Ya Kanumba: Konzo ya Maji Haifumbatiki na Mvumbika Changa Hula Mbovu

That only happens in DANGANYIKA land.

wewe hujajua miti yote ya ccm imeteleza wanatafuta sehemu ya kujishikiza sasan wanadhani kuwa wapenzi wa kanumba watakuwa wapenzi wa ccm ndo maana wanaenda hapio kujionyesha
 
Unanikumbusha msiba wa mzee Kipara Mungu aiweke pema peponi roho yake Amin, nashindwa kuelewa vigezo vilivyotumika wanasiasa kama kina Sugu cdm na mawaziri wa serikali kuuuteka msiba wa Kanumba lakini hawakuwa na msaada wowote wakati mzee Kipara akiugua na hawakushiriki msiba wa mzee yule.

Lazima kuna jambo si bure!
 
mimi ni mshabiki mzuri sana kazi nzuri za sanaa. Nilimkubali marehemu kanumba katika jitijada zake katika kuiendeleza tasnia ya filamu za kibongo. Kibinadamu, inasikitisha kwa taa ya kijana kama huyu kutoweka ghafla katika umri wa ujana wake.
Pamoja na hayo, zipo hisia, maneno na matendo yaliyoibuka wakati wa msiba hadi mazishi yake ambayo sikubaliani nayo. Hapa nimeamua kuwashirikisha maana konzo ya maji haifumbatiki kiganjani, itapenya tu! Pamoja na kwamba alikuwa maarufu (bongo celeb),
1. Hakukuwa na haja ya viongozi wengi wa ngazi za juu kuacha shughuli nyingine nyeti za taifa kwenda msibani, kusaini vitabu na kuhudhuria mazishi. Ni bayana kuwa huyu hakuwa kiongozi wa serikali, hata wawakilishi tu wa hao wakubwa wetu wangeweza kuwawakilisha vyema. Fikiri kuwa waziri (na naibu wake) wa habari, vijana na michezo wote hawakuonekana kujibu swali husika katika kikao cha 7 cha bunge la 10 eti kwa kuwa walikuwa kwenye msiba wa msanii maarufu! Wapi vipaumbele vyetu kama taifa.

2. Ilishangaza waziri kutangaza kutoa mchango wa tshs.15 m (kwa niaba ya serikali) na pia (tulisikia) kuwa serikali iligharimia maziko yake. Ni kigezo gani kimetumika kuamua hivyo na pia kwa uamuzi wa nani aliyeidhinisha matumizi hayo? Ni bongo stars wangapi wamefariki bila hata mchango wowote (toka serikalini) na hata kama tungelinganisha michango yao katika jamii mfano akina sembuli, remmy, tx moshi, marijani n.k basi hata tungesikia kiwango kama hicho au hata angalau nusu yake. Utashangaa kusikia kuwa mimi babu yangu alifariki na alikuwa mwenyekiti (mwadilifu) wa ccm (m) na mjumbe kwenye jumuiya ya ccm (t) lakini cha ajabu hata hatukuona hata salamu tu za maandishi za rambirambi toka kwa mwenyekiti wa ccm (t) kwa wafiwa hata mjane wa babu yetu hajawahi kutembelewa wala kupewa mkono wa pole hata siku moja! Vitendo kama hivi vinatafsirika kuwa ni matumizi zaidi ya hisia (feelings) kuliko taratibu na kanuni zinazotuongoza na huleta manungúniko ambayo hayataisha kwa wengine wengi (nimewataja wachache tu).

3. Inasikitisha watu wengi (akiwamo mchungaji muongoza mazishi, mkuu wa nchi na waziri wa hvm) tunapotoa wasifu wa kanumba, eti "kijana mwenye tabia nzuri ya mwenendo wa maisha wa kuigwa katika jamii" nayo ni sifa yake. Je, hii ni kweli? Kwa vile wakati pumzi ya mtu imekoma huwa hatusemi mabaya basi tungeishia hapo tu katika kumsifia weledi wake katika kazi ya sanaa ya kuigiza na filamu. Kusema kuwa vijana wengine waige tabia ya mwenendo wa maisha yake ni kuvumbika changa ambayo itawaletea vijana wanaoiga wale mbovu!

Tuwe wakweli na tuwasaidie wasanii wengi, wasomi na pia wanasiasa maarufu hasa katika kipengele cha mienendo ya maisha yao ili waendelee kuishi maisha marefu wakitoa michango yao mbalimbali ya vipawa walivyojaliwa na mungu.

Nami mungu anisamehe na muendelee kuniombea maana katika hili nami si mfano wa kuigwa kabisa!

rip the great kanumba!!!!!mengi yatasemwa,lakini msiba huu umetuonyesha tuna viongozi wa ajabu sana kupata kutokea nchi hii!!!amin usiamin mambo kama haya yanatokea kwenye nchi zetu hizi za ajabu ajabu,cdhani jambo kama hili linaeweza kutokea hata ghana baada ya kuidemoktisha nchi yao!!labda la msingi hapa pamoja na hila zote kwenye katiba mpya,watanzania tuhamasishane kila mwananchi apate fursa ya kunena,pengine tutakuwa na katiba bora ambayo itaweza kukuwawajibisha watu kama hawa wakina nchimbi na naibu!!!inakuaje mmoja wapo asiwepo bungeni kuratibu shughuli za wizara yake zitazohitaj maelezo kutoka bungeni?tanzania yetu hii ni kioja!!!tunadhani kila event ni sehemu muhafaka wa kujenga taswira ya chama!!!!!nasema hapana hapana,big no!!!hata watanzania wote museme yes!!!mi nasema hapana,big no!!
 
Mimi ni mshabiki mzuri sana kazi nzuri za sanaa. Nilimkubali Marehemu Kanumba katika jitijada zake katika kuiendeleza Tasnia ya Filamu za kibongo. Kibinadamu, inasikitisha kwa taa ya kijana kama huyu kutoweka ghafla katika umri wa ujana wake.
Pamoja na hayo, zipo hisia, maneno na matendo yaliyoibuka wakati wa msiba hadi mazishi yake ambayo sikubaliani nayo. Hapa nimeamua kuwashirikisha maana konzo ya maji haifumbatiki kiganjani, itapenya tu! Pamoja na kwamba alikuwa maarufu (Bongo Celeb),
1. Hakukuwa na haja ya Viongozi wengi wa ngazi za juu kuacha shughuli nyingine nyeti za Taifa kwenda msibani, kusaini vitabu na kuhudhuria mazishi. Ni bayana kuwa huyu hakuwa Kiongozi wa Serikali, hata Wawakilishi tu wa hao wakubwa wetu wangeweza kuwawakilisha vyema. Fikiri kuwa Waziri (na Naibu wake) wa habari, Vijana na Michezo wote hawakuonekana kujibu swali husika katika Kikao cha 7 cha Bunge la 10 eti kwa kuwa walikuwa kwenye msiba wa Msanii maarufu! Wapi vipaumbele vyetu kama Taifa.

2. Ilishangaza Waziri kutangaza kutoa mchango wa Tshs.15 M (kwa niaba ya Serikali) na pia (tulisikia) kuwa Serikali iligharimia maziko yake. Ni kigezo gani kimetumika kuamua hivyo na pia kwa uamuzi wa nani aliyeidhinisha matumizi hayo? Ni Bongo Stars wangapi wamefariki bila hata mchango wowote (toka Serikalini) na hata kama tungelinganisha michango yao katika jamii mfano akina Sembuli, Remmy, TX Moshi, Marijani n.k basi hata tungesikia kiwango kama hicho au hata angalau nusu yake. Utashangaa kusikia kuwa mimi babu yangu alifariki na alikuwa Mwenyekiti (mwadilifu) wa CCM (M) na Mjumbe kwenye Jumuiya ya CCM (T) lakini cha ajabu hata hatukuona hata salamu tu za maandishi za rambirambi toka kwa Mwenyekiti wa CCM (T) kwa wafiwa hata Mjane wa babu yetu hajawahi kutembelewa wala kupewa mkono wa pole hata siku moja! Vitendo kama hivi vinatafsirika kuwa ni matumizi zaidi ya hisia (feelings) kuliko taratibu na kanuni zinazotuongoza na huleta manungúniko ambayo hayataisha kwa wengine wengi (nimewataja wachache tu).

3. Inasikitisha Watu wengi (akiwamo Mchungaji Muongoza Mazishi, Mkuu wa Nchi na Waziri wa HVM) tunapotoa Wasifu wa Kanumba, eti “Kijana mwenye TABIA nzuri ya mwenendo wa maisha wa kuigwa katika Jamii” nayo ni sifa yake. Je, hii ni kweli? Kwa vile wakati pumzi ya mtu imekoma huwa hatusemi mabaya basi tungeishia hapo tu katika kumsifia Weledi wake katika kazi ya sanaa ya kuigiza na filamu. Kusema kuwa vijana wengine waige tabia ya mwenendo wa maisha yake ni kuvumbika changa ambayo itawaletea vijana wanaoiga wale mbovu!

Tuwe wakweli na tuwasaidie Wasanii wengi, Wasomi na pia Wanasiasa maarufu hasa katika kipengele cha mienendo ya maisha yao ili waendelee kuishi maisha marefu wakitoa michango yao mbalimbali ya vipawa walivyojaliwa na Mungu.

Nami Mungu anisamehe na muendelee kuniombea maana katika hili nami si mfano wa kuigwa kabisa!


mkuu habari!asante kwa mpangilio mzuri wa hoja yako ambayo kwa kweli inatoa nafasi ya wengine ku pingana kwa hoja na bila kuvunjiana heshima.asannte.
leo nimeona nisign in angalau na mimi nichangie baada ya kupitia "thread"nyingi na kwa kweli nyingine zilikuwa zinasikitisha sana!labda kwa kuanza naomba niseme mimi si mshabiki wa kanumba,si mshabiki wa ccm na si mshabiki wa chama kingine chochote!lakini naomba ieleweke kwa dhati kabisa nawaheshimu sana wasanii,mashabiki na na wote wengine wanao shiriki katika siasa,kwani wote hawa wanashiriki kuishape hii jamii yetu iwe kwa mazuri au mabaya.
mtoa mada naomba niweke wazi nimeungana nawe ktk kipengele cha tatu,lakini nyingine naomba nitofautiane na wewe.
hivi tunaposema jambo fulani ni nyeti na lingine si nyeti tunazingatia nini?mimi kwa mtazamo wangu,jambo nyeti ni lile rinalohusu usalama kitaifa,afya,amani na utulivu na haswahaswa linapohusu watu wengi kitaifa.list ni ndefu ,hivyo hata swala la kiuchumi pia linaweza kuwa swala nyeti kwa sababu tu linahusu watu wengi na pengine kuwa na athari ambazo zitakuwa zinaonekana moja kwa moja!kwa mfano tunajua serikali nyingi duniani zinamfumo wa ki intelijensia ambapo kuna watu hulazimika kufa kwa manufaa ya wengi kwa kupitia assassination ingawa kamwe haiewekwi wazi.
kwa misingi hii,kama jambo linahusu ushiriki au hisia za wengi basi tayari linakuwa nyeti,kwani mda wote serikali na viongozi kazi yao ni kuwahudumia wananchi,kiuchumi,kisiasa,kisaikolojia na mengineyo.hapa pia list ni ndefu lakini nimetaja kisaikolojia kwa maana moja.natumai wote tumeona ule umati wa watu.hivi wangejisikiaje kama wangesikia rais wao yuko likizo ya pasaka ila anawapa pole sana!?jamani mimi nilikuwa pamoja nanyi pale waungwana mliposema rais alitakiwa awepo katika ule mgomo wa madrs nchini,kwanza kwa sababu ya unyeti unaotakana na ukweli kwamba tulikuwa tunadili na maisha ya watu,lakini pili,ni kuhusika kwa watu wengi kihisia ambapo kwa kweli ilihitaji kuondolewa wasiwasi na viongozi wa kitaifa.
jamani lazima tukubali kwamba binadamu tuko wengi na tuko sawa lakini tunatofautiana.mimi nikifa leo pengine unaweza hata usijue hata kama utakutana na maiti yangu ikipelekwa makaburini, na pengine nikazikwa na watu watano.lakini hiyo haitamaanisha wewe ni katili.ndivyo hivyo kuna wale ambao ni public figures na kwa hivyo inakuwa si wanne tena bali laki nne,msiba wa mtu unaemfahamu na usiyemfahamu ni tofauti sana.huu ni ukweli wa maisha.
turudi kwa kanumba!je ni kweli huyu kijana hakuwa na umuhimu!?lahasha,mimi nadhani alikuwa na umuhimu mkubwa tena sana.kama ambavyo mzee kipara,pwagu,hamisigagarino,kizota,mtoto wa dandu to mention afew!lakini tukubaliane kwamba walikuwa under utilised,robbed and unrecognised!tukiondoa ukweli hawa walikuwa ni waburudishaji lakini pia wanamchango mkubwa ktk kuishape jamii yetu.kutokana na hali ngumu ya kimaisha ya sasa unaweza ukajikuta starehe ni kama dhambi kuitamka,lakini ukweli ni kwamba,sport,burudani na vinginevyo ni vitu vya muhimu sana ktk maisha ya binadamu.unapokosa hivi ni rahisi sana kuingia ktk deviation na kufanya vitu vingine ambavyo vinaweza kukuathiri kiafya,kiuchumi na hata kiakili wakati mwingine.
lakini lingine,mtu kama kanumba angeweza kuingiza pato kubwa serikalini kama angekuwa properly utilised na kuwa chanzo cha mapato kama ilivyo secta za madini,kilimo na nyinginezo.marekani,uingereza nanchi nyingine zilizoendelea wasanii wanalipia kodi kubwa sana ambazo zinarudi kutoa huduma za kijamii.kwa maana hiyo kama ambavyo kuna unyeti wa kufuatilia mikataba ya madini,ndivyo ambavyo kanumba anakuwa na unyeti kwa mantiki ya chanzo ya kipato serikalini.
nafahamu,kuwa alikuwa analipa kodi,lakini si kwa kiwango ambacho angetakiwa kwa mantiki hiyohiyo ya kutokuwa na mapato kinachofanana na thamani yake.wenzetu huwa wanatengeneza hata mastaa ilimradi tu wapate mtu ambaye ataingiza kipato kama kodi serikalini.mimi naomba niseme kama ambavyo juhudi zinatakiwa kuongezwa kuhakikisha sekt kama ya madini inaongeza changio la kodi,ndivyo hivyo secta za michezo,burudani,na nyinginezo zinatakiwa kufanya.lakini pia hata watu ikiwemo mimi na wewe ndio tutaona unyeti wa watu kama hawa.na lingine sote tumeona umati ule.
kufanya kosa kwa sababu ulifanya kosa hutatui kosa lakini unaongeza ukubwa wa kosa.kwanza tuanze kukubali tulikosea na ndio maana watu kama Marijani,Kipara,remmy,na wengineo wengi wamekufa maskini na manung'uniko makubwa zidi ya nchi yao.kipara na wengine walipaswa kuwa recognised wakiwa hai na hata walipokufa.lakini,kwa sababu hatukufanya hivyo haitupi uharali wa kuendelea kufanya hivyo.tuchukulie mfano maskini mzee kipara<rip>alilazimika kuomba msaada alipokuwa anaumwa na alipokufa hakupata publicity kubwa ingawa nae alikuwa ni star.kwa mtazamo wangu mimi nazani viongozi wasingeweza kwenda kwa aibu ya kuulizwa ni kwa nini amekufa maskini vile maana haki za wasanii ni kama wimbo wa kitaifa!kwa kanumba wamesema mnaona mwenzenu kajituma na wengine wajitume,kwa maneno mengine ni kulegitimise na kuwatupia lawama wasanii wenyewe kwa kupitia juhudi za kanumba!mimi naomba viongozi kama ambavyo nimesikia waziri husika amesema,wafanyie kazi ili kubadilisha maisha ya wasanii wetu na kuongeza pato kwa taifa.mkuu wangu mtoa mada;heshima kubwa kwako,kipengele cha 3 nimekubaliana nacho mstari kwa mstari.naomba mnisamehe kwa grammatical errors,ni maswala ya typing,nikiwaambia nimechukua mda gani kuandika haya mtacheka na kunionea huruma maana hata sijamaliza!hahaha!wacha nikusanye nguvu nitarudi baadaye
 
rip the great kanumba!!!!!mengi yatasemwa,lakini msiba huu umetuonyesha tuna viongozi wa ajabu sana kupata kutokea nchi hii!!!amin usiamin mambo kama haya yanatokea kwenye nchi zetu hizi za ajabu ajabu,cdhani jambo kama hili linaeweza kutokea hata ghana baada ya kuidemoktisha nchi yao!!labda la msingi hapa pamoja na hila zote kwenye katiba mpya,watanzania tuhamasishane kila mwananchi apate fursa ya kunena,pengine tutakuwa na katiba bora ambayo itaweza kukuwawajibisha watu kama hawa wakina nchimbi na naibu!!!inakuaje mmoja wapo asiwepo bungeni kuratibu shughuli za wizara yake zitazohitaj maelezo kutoka bungeni?tanzania yetu hii ni kioja!!!tunadhani kila event ni sehemu muhafaka wa kujenga taswira ya chama!!!!!nasema hapana hapana,big no!!!hata watanzania wote museme yes!!!mi nasema hapana,big no!!
Hapa wengi hatutaki kukubali kuwa tulipitiliza katika maomboleza, eti kushindanisha misiba (Nyerere vs Kanumba)!

Mwishoni ndio tunaanza kujua ukweli kuwa waliokuwa msitari wa mbele kuhamasisha kumbe walikuwa si kwa sababu ya uchungu bali sasa tunasukia kuwa pesa za michango ya rambirambi zimeliwa. Tz hatuko sawa, tukubalini hili

 
Back
Top Bottom