Ya JK, CCM na serikali yake ni dalili za kufa kwa mhimili wa dola (executive) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya JK, CCM na serikali yake ni dalili za kufa kwa mhimili wa dola (executive)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, May 2, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  [h=2][/h]KATIKA HALI YA KUSHANGAZA KABISA BAADA YA BUNGE KUWATAKA MAWAZIRI 8 WALIOTAJWA KATIKA RIPOTI YA CAG KUJIUZULU WENYEWE AU LICHUKUE HATUA DHIDI YA WAZIRI MKUU JK, CCM NA SERIKALI YAKE SASA WANAGEUZA SUALA HILO KUWA NI LA MZAHA KWA KUPIGA POROJO NYINGI ZISIZO NA MASHIKO ZIKIWA NA LENGO YA KUJISAFISHA.

  MATHAHALANI KATIKA HOTUBA YA JK YA MEI MOSI ALIYOTOA MKOANI TANGA (AMBAYO IMENUKULIWA HAPA CHINI) JK ANADAI KUWA NI YEYE ALIYEAGIZA RIPOTI ZA CAG ZIPELEKWE KUJADILIWA BUNGENI BAADA YA KUONA KUWA WAPO WATENDAJI WA SERIKALI WANAOGEUA "MCHWA WA MALI YA UMMA".

  KATIKA HARAKATI ZA KUJISAFISHA NA KUFICHA UDHAIFU WAKE JK NA CCM WANASHAU KUWA MHIMILI WA DOLA NDIO WENYE JUKUMU LA KUWASHUGHULIKIA IPASAVYO WEZI WOTE WA MALI YA UMMA PASIPO KUSUBIRI RIPOTI ZA CAG WALA SHINIKIZO TOKA BUNGENI.

  KITENDO CHA JK KUSHINDWA KUELEZA NI HATUA ZIPI AMEKUWA AKICHUKUA KAMA KIONGOZI WA SERIKALI DHIDI YA "MCHWA WA MALI YA UMMA ALIOWATAJA KUWA WAMEKUWA WAKITAFUNA FEDHA ZA UMMA KWA MUDA MREFU" HUKU AKIFAHAMU NI UDHAIFU NA MAPUNGUFU MAKUBWA VYENYE KUONYESHA DHAHIRI KUWA YEYE KAMA KIONGOZI WA DOLA YA TANZANIA NI DHAIFU NA ASIYE NA UWEZO WA KUWASHUGHULIKIA WEZI WA MALI ZA UMMA HADI KUSAKA MSAADA TOKA MHIMILI WA BUNGE. NA HILI LINAWEZA KUTHIBITISHWA NA KITENDO CHAKE KUWAKINGIA KIFUA WEZI WA EPA WASICHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA HADI LEO NA KUWATAKA KUREJESHA FEDHA WALIZOIBA NJE YA UTARATIBU WA KISHERIA.

  KITUKO NA AIBU KUBWA NI PALE KIJANA TULIYEKUWA TUKIMTEGEMEA NAPE NNAUYE NAYE ANAPOJIUNGA NA POROJO HIZI BADALA YA KUTUELEZA TOKA AMEKUWA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM AMETUMIA VIPI NAFASI HIYO KUDHIBITI WIZI WA MALI YA UMMA BADALA YA WAJUMBE KAMATI KUU YA CCM KUGEUKA MASHABIKI WA HATUA ZA MHIMILI WA BUNGE.

  TOFAUTI NA MADAI JK NA CCM YAKE UIMARISWAJI WA OFISI YA CAG NI MOJA YA MASHARTI YALIYOWEKWA NA WAFADHALI ILI TANZANIA IWEZE KUENDELEA KUPOKEA MISAADA TOKA NJE BAADA YA WAFADHILI KUONA KUWA SERIKALI YA TANZANIA KWA MUDA MREFU IMEKUWA HAICHUKII HATUA ZOZOTE DHIDI YA WEZI WA MALI ZA UMMA KUTOKANA NA KUWA VIONGOZI DHAIFU KAMA JK


  [h=2][​IMG] Kikwete agonga msumari wa mwisho kwa mawaziri............hii inaashiria nini hasa?[/h]
  ASEMA ALIFURAHIA MJADALA MKALI BUNGENI, AJIPANGA KUTEKEKELEZA MAPENDEKEZO................WAKATI akitarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya Baraza la Mawaziri muda wowote kuanza sasa, Rais Jakaya Kikwete amesema amefurahishwa na mjadala mkali ulioibuka bungeni kuhusu kuwajibishwa kwa wasaidizi wake wakuu serikalini.Kwa muda wa wiki mbili sasa, kumekuwa na mjadala mkali juu ya matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Ripoti tatu za Kamati za Bunge za mwaka 2009/10, ambazo zimependekeza kuwajibishwa kwa baadhi ya watendaji serikalini wakiwamo mawaziri wanane.

  Akihutubia katika sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Rais Kikwete alisema ndiye aliyeagiza Ripoti ya CAG iwe inajadiliwa kwa uwazi bungeni kila mwaka, hivyo yote yaliyoanishwa na kuthibitika wahusika watajibishwa.

  “Kuna mambo matatu nataka kuyazungumza kabla ya kumaliza hotuba yangu... Bungeni kulikuwa na mjadala mkali kweli kuhusu Ripoti ya CAG na Ripoti nyingine tatu za Kamati za Bunge. Mimi nilikuwa Marekani, lakini niliporudi yakazungumzwa mambo mengi kweli,” alisema na kuongeza:

  “Mara Kikwete ampinga Pinda, mara nimepanda ndege kwenda Dodoma. Mengine yamesemwa ya kweli, mengine yameongezewa na mengine ni ya uongo kabisa. Lakini, mjadala ulikuwa ni mkali kweli bungeni. Wengi wakitaka mawaziri waliotajwa kwenye ripoti hiyo wawajibishwe, ninachowaahidi ni kwamba tumejipanga vizuri kutekeleza mapendekezo ya wabunge na Kamati za Bunge.”

  “Sikukasirishwa na wala kufedheheka na mjadala ule, nilifurahia ripoti kujadiliwa kwa uwazi. Tatizo watu wanasahau mapema. Mimi ndiye niliyeamua ripoti hii ya CAG ijadiliwe kwa uwazi bungeni tangu mwaka 2007. Nilifikia uamuzi huo baada ya kuona wapo baadhi ya watu ambao ni mchwa wanaokula fedha za umma.”

  “Kwa hiyo mjadala ule ulipokuwa unaendelea bungeni nikaona sasa tunaelekea kufanikiwa katika kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali.”

  Alisema kabla ya utaratibu huo aliouasisi, ripoti ya CAG ilikuwa haisikiki wala haijadiliwi kwa uwazi na kina jambo ambalo liliwafanya baadhi ya watendaji kuendeleza wizi wa fedha za Serikali kwani ripoti hiyo ilikuwa ikiwasilishwa tu bungeni kama ‘Order paper’.

  “Hata ripoti hiyo ilipowataja baadhi ya watendaji wa Serikali kuhusika katika matumizi mabaya ya fedha za Serikali, hawakujali waliendelea na matumizi hayohayo,” alisema.

  Rais Kikwete alisema ulishajengeka utamaduni kwamba ripoti ya CAG ilipokuwa inatolewa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wezi wa fedha za umma.

  Alimsifu CAG, Ludovick Utouh akisema amekuwa akifanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuongeza: “Huyu sasa yuko huru. Katiba inasema wazi huyu akishateuliwa huwezi kumuondoa na wala huwezi kusema kuna chombo cha kumdhibiti. Kama kuna kitu umeona hakijakufurahisha unapaswa kwenda Mahakama Kuu kupinga siyo kusema tumdhibiti, hamuwezi.”

  “Mfano, hata akinitaja mimi siwezi kusema nimdhibiti nitabaki na kinyongo cha roho. Ninachotaka sasa ni nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, niliwahi kuwaita mawaziri nikamwambia awaambie matatizo yao kila mmoja, nikawaita makatibu wakuu nikamwambia nao awaambie na Aprili 28, wenyeviti wa halmashauri nikamwambia awaambie.”

  “Niliiboresha taasisi hiyo ili iweze kufanya kazi vizuri na uwazi mnaouona hivi sasa wa wabunge kuijadili ripoti ya CAG ni mambo ambayo niliyaanzisha mwenyewe,” alisema Rais Kikwete.

  IKULU YAFAFANUA........
  Awali Ikulu, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema mchakato wa mabadiliko ya mawaziri unaotarajiwa kufanywa ni wa kawaida na utafanyika kwa umakini ili kutenda haki kwa watuhumiwa.

  Ikulu imetoa ufafanuzi huo siku moja baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuanza kuwachunguza watendaji wote waliohusika, wakiwamo mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma zilizoanikwa kwenye ripoti ya CAG.
  Tayari Kamati Kuu (CC) ya CCM imebariki uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kulisuka upya baraza kama hatua mojawapo katika kutekeleza maazimio ya Bunge kutaka mawaziri na watendaji waliotajwa katika ripoti ya CAG, wawajibishwe.

  Mawaziri waliotajwa katika ripoti hiyo ya CAG ni William Ngeleja (Nishati na Madini) Omari Nundu (Uchukuzi), Mustafa Mkulo (Fedha), George Mkuchika (Tamisemi), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Dk Cyril Chami (Waziri wa Viwanda na Biashara).

  Balozi Sefue alisema licha ya kukabiliwa na tuhuma, lazima maziri husika wachunguzwe ili kujiridhisha kama ni kweli wanahusika.

  “Ripoti imetolewa lakini lazima yapimwe ili kama unafanywa uamuzi uwe ni sahihi na kutenda haki,” alisema Balozi Sefue​
   
 2. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  nawapa pongezi nyingi sana wapinzani (not sure of CCM B) kwa kuwezesha mchakato huu kufika hapa ulipo. bila ya wao, tungebaki pale pale ktk usemi wa LIFE GOES ON. mkuu wa kaya kwa mara nyingine tena amedandia treni kwa mbele. last time nakumbuka ilikuwa ni issue ya katiba. baada ya kuona mambo yamekuwa moto, na waziri wake pamoja na mwnasheria mkuu kuanza kuropoka na kujifanya wao ndo wasemaji wakuu, na kupotosha uma kwa kauli zao kinzani, mkulu mkulu akaamua kudandia treni kwa mbele.
  sipati picha ingekuwaje kama upinzani ungekuwa uko weak! rpoti ya CAG haijawahi kuwa clean toka achukue madaraka. hatua gani ilichukuliwa?

  wabunge wa Chichiem walikuja kuwa mbogo bungeni baada ya kuona majimbo yao yamo hatarini kuchukuliwa. sasa hivi funga mdomo mjengoni uone wenye jimbo watakavyokupa kitu kinachouma. lakini ndo inavyotakiwa mjengoni- solidarity - siyo siasa za chooni ambazo Inzi pekee ndo atafaidi.
  nawasilisha
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Kombani na Mwana sheria Mkuu wa Serikali hawakukosea walipopinga hoja ya mabadiliko ya Katiba kwa kuwa suala hilo halikuwamo katika ilani ya uchaguzi wa CCM ya 2010. Aliyekenguka na kuanza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA akiwa ndani ya CCM ni JK. Hata sasa amethibitisha alivyodhaifu kwa kuacha kutumia vyomba vya Dola kama vile TAKUKURU, Polisi n,k kudhibiti wizi wa mali ya umma toka mwaka alipoingia madarakani hadi 2007 alinapodai kuwa hatua pekee aliyochukua ni kutaka haoja ya wizi wa mali za umma ijadiliwe bungeni.

  Hii inatuthibitishia kuwa tunaye Rais asiyefahamu nini anatakiwa kufanya na hatua zipi anapaswa kuchukua katika mazingira fulani. Haishangazi ndio maana aliwasemehe wezi wa EPA badala ya kutumia fedha wazlizorejesha kama vithibiti kuthibitisha tuhuma dhidi yao.
   
Loading...