Ya G. Jonathan Nigeria na muongo mmoja wa uongozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya G. Jonathan Nigeria na muongo mmoja wa uongozi

Discussion in 'International Forum' started by Kingo, Jul 27, 2011.

 1. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Kutoka Deutche Welle Swahili. Rais wa Nigeria Jonathan atawasilisa rasimu ya marekebisho ya sheria kutaka muda wa uongozi wa urais na magavana nchini humo upunguzwe kutoka mihula miwili hadi mmoja huku muda wa huo muhula ukiongezwa kutoka miaka 4 ya sasa. Sababu: Kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa viongozi, kwani wanatumia muda mwingi kuhangaikia kuchaguliwa tena uchaguzi unaofuata na pia kupunguza gharama ya uchaguzi wa kila mara. My take: Mimi hii natamani hata hapa Tz sheria itungwe tuwe na muhula 1 kwa uongozi, kwa rais, mawaziri, hata na wabunge na wk wa mikoa. Hamna mwenye hatimiliki ya jimbo au uongozi. We do not want recycled inefficient leaders and autocratic
   
 2. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima kwako.
  Nillisikia hii jana kwenye NPR. Nilishtushwasana na pendekezo hilo maana nimelitafsiri kama vile Bwana Goodluck Jonathan anataka kuleta aina ya kukaa madarakani kwa muda mrefu amabayo itawaharibia wananchi nafasi ya kuchagua mtu mwingine kama wanaona yeye hafai ( au raisi aliye madarakani hafai) Je kama anavurunda anataka aendelee kuvurunda mpaka lini? Yaani yeye ni nani anataka kubadili katiba ya nchi ambayo imefanya kazi miaka yote hiyo? Hii kazi ya kutoa ushauri si iachiwe kwa Wanaigeria wenyewe badala ya rais kuamua?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Soma tena vizuri tamshi la Goodluck. Hilo ni pendekezo lake na kama raia namba moja nchini anayo haki ya kulitoa. Yeye amesema haya mambo ya mihula yanaingilia tija kwa sababu badala ya kushughulikia matatizo ya nchi unaanza kujiandaa kushughulikia uchaguzi ujao. Huu utaratibu umefanya kazi vizuri tu katika jimbo la Virginia, USA. Gavana anachaguliwa kwa kipindi kimoja tu cha miaka minne akimaliza uchaguzi unafanyika anaingia mwingine. Hii imempa gavana muda wa kumulika vision yake na kujaribu kuikamilisha katika hiyo miaka minne. Kwa kifupi it is a good idea. Unaweza kupewa kipindi cha kuongoza miaka 5 au sita ikimalizika anaingia mwingine.
   
 4. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Alisema mabadiliko kama yatakubaliwa yataanza baada ya muhula wake 2015.
   
 5. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni tofautoi akiingia kichwa mbuzi ambaye anajua afanye mema asifanye hachaguliwi sasasi ndo ataiiba kiroho mbaya? Awamu za pili na za mwisho kwa viongozi wengi waafrika zimekuwa mbaya saana, kwani kumekuwa na wizi wa ajabu na utawala mbaya saana usiofuata hata sheria.
   
Loading...