Ya Butiku, Qaresi na Kikwete nani zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Butiku, Qaresi na Kikwete nani zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sajenti, Dec 17, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Baada ya mtifuano uliotokea hivi karibuni ambapo wanasiasa wakongwe nchini Joseph Butiku na Matei Qaresi kueleza udhaifu wa raisi kikwete katika uongozi wake kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu,na baadae JK kudai kuwa atafanyia kazi yaliyozungumzwa na hatimaye kuwajibu wanasiasa hao.
  Nimekuwa nikifikiria busara na hasa kwa JK kutaka kujibu hoja za akina Butiku badala ya kuona kuwa ana bahati watu wanamshika sikio kuwa gari analoendesha linaacha barabara na kuingia porini, sidhani kama ni sahihi kwa kwake kuanza kufanya majibizano. Nilidhani kma kiongozi wa nchi ashukuru kuwa wananchi wake wanafatilia uongozi wake kwa umakini na wako tayari kumuamsha usingizini pindi akilala wakati muda wa kulala bado.....Kuna ule msemo wa kichaa akikuvua taulo ukaanza kumkimbiza ukiwa uchi sijui watu watajua tofauti???...Ni mtazamo wangu tu.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Tatizo mkuu anaona anaonewa kwa sababu hata sisi tunaowaona ndio wapiganaji wa ufisadi *(Mwakyembe. Kilango nk) wanamsaport na kumsifia JK,
  sasa kwa Wazee hao (Butiku na Qares) ni kama watu walioshindwa na wasiojua siasa za nchi hii, hivyo hata kauli zao hazina nguvu kwa umma wa WaTanzania, na kama atawajibu bac kwa asilimia kubwa atawajibu kwa dharau na kebehi kuwa hao ni watu walioshindwa
   
 3. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kituko unadhani kwa mtazamo wako ni kweli kuwa hawa wazee ni watu walioshindwa? Yawezekana jibu likawa ndio lakini kwangu mimi nina mtazamo tofauti kwani si watanzania wote tunaweza kupata sehemu ya kueleza hisia zetu kuhusiana na uongozi wa JK. amekuwa akitoa hotuba kupitia vyombo vya habari kila mwisho wa mwezi lakini hakuna fulsa ya kutaka hata kumuuliza swali. Siku alipojifanya kuwa atafanya mjadala wa moja kwa moja kwenye TV kama uliangalia kipindi kile maswali yalikuwa filtered kupunguza ukali wake...why?? Hao wanao-filter hayo maswali may be kwa kuhofia kuwa anaweza kukosa majibu wanadhani watanzania wote tuna mtazamo unaofanana na wao kuhusu uongozi huyu jamaa?? wengi wako pale kuneemesha matumbo yao wakati majority ya watz wanapigika sio pole pole kila siku ni ngumu afadhali ya jana... Mi naamini Butiku na Qaresi wamewakilisha idadi fulani ya watanzania ambao we are not happy na leadership yake?? mi binafsi nimependa comments za akina Butiku pamoja na kejeli wanzowatupia.
   
Loading...