Ya Haille Selasie na msafara wa simba ulaya na ya JK na msafara wa ombaomba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Haille Selasie na msafara wa simba ulaya na ya JK na msafara wa ombaomba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAGL, Nov 28, 2010.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF katika historia ya Haile Selasie, aliwahi kufanya ziara ulaya na asia akiwa na watu wake mashuhuri (nobles) huku akiwa na kundi la simba(pride of lions). Mbali na simba hao pia alikuwa na vitu vya thamani alivyowaachia watawala wa huko akiwemo mfalme wa Ufaransa aliyepewa zawadi ya simba dume na jike. Wakati anasimikwa kuwa mfalme wa Ethiopia, viongozi wengi mashuhuri walihudhuria, walioshindwa kuhudhiria kama raisi wa Marekani aliomba radhi na kutuma muwakilishi. Pia katika sherehe hizo zawadi mbalimbali zilitolewa na mfalme Selasie ikiwemo biblia yenye gamba la dhahabu aliyopelekewa kiongozi mashuhuri wa dini wa huko Marekani. Kama nitakuwa sijasahau tuliambiwa kuwa misafara mingi ya JK Ulaya ndo imesaidia sisi watz tusilale njaa. Pia hilo likathibitishwa mhe Lowasa pale jimboni kwake wakati wa kampeni, kwamba tz inahitaji mtu ambae anaweza kuongea vizuri na waingereza ili watusaidie fedha za bajeti, na mtu huyo ni JK, hivyo mpeni kura zenu. Hii ilimaanisha kuwa misafara mingi ya mhe prezda ulaya, ni ya kwenda kuomba misaada. Nimejaribu kulinganisha viongozi hawa wawili na kujiuliza maswali yafuatayo. Ni nani kati ya Haile Selasie na JK yuko sahihi na ana mapenzi mema na nchi yake? Kati ya Ethiopia ya kipindi hicho na tz ya leo, ni nani mwenye simba wengi na madini mengi? Hivi watz na utajiri wote huu tumeshindwa kuwafanya wazungu watusujudu kama walivyomsujudu Selasie kipindi kile? NB: naomba uchangiaji wa mada uzingatie kinazungumzwa na sio mpangilio wa paragraphs, lazima tutambue wengine tunatumia simu za kimaskini, hatuna kompyuta, hivyo hatuwezi kupanga vizuri. Nawasilisha.
   
Loading...