuwa na ukweli. CCM hawaminiki tena.
 
Lowassa akigombea 2015 ataangushwa tu kama ilivyokuwa kwa Msuya na baadaye Sumaye.

CCM watakuwa wamechoka mno na mambo ya akina JK na Lowassa na matokeo yake atatemwa tu.

Sijui na yeye baada ya hapo ataenda Havard kusoma?
 
sina uhakika kama ni kweli ,lakini kutokana na matendo yaliyotokea na yanayoendelea kuzunguzwa (Buzwagi,BOT nk)na vile vile historia ya CCM.najiuliza-
je kwa hali na mwendo huu ,tutafika kweli??
kila kitu tunababaisha yaani longo longo kibao.
 
Sasa kama wanaibiana wao kwa wao wataacha kuwaibia wapinzani? Mwizi akikosa wa kumuibia huhamisha fedha kutoka mfuko wa kulia kwenda wa kushoto.
 
Hii ni kweli kabisa,na tuliisha ijadili baada tu ya uchaguzi.Kilichotokea ni kwamba,Lowassa kwanza ilisemekana alipata kura 600 na Makamba 300,lakini baadae ilibainika kuwa Lowassa alipata kura 300 na Makamba alipata 150.Hizi habari zilifikishwa kwa mwenyekiti wao(JK) na inasemekana aliagiza zitangazwe kama zilivyo.Ilibidi usalama wa Taifa upeleke habari hizi kwa Mwinyi na Mkapa ambao wakamshauri JK zisitangazwe kama zilivyo,maana haitaleta picha nzuri ndani ya serikali yake.Ndio hapo zikawa doctored.
Inasemekana Lowassa alitoa machozi alipopata hizo taarifa....
Tunae sana tu bado!
 
Pamoja na uozo huo, come election, CCM watachaguliwa kwa kishindo. Wadanganyika bwana...tuna mambo!
 
Hii ni kweli kabisa,na tuliisha ijadili baada tu ya uchaguzi.Kilichotokea ni kwamba,Lowassa kwanza ilisemekana alipata kura 600 na Makamba 300,lakini baadae ilibainika kuwa Lowassa alipata kura 300 na Makamba alipata 150.Hizi habari zilifikishwa kwa mwenyekiti wao(JK) na inasemekana aliagiza zitangazwe kama zilivyo.Ilibidi usalama wa Taifa upeleke habari hizi kwa Mwinyi na Mkapa ambao wakamshauri JK zisitangazwe kama zilivyo,maana haitaleta picha nzuri ndani ya serikali yake.Ndio hapo zikawa doctored.
Inasemekana Lowassa alitoa machozi alipopata hizo taarifa....
Tunae sana tu bado!

kwa hapa baba nnakupongeza kwa kudhani kuwa unazungumza na watoto wenzio


pole sana mwenzetu, ndivyo mnavyopeana tumbaku hivi?
 
TZ yawezekana ila SOUTH AFRICA. Kama watu hawakutaki kwanini ugombee au ung'ang'anie MADARAKA?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom