Ya kale ni dhahabu: SAY - Mtoto wa Mwarabu mhamiaji aliyeitikisa Nchi kwa Muziki

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,103
37,633
Mtoto wa Mwarabu mhamiaji aliyeitikisa Nchi kwa muziki

MOJA kati ya matukio ambayo wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla hawatoyasahau ni kuondokewa na mwanamuziki bora sana kitaifa, Salum Abdallah

Yazid, maarufu ‘SAY’, hata ikaacha majonzi makubwa kwa mashabiki wa dansi Afrika Mashariki.

Ilikuwa Novemba 18, mwaka 1965, mwanamuziki huyo alipopoteza uhai tayari alishautwaa umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ni kifo cha ajali ya lori la mchanga alikokuwa akiliendesha, pale alipochomoka kutoka kwenye usukani ukawa mwisho wake, wapenda muziki wakiachwa katika majonzi mawazoni wana

nyimbo zilizompa umaarufu mkubwa.

Hapo kuna vibao kama vile Ngoma Iko Huku; Shemeji Shemeji; Mkono wa Iddi; Wanawake Tanzania; Sipati Majibu; 'Naumia; Cuba Chacha; na Ewe Mola Wangu, ambao wachambuzi wengi wa muziki, wanakitafsiri katika sura ya utabiri wa kifo chake.

Alikuwa ‘mboga saba’ Historia inaonyesha wanamuziki wengi wanatoka kwenye familia za kimaskini, lakini haikuw kwa Salum Abdallah. Yeye alitoka kwenye familia ya kitajiri. Baba yake, Mzee Abdallah Yazid, ana asili ya jamii ya Kiarabu kutoka nchini Yemen, aliyejikita mjini Morogoro, alikofunga ndoa na mwanamama wa Kitanzania.

Mzee huyo, alikuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio kwa kumiliki migahawa kadhaa, maduka, Salum, aliyezaliwa Mei 5, mwaka 1928, alilelewa kwenye mazingira hayo ya vijana wa mjini kwa sasa wanayaita 'mboga saba', lakini kichwani alishatekwa na wito wa muziki ulioshika nafasi zote.

Tangu katika umri mdogo, Salum alipenda kwenda kwenye nyumba jirani zilizokuwa na mashine za santuri, maarufu 'rekodi pleya'. Wakati huo nyimbo zilizovuma ni kutoka nchini Cuba, katika mitindo ya charanga, salsa, borelo zikiwa katika santuri zilizoitwa ‘GV.’

Baba yake alimuweka Salum kwenye moja ya maduka yake, lakini mara nyingi alitoroka kwenda kusikiliza nyimbo hizo, kitu kilichomkasirisha sana mzazi, hata akamcharaza bakora kila mara. Mtoto hakukoma kiasi kwamba baba akaamua kubadilisha mbinu, aliamua kumnunulia 'pleya' ili kijana wake atulie dukani.

Hiyo kisaikolojia ikawa dawa, kwani Salum alitulia dukani na kufanya biashara vizuri, kiasi hata baba yake alifurahi na kuzidi kumpenda. Baba alikerewa na uhalisia, akioona kijana wake kawehuka na muziki wa dansi, kwani itikadi yake kiimani haikukubaliana nayo hata kidogo.

Zengwe la rafikize baba Hata hivyo, kitendo hicho kiliwakera baadhi ya marafiki wa Mzee Abdallah, waliomwambia mtu mwenye heshima zake kwa sifa za tajiri, muungwana na mwenye itikadi safi kiimani, haiwezekani mtoto wake apige muziki.

Ikumbukwe kuwa wakati huo muziki ulichukuliwa kama kazi ya watoto, umaskini na uhuni, huku Mzee Abdallah alikuwa Mwenyekiti wa Wazee wa Kiarabu Morogoro, hivyo ilionekana Mtoto Salum anadhalilisha, pia kuidhalilisha itikadi yao.

Baba yake aliungana nao, kwa sababu aliyakubali yaliyosemwa na rafiki zake, lakini katika sura ya pili alimpenda kijana wake na hakutaka kumkera, kwa sababu alionekana kuwa na akili ya kusimamia mali zao.

Hali hiyo ilisababisha kutoroka kwenda nchini Cuba, lakini meli iliishia Mombasa Kenya na pesa zilipomuishia alianza biashara ya kuuza mishikaki, hali aliporudishwa Morogoro na chama cha wafanyabiashara wa Kiarabu ambao tayari walishafahamu kuwa ni mtoto wa mwenzao mzee Yazid.

Kifo Chake Ilikuwa Novemba 18, mwaka 1965, mwanamuziki huyo alipopoteza uhai alipokuwa amelazwa hospitalini, baada ya lori la mchanga alilokuwa akiendesha kupata ajali, ikiwa ni siku ambayo bendi yake ilitarajia kutumbuiza kwenye sherehe za kitaifa, ugeni mkubwa ulikuwa unasubiriwa katika mji huo.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mheshimiwa Rashid Mfaume Kawawa, viongozi wakuu wa nchi wakati huo, walikuwa wakisubiriwa na wananchi wa hapa katika sherehe ya kufungua Chuo cha Kilimo ambacho kwa sasa kinajulikana kama SUA (Sokoine University of Agriculture).

Pamoja na wageni hao pia alitegemewa kuwapo aliyekuwa Mbunge wa Morogoro mjini wakati huo Mheshimiwa Oscar Kambona. Watu wakakesha na marehemu. Kesho yake hali ilizidi kuwa ngumu wakati wa kusindikiza maiti kwenda makaburini ilikuwa kama kila mtu alikuwa akitaka japo abebe kidogo jeneza, hadi ikalazimu FFU wawepo kuleta amani.

Jeneza la Salum liliweza kubebwa kutoka Nunge nyumbani kwa mama yake hadi Msamvu kwenye eneo alipozikwa, watu wakiwa wamejipanga mstari mrefu, hakukutumiwa gari.



Kwa hisani ya NIPASHE
 

Attachments

  • muzikli.jpg
    muzikli.jpg
    32.3 KB · Views: 3
Cuban marimba band ilikuwa tishio enzi zake .kuna mtu anaitwa waziri nyange aliiga sauti yake baada ya mauti kumkuta ila wapi
 
Ikiwa "rekodi pleya" na santuri hauzifaham hauwezi kuelewa huu uzi.
Umenikumbusha siku moja tumeenda Nairobi na rafiki yangu mmoja kupiga muziki.

Yeye anapenda sana kutumia vynils (LPs). Basi akawa kabeba vinyls zake kibao.

Basi tumefika ile club, tunafanya sound check. Akawauliza record player yenu iko wapi? Wakamwambia hapa ni mwendo wa CD tu.

Akahamanika sana, kwa sababu alibeba vynil records tu.

Basi kama machale vile nilikuwa nimebeba CDs kama 100 hivi. Nikamwambia nimekuja na CDs zipo maskani tulipofikia. Nikaenda kuchukua CD, tukaendeleza burudani.

Siku hizi unaweza kukutana na DJ hata CD hatumii. Anapiga muziki wa computer tu.

Kuna siku mdogo wangu alikuja kunitembelea akakuta kikasha kina CDs kwenye gari, akanicheka sana, akisema bado unatumia CD?

Hawa ma DJ wa siku hizi habari ya record player wengi wanazisoma tu kama historia.
 
Umenikumbusha siku moja tumeenda Nairobi na rafiki yangu mmoja kupiga muziki.

Yeye anapenda sana kutumia vynils (LPs). Basi akawa kabeba vinyls zake kibao.

Basi tumefika ile club, tunafanya sound check. Akawauliza record player yenu iko wapi? Wakamwambia hapa ni mwendo wa CD tu.

Akahamanika sana, kwa sababu alibeba vynil records tu.

Basi kama machale vile nilikuwa nimebeba CDs kama 100 hivi. Nikamwambia nimekuja na CDs zipo maskani tulipofikia. Nikaenda kuchukua CD, tukaendeleza burudani.

Siku hizi unaweza kukutana na DJ hata CD hatumii. Anapiga muziki wa computer tu.

Kuna siku mdogo wangu alikuja kunitembelea akakuta kikasha kina CDs kwenye gari, akanicheka sana, akisema bado unatumia CD?

Hawa ma DJ wa siku hizi habari ya record player wengi wanazisoma tu kama historia.


Kumbe mwamba mambo ya strategy umeyaanza kitambo sana? Hapo mngeumbuka usingejiongeza
 
Kumbe mwamba mambo ya strategy umeyaanza kitambo sana? Hapo mngeumbuka usingejiongeza
Yani kitambo sana. Kuna stories nyingi za aina hiyo lakini naona si pahala pake hapa.

Kuna vitu fulani ukiweza kuwa na mentality ya kuwa na backup, hata vikiharibika, unaweza kuwa na jinsi ya kuokoa jahazi.
 
Back
Top Bottom