Ya Kandoro inatisha... Ajiuzia gari la TZS milioni 300 kwa milioni 2 tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Kandoro inatisha... Ajiuzia gari la TZS milioni 300 kwa milioni 2 tu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Sep 12, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,149
  Likes Received: 2,109
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mteule wa JK mh. ABASI KANDORO, amefanya kufuru ya mwaka kwa kujiuzia gari la kifalme lililogarimu wavuja jasho zaidi ya milion 300/= ambalo wanaharakati tumekuwa tukiyapigia kelele kwa pesa za kitanzania Tsh. 2,000,000 tu.

  Gari hilo ni VX TOYOTA LANDCRUISER, LENYE SPEED MITA 240, namba za usajili STK 3643 lililonunuliwa na mtangulizi wake kwa matummizi ya OFISI YA MKUU WA MKOA wa Mwanza.

  Gari hilo lililonuliwa na mkuu wa mkoa kabla ya Kandoro bado ni mpya na hali yake ni nzuri sana, wala halijamaliza hata miaka 10 likitumika.

  Baada ya kandoro kufika mwanza, alilikataa kulitumia na kusema kuwa halifai kuwa la mkuu wa mkoa na hivyo alitenga fedha la kununua gari lingine la kifahari zaidi LANDCRUISER V8, BEI MILLION 400/= speed mita 260 ambalo ndilo analolitumia mpaka sasa.

  Baada ya kununua gari hilo la kifalme, gari la awali lilipewa namba za serikali STK 3643 na kupaki kwenye ofisi za mkoa na mara chache sana kutumika mkoani.

  Ndipo Mh. Abasi kandoro akaunda mbinu za kujiuzia gari hilo alilolikataa kwa madai kwamba halifai kuwa la mkuu wa mkoa, akijiuzia kwa Tsh. 2,000,000/= milion mbili pesa za kitanzania.

  Kwa sasa yuko kwemnye hatua za mwisho za kupata kibali, ili aondoe hiyo STK, na kubandika namba za kiraia anze kula maisha na gari hilo la kifahari lililogarimu pesa za walipa kodi karibu au zaid ya 300,000,000/= na kuuzwa kwa bei ya kifisadi 2,000,000 tu.

  Nawasilisha tafadhali.

   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kuna siku watakuja kulipa ipo siku tuu,wasidhani CCM itakaa madarakani milele
   
 3. lukatony

  lukatony JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  kandoro ashitakiwe!!!!!!!!!
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Anyang'anywe na ashitakiwe!
   
 5. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama haya uliyoyaandika yana ukweli asante kwa taalifa. Tutampelekea Dk Slaa aongeze idadi ya mafisadi kwenye orodha yake.
   
 6. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  nasikia maumivu kichwani watanzania tuamke
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Atokee Rawlings wa Tz awatwange risasi hawa wote kule Coco Beach! Bila hivyo nchi hii haitanyooka.
   
 8. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kandoro si wa kwanza kufanya hivyo huo ni utaratibu wa kawaida tu kwa viongozi wengi hasa wa serikali kuu na Taasisi mbalimbali kujiuuzia magari ya thamani kubwa kwa bei sawa na bure.

  Tena hizo milioni 2 za kandoro ni nyingi sana kuna watu wananunua GX kwa laki tisa (900,000/=) tu, yaani ufisadi ni mkubwa sana serikali kuu na kwenye taasisi za serikali ila chakushangaza watu wanapiga kelele kuwa halmashauri zinaongoza wakati sio kweli, asilimia kubwa ya wizi kwenye halmashauri ni chini ya milioni 10 tu.
   
 9. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inachosha!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu, unajua mimi mpaka kesho huwa sielewi Toyota kuuzwa milioni sijui 300 au 400, Toyota haimo kabisa kwenye hiyo ligi. can someone pls explain to me??????
   
 11. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ee Mungu usikiae sale zetu uturehemu!
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  unashangaa ya mwanza?ccm kila kona mtindo ndio huo ila sasa inakula kwao muda si mrefu,
  tusuburi waislam wawanzishie ili na sisi tuzibuke masikio.
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  aliacha 'maumivu' Dar es Salaam ya kufidia kuhamisha wakazi wa Tabata dampo ambapo inasemekana ililipwa Billion 20 (20b) kwenye kiwanja ambacho hata milioni 500' hakifikii. Yaani hakulidhika tu!? ...kweli ukila nyama ya binadamu huwezi acha!
   
 14. G

  Greard Member

  #14
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kandoro atalichukuwa na atakaa nalo na hatafanywa lolote. Nani wakumfunga paka kengere? Nchi nzima viongozi wameoza
   
 15. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Watanzania tupunguze majungu tufanye kazi. Kila taasisi ina kitu kinaitwa "Disposal Policy" kwamba gari likifikisha Kilometer/miaka flani linauzwa linanunuliwa lingine. Wengi hutumia Kilometer 250,000 au miaka mitano. Hata kama gari lilinunuliwa kwa 300 million baada ya kutumika miaka mitano thamani yake haitabaki kuwa 300 milion tena kutokana na uchakavu ambao utakuwa umekadiriwa kuwa 60 million kwa mwaka kama Policy yao ni miaka mitano.

  Ila kwa swala la kuuzwa 2 million, kama ndio bei iliyopatikana kwa ushindani "Tender process" bado mtu hawezi kuhoji. Ila kabla ya kutangaza tender ilitakiwa gari hili lifanyie "valuation" kujua market value na hivyo lisingeweza kuuzwa chini ya "market value
   
 16. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiyo ni bei maalum kwa serikali ya Tanzania, hujui kuwa watanzania ni mamilionea hivyo hata bei zetu huwa ni special teh teh teh teh!

  Hiyo ndio bongo mkuu!
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hata mimi huwa nashangaa pengine ni ufisadi tu kati ya watumishi wa serikali na Toyota Tanzania
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nadhani itakuwa hivyo maana hizo ni bei za magari ya kiitaliano!!!!!!!!!
   
 19. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hizi sayansi zenu za uhasibu ndio zinatufanya mtuibie pesa zetu........eti gari zima bado linatembea na linang'aa mnatuaniambia lina zero value kisa sijui wenyewe mnaita "depreciation", cha kushangaza mtu akishalinunua hilo gari utakuta anakaa nalo hadi miaka 15 au zaidi, sasa hiyo depreciation ni kwa serikali tu, kwa watu binafsi hai-apply?

  Nyie wasomi ndio mnatuharibia nchi. Mwizi ni mwizi tu, hata ukiiba kwa kalamu wewe ni mwizi tu!
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nazidi kuamini ccm hakuna msafi hata kidogo na chakushangaza wanaendelea wakidhani bado watz wa mwaka jana ni sawa na waleo iko siku kwani mwosha huoshwa
   
Loading...