Ya kina Mbowe, Lipumba na Mbatia ni hasara kwa upinzani na Taifa lkn faida kwa CCM.

lulumba

Member
Mar 23, 2014
60
67
Watanzania wazalendo, waerevu na wapenda mageuzi ni wengi sana, na wangependa kuwepo na mabadiliko ya kidemokrasia kuanzia ndani ya vyama vya siasa halafu baadae katika nchi kupitia chaguzi zinazoendeshwa kidemokrasia na kufuata katiba adilifu sio katiba za kupitishwa kiujanjaujanja. Chama chenye viongozi waadilifu na wapenda demokrasia ya kweli kitapendwa na kila mtanzania hata bila maaandamano na muda ukifika kitapewa dola na raia.

Lakini tunaangushwa kwanza kabisa ndani ya vyama vyetu mbadala vya siasa. Sioni km kuna demokrasia ya kweli na ukomo wa madaraka ukiheshimiwa ndani ya vyama mbadala. Sioni "haki kwa wote" ikifanya kazi ndani ya CUF. Sioni mageuzi ya kimaendeleo ndani ya NCCR Mageuzi. Sioni demokrasia ya kweli ya kimaendeleo ndani ya Chadema. Kote huko mambo ni yale yale demokrasia/udikteta mchafu ama demokrasia/udikteta vuguvugu kwa kupunguza ukali ya maneno.

Demokrasia ya kweli na kuheshimu katiba adilifu ingeanza ndani ya vyama vya siasa tungekuwa na mfano hai wa jinsi demokrasia ya kweli na katiba bora ktk nchi ingelipaswa kuwa. Nyerere alitufundisha kurekebisha demokrasia ati ifanane na mazingira, basi imekuwa nongwa: fungulia mbwa na uchafu mtupu. Kama tunaisiginya demokrasia ktk vyama tusitegemee ktk nchi tukawa na demokrasia ya kweli. "Charity starts at home".

CCM wakiachia madaraka ndio wajue kwaheri maana watakaochukua ni walewale ambao ktk vyama vyao wameshindwa kuwa na demokrasia, je wakipewa nchi watabadilika?

Hatutaweza kuwa na maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutawala bila kuwa na demokrasia ya kweli. Demokrasia hiyo lazima ianzie katika vyama mbadala. Udikteta mtukufu (benovalent dictatorship) ulimshinda Nyerere hatutarajii kama kuna atakayeweza tena japo kuna nafasi na upenyo mkubwa wa udikteta mtukufu kutokana na Raisi kurundikiwa madaraka hata kwenye rasimu mpya ya katiba ya CCM. Tulishindwa na tumeshindwa kutumia udikteta mtukufu basi tujaribu demokrasia ya kweli, utawala wa sheria na haki.

Km ilivyo ktk udikteta mtukufu nchi hupata maendeleo haraka maana watu hulazimishwa kufanya kazi na huwa wabunifu kuwaridhisha wakubwa na mfumo ulioko. Ukienenda kinyume na matakwa ya mkubwa ama wakubwa mfumo utakushughulikia hata kupoteza uhai wako.Tunayaona hayo kwa jirani zetu Rwanda na Uchina.

Ndivyo ilivyo kwa demokrasia ya kweli na utawala wa sheria wa haki kila mtu hula kwa jasho lake na hivyo huwalazimisha watu kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa wabunifu. Maisha yanakuwa ni kazi bila ujanjaujanja wote wote. Ukikosa sheria inachukua mkondo bila kuangalia wewe ni nani na una nafasi gani. Maisha-Demokrasia ya kweli-utawala wa sheria na haki;Hapo kila mtu atafanya kazi, mifumo itafanya kazi kwa haki na umahiri mkubwa na hatimaye maendeleo.

Hii ndio faida tutakayopata tukiwa na demokrasia ya kweli na tukiziheshimu katiba za vyama vyetu kuanzia ndani ya vyama na baadae Taifa/nchi yetu. Msingi wa demokrasia ya kweli kwa sababu tuko katika vyama vingi unatakiwa uanze kwenye vyama vyetu mbadala. Chama kinachoongoza kimeshindwa vyote viwili udikteta mtukufu na demokrasia ya kweli. Tumekuwa washabiki wa udikteta mchafu wa chama na demokrasia kiuwongo uwongo kwa sababu ndicho kinacholelewa na chama kilichoko madarakani na sasa ndani ya vyama mbadala. Hatuna pakukimbilia.

Wanayofanya kina Mbowe, Lipumba, Seif na Mbatia, achilia mbali kina Mrema, Cheyo, Mtikila na wengineo km hao kina madhara kwa demokrasia na utawala wa sheria na haki ktk Taifa. Udikteta/Demokrasia vuguvugu ktk vyama ni hasara kwa Taifa zima na ni faida kwa watawala-CCM.

Watanzania tusimame tuwakatae wote kiuzalendo, sio kiushabiki wa vyama. Mbowe, Lipumba, Mbatia safisheni kwanza vyumba vyenu mnakolala kabla ya sebule jiko na baadae nyumba nzima.CCM uchafu mnaoufanya tunaufahamu na majibu tunayo tunasubiri wakati, chama muafaka na viongozi waadilifu. CCM ni janga la kitaifa na ni adui wa haki!
 
Watanzania wapenda mageuzi ni wengi sana, na wangependa kuwepo na mabadiliko ya kidemokrasia kuanzia ndani ya vyama vya siasa halafu baadae katika nchi kupitia chaguzi zinazoendeshwa kidemokrasia na kufuata katiba adilifu sio katiba za kupitishwa kiujanjaujanja.

Lakini tunaangushwa kwanza kabisa ndani ya vyama vyetu vya siasa. Sioni km kuna demokrasia halisi na ukomo wa madaraka ukiheshimiwa. Sioni "haki kwa wote" ikifanya kazi ndani ya CUF. Sioni mageuzi ya kimaendeleo ndani ya NCCR Mageuzi. Sioni demokrasia halisi yakimaendeleo ndani ya Chadema. Kote huko mambo ni yale yale.

Demokrasia halisi na kuheshimu katiba adilifu ingeanza ndani ya vyama vya siasa tungekuwa na mfano hai wa jinsi demokrasia halisi na katiba bora ktk nchi ingelipaswa kuwa. Nyerere alitufundisha kurekebisha demokrasia ati ifanane na mazingira, basi imekuwa fungulia mbwa na uchafu mtupu. Km tunaisiginya demokrasia ktk vyama tusitegemee ktk nchi tukawa na demokrasia ya kweli. CCM wakiachia madaraka ndio wajue kwaheri maana watakaochukua ni walewale ambao ktk vyama vyao wameshindwa kuwa na demokrasia.

Sio kwamba CCM hawapendi demokrasia halisi, sio kwamba CCM hawapendi kuachia madaraka na sio kwamba CCM hawapendi katiba bora ila ni nani atakuwa mwadilifu na muumini mzuri wa demokrasia halisi atakaechukua nchi na kuruhusu demokrasia na utawala wa sheria vichukue mkondo wake.

Km ilivyo ktk udikteta halisi nchi hupata maendeleo haraka maana watu hulazimishwa kufanya kazi na huwa wabunifu kuwaridhisha wakubwa. Ndivyo ilivyo kwa demokrasia halisi na utawala wa sheria wa haki kila mtu hula kwa jasho lake na hivyo huwalazimisha watu kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu. Maisha yanakuwa ni kazi bila ujanjaujanja wote wote.

Hii ndio faida tutakayopata tukiwa na demokrasia halisi na tukiziheshimu katiba za vyama vyetu kuanzia ndani ya vyama na baadae Taifa/nchi yetu.

Wanayofanya kina Mbowe, Lipumba, Seif na Mbatia, achilia mbali kina Mrema, Cheyo, Mtikila na wengineo km hao kina madhara kwa demokrasia na utawala wa sheria ktk Taifa. Udikteta vuguvugu ktk vyama ni hasara kwa Taifa zima na ni faida kwa CCM.

R U Serious ??? sasa kama ni HASARA MBONA wanasema Rais kakubaliana na TCD kuhusu Katiba na Serikali tatu? kabla ya kuweka hii article yako Ungesoma iliyo juu yako inayosema kuwa....
Rais Kikwete akutana na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ikulu ndogo Dodoma

Started by Informer, Today 10:56 1234



c.c lulumba


Au ulikuwa unakimbilia PESA za Breakfast MONDAY MORNING huko LUMUMBA???


Wataje kwa Majina yao Leo huko IKULU - DODOMA... Your HomeWork


uk16.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
R U Serious ??? sasa kama ni HASARA MBONA wanasema Rais kakubaliana na TCD kuhusu Katiba na Serikali tatu? kabla ya kuweka hii article yako Ungesoma iliyo juu yako inayosema kuwa....
Rais Kikwete akutana na Wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Ikulu ndogo Dodoma

Started by Informer, Today 10:56 1234



c.c lulumba


Au ulikuwa unakimbilia PESA za Breakfast MONDAY MORNING huko LUMUMBA???


Wataje kwa Majina yao Leo huko IKULU - DODOMA... Your HomeWork


uk16.jpg

Usiende na matukio na ushabiki. Hio mikutano ilianza toka enzi za kutungwa sheria ya kusimamia utungwaji wa katiba mpya lkn bado ilikuja ya hovyio na ikawapa nafasi CCM kujaza watu wao ktk BMK, Tume imevunjwa hata website yao haipo tena. Je mikutano hio ilisaidia? Huoni hayo. Msingi wa nyumba ndio uimara wa nyumba sio urembo na rangi ya nyumba." Nyumba ikiwa nzuri ya kupendeza halafu baadae ikapasukapasuka kwa kukosa msingi imara huwezi ukasema ilikuwa imara bali ilipendeza lkn ilikuwa dhaifu. Fikiria kwa kina rafiki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom