Ya Chanika ndiyo inayoweza kuvuruga amani si maandamano ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Chanika ndiyo inayoweza kuvuruga amani si maandamano ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PatriotMzalendo, Mar 26, 2011.

 1. P

  PatriotMzalendo Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata habari za uhakika kabisa leo kwamba watu wenye makazi ya muda mrefu,chini ya uongozi unaotambulika kitaifa toka ngazi ya chini,wenye mashamba ya mazao ya kudumu na ya msimu, wameondolewa hivi karibuni kwa kuharibiwa vibaya mazao yao, kuvunjiwa nyumba zao,kuporwa mali zao na nyumba nyingine kuchomwa moto huko Chanika Wilayani Ilala,Mkoani Dar es Salaam kwa madai kwamba wamevamia eneo la hifadhi!

  Kibaya sana ni kwamba watu hao wamevamiwa na kutendewa unyama huo bila taarifa yoyote iliyotangulia ya kuwataka watoke eneo hilo. Kinachoshangza ni kwamba ni lini serikali imefahamu kuwa eneo hilo ni la hifadhi wakati watu wameishi hapo kwa miaka mingi na vituo vya kura vimekuwepo eneo hilo uchaguzi baada ya uchaguzi uliojumuisha kuchaguliwa kwa watendaji wa vitongoji vya eneo hilo? ilipofahamu kwamba eneo hilo ni la hifadhi (kama ni kweli) kwa nini serikali haikuwajulisha watu hao na kuwapa muda wa kuvuna angalau mazao yao ya msimu na waondoke kwa kuvunja vizuri nyumba zao ili vifaa vingine wavitumie kwa kujenga nyumba za kuwastiri baada ya tukio hilo?

  Kama Mrema na Cheyo pamoja na wengine wenye akili kama zao wangekuwa wanatoa matamshi ya kulaani vitendo vya uvunjifu wa amani kwa uhuru toka kwenye akili zao zinazojitegemea,wangetoa kauli za kutahadharisha kuvunjwa kwa amani kufuatia matukio kama hayo ya kimaonezi na ya kuhatarisha hasa amani badala ya kulaani watu wanaotoa kauli za kuitaka serikali iweke mambo sawa kwa manufaa ya wananchi ambao kina Mrema na Cheyo wanadai kuwatetea na kuwaita watetezi wa kweli wa wananchi hao eti wanavuruga amani.

  Watu hawa-Mrema na Cheyo- wanaililia serikali ya CCM inapoonyeshwa njia sahihi kwa kuingiziwa nini na nani vichwani mwao ili nasi tutumie mbinu hiyo hiyo ya kuingiza kitu hicho vichwani mwao ili itokee waite waandishi wa habari na kuwaambia wananchi kupitia kwao kwamba serikali ya CCM inahatarisha amani kwa kufanya maonezi kama hayo ya Chanika?

  It goes without saying that mambo ya Chanika ndiyo yanayoweza kuvuruga amani na si kauli ya CHADEMA kwamba mfumuko wa bei uko juu mno. Naomba kuwasilisha.
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kama hao wamevunjiwa bila taarifa sababu wako ktk eneo la hifadhi kwa nini wamemzuia magufuli kuvunja nyumba za watu waliojenga ktk hifadhi ya barabara? Tena yeye alitoa notisi. Wote si wamevunja sheria wamevamia maeneo ya hifadhi! Au wale wa chanika si watz? Dah hii nchi inaendeshwa hovyo hovyo saana kweli kuna fairness? Usawa mbele ya sheria ka unavyoanishwa kwenye katiba unafatwa? Au sababu wengi wa wananchi wa chanika ni maskini?
   
Loading...