Ya "Habari Leo" Nao!.. mwaka huu tuna kazi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya "Habari Leo" Nao!.. mwaka huu tuna kazi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 27, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Haya ni maoni ya Mhariri wa gazeti la Habari Leo. (msisitizo wa rangi nyeusi wangu na maoni ya kwenye mabano - MM)

  Tukarabati haraka miundombinu bila kuogopa gharama

  Imeandikwa na Mhariri;
  Tarehe: 26th January 2010


  UHARIBIFU wa miundombinu uliotokana na mvua kubwa zilizonyesha Tanzania Bara, si siri tena kuwa ni mkubwa na unaohitaji hatua za haraka ili kuirekebisha na shughuli za kawaida zirejee.

  Hilo linajidhihirisha hasa kutokana pia na Rais Jakaya Kikwete, kushtuka na kutaka kuchukuliwa kwa hatua za kutengeneza upya miundombinu hiyo, hasa reli na barabara, katika baadhi ya mikoa nchini.

  Kama alivyotahadharisha Rais, tukicheza, Watanzania tutashuhudia uchumi wetu ukiishiwa nguvu na kuanza kuhaha tena kutafuta misaada kwa wahisani na wafadhili, ambao wengi wao wamekuwa wakirudi nyuma katika misaada kutokana na sababu zao.

  Cha msingi ni kuelewa tu kuwa hatuna mjomba wa kutubebea misalaba yetu na hivyo hatuna budi kujizatiti kwa lengo la kurejesha miundombinu yetu ili kunusuru uchumi huu ambao tayari ulishaguswa na kudorora kwa uchumi wa dunia.
  (really?)

  Wataalamu wanasema uharibifu uliofanyika katika Reli ya Kati na hasa kati ya Stesheni za Gulwe na Kilosa, katika mikoa ya Dodoma na Morogoro, kutokana na mvua zilizonyesha Mpwapwa na Kilosa kati ya Desemba 24 mwaka jana na Januari 10 mwaka huu, ni mkubwa. (kweli walihitajika wataalamu kusema kilicho wazi?)

  Walimwambia Rais kuwa katika maeneo ya Kilosa, mvua hizo na mafuriko, yalingÂ’oa kabisa sehemu ya Reli ya Kati na kusimamisha huduma za reli hiyo kati ya Dar es Salaam na Dodoma. (hakuna aliyeona?)

  Pia madaraja tisa yalisombwa na maji na mengine matatu yako katika hatari ya kusombwa. Ukarabati huo ni kazi kubwa kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, kwamba unaweza kuchukua hadi miezi mitatu na gharama inakadiriwa kuwa Sh bilioni 13.2 na hasa ikizingatiwa kuwa uharibifu huo umefanyika katika mikoa 18 nchini.

  Sisi tunauelewa uzito wa kazi yenyewe, lakini pia umuhimu wa kurejeshwa kwa miundombinu hiyo ambayo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya uchumi wa nchi hii masikini ambayo inajikongoja kufikia maendeleo ya kweli.

  Huu ni mzigo wa Watanzania wote, hivyo tuitie moyo Serikali iweze kuzipata fedha hizo na kuanza kazi mara moja, ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao kwenda sokoni na pia wafuate huduma na bidhaa kutoka wanakozihitaji.
  (kama ni mzigo wa Watanzania wote kwanini tusiubebe?)

  Lakini pia wadau wanapaswa kujitokeza kushirikiana na serikali kwa namna moja au nyingine, kwa hali na mali, katika kurejesha miundombinu hii, tunazungumzia wafanyabiashara wakubwa na kampuni mbalimbali zenye uwezo wa kuchangia. (Habari Leo je?)

  Tunaamini kampuni zenye migodi mathalan, ni wasafirishaji wakuu wa zana na mazao yao kupitia barabara na reli, hivyo kuvurugika kwa miundombinu hii ni jambo ambalo linawasibu zaidi na watakuwa na uchungu na watajitolea kwa sababu kutoa si utajiri.

  My Take:

  Tuna tatizo kubwa kweli katika kutazama mambo. Yaani hawa jamaa kitu ambacho wameona ni kikubwa zaidi kuathirika ni miundo mbinu! Vipi kuhusu "watu"? Yaani kuvurugika kwa miundo mbinu kumewaathiri zaidi makampuni ya migodi kwa vile sasa hawawezi kusafirisha madini?

  Kilichoniacha hoi zaidi ambacho ni kufanana kule kule kwa fikra za Guardian na Habari Leo ni hilo la kichwa chao cha habari. Kwa vile ni dharura basi tusijali gharama? kama huu siyo kuitisha mlango wa ufisadi tuiteje. Hivi kuna mtu yeyote anayefikiria suala la kuangalia matumizi ya serikali na kubana matumizi au sasa hivi ndio imekuwa "spend spend spend"..!?
   
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  MMK;
  Pole, unachotakiwa kifahamu kuwa wao wapo kwa ajili ya kuendesha Propaganda na wala siyo kwa maslai ya wananchi. Wamejiandikia tu kwa lengo na nia ya kuonyesha alichosema anayewalipa mishahara ni safi wakati kwa JK dhamira yake ni kuhakikisha wawekezaji wake hawapati taabu tena kusafirisha bidhaa zao.
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  You should know Tanzanians by now...Tuvipofu kabisaaaaaaaaaa
   
 4. T

  TheUchungu Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukishakuwa muandishi muajiriwa, mtizamo wako hauwezi kuwa independent hata kidogo, kuna fikra au idea za mwajiri wako ambaye ni lazima ziwe mbele nae mwajiri anawadau amabao ndio wanaoathiri kazi zake.....

  Na pia tunapoona tatizo pia tusiishie kusema tu na kuandika katka lugha nzuri bali tuonyeshe pia njia katika kusaidia....ningependa kuona vitendo zaidi kutoka katika mashirika mbalimbali hapa nchini katika kuchangia waliopatwa na maafa....mimi katika nafasi yangu nimehimiza sana wenzangu katika uchangiaji wa maafa kupitia mtandao wa wana taaluma, najivunia kushawishi zaidi ya watu 200 kujiunga.....
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  msiniambie kuwa kuna watu wanasoma haya halafu wanasema kesho nitanunua tena gazeti hili! ansinkabo!!
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuwa mwangalifu usitunyime chakula cha watoto ikiwa magazeti yatadoda..hatuna mjomba ati!
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Jan 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kweli kuna tatizo katika muktadha mzima wa kukabiliana na majanga, wengi tunadhani kazi ya serikali ni kujenga mabarabara ma reli , wala sikazi ya serikali kuwaondoa watu toka katika makazi yenye matatizo lukuki, sasa mtazamom wa jumla ni kukarabati reli na barabara bila kujali gharama wala bila yakuwajengea nyumba hao wadau wanaoangamia, unaposikia kule Haiti jumuia ya Kimataifa inajitwika mzigo wakujenga makazi ya raia usio kua ni kujipendekeza, daima serikali makini watu huwa kipaumbele.
  lakini hakuna 10% ya maana katika kuwahudumia watu tofauti na ujenzi wa mabarabara na reli maana TUTATUMIA UWEZO WETU WOTE BILA KUJALI GHARAMA.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  The world of politics, especially Tanzania, hates independent thinkers. I wonder how Adam Lusekelo survives in such an environment! Lol
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  toleration? ...
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wachumia tumbo!
  Hivi ni kweli kuwa hiyo tahariri imehaririwa? inaonekana kama vile kijana wa kidato cha pili alikuwa ziarani na msafara wa rais, na kutakiwa kuandika insha ya yatokanayo.
  Shame on you HL
   
 11. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Ni gazeti la serikali
  • Mhariri ni mwajiriwa wa serikali
  • ...anatetea kitumbua chake kwa kuandika chochote kitachompendeza 'bosi' wake.
  • ...amefilisika kimawazo...hana uwezo wa kutafakari na kupambanua mambo vinginevyo anajifanya hamnazo!
   
Loading...