Ya Balozi wa China Dhidi ya Charles Teila na ALmasi ya damu(BLOOD DIAMOND)LIBERIA.

RC.

JF-Expert Member
May 24, 2012
444
41
Mambo yaliyofanywa na Balozi wa China nchini TANZANIA,yameanza kutuonesha rangi halisi ya hawa tunaowashabikia kila siku na misaada ya kutusaidia kwenye maendeleo,tukitafakari yanayotokea katika nchi nyingi za AFRICA leo hii ni matokeo ya hawa mabalozi wa nchi za kigeni kuchota taarifa za nchi zetu na kuzitumia kuunda makundi haramu yanayoibuka kupigana na serikali za nchi zao kwa kisingizio cha kudai haki,kama tunavyoshuhudia makundi kama M23 Linalopambana na serikali ya kabila huko Congo DRC,SELEKA REBELS katika Afrika ya kati,AL-SHABAAB(SOMALIA),TUAREG-REBELS,North-Afrika,BOKO-HARAM(Nigeria), ANSALDIN WEST AFRIKA,kwa kutaja machache, makundi haya yamepelekea nchi nyingi za kiafrika kukosa utulivu na kupelekea ndugu zetu waafrika kutangatanga bila makao maalum,na kuwafanya kama sehemu ya maonesho ya ufukara huko ulaya kwa kuwafanya chanzo cha kupatia mitaji ya kuja kuanzisha NGOS,uchwara za kuwasaidia kwenye makambi ya wakimbizi kwa chater ya umoja wa mataifa.


Balozi huyu wa China kaonesha kile wenzake huwa wanakifanya siri,kwamba watu hawa yaani mabalozi hawako kidiplomasia kivile ila wapo kimaslahi ya mataifa yao,na pale maslahi ya nchi zao yanapoonekana kuzidiwa kete na wananchi hukimbilia kuokoa jahazi kwenye mikutano ya chama tawala kama tulivyoshuhudia kwa balozi wa china nchini Tanzania.

Mabalozi kama huyu wa China wako tayari kufadhili makundi haramu nchini ili kulinda maslahi ya nchi zao kwenye nchi hasa zenye upinzani mkubwa,kama tuonavyo mtiti unaoendelea kwa ndugu zetu nchi za kiafrika. Sio jambo geni kwa watu kutoka nje ya nchi kufadhili vita na hata kuuza silaha kwa makundi hasimu ili wavune rasilimali za nchi husika.Kwa bahati nzuri mambo haya tunayaona kipindi hiki ambapo china imesaini mikataba zaidi ya 19 na chi yetu na mikataba hii hatujaambiwa walisaini nini humo,pia tunashuhudia ujenzi mkubwa wa miundombinu ambayo inauwezo wa kusafirisha mizigo mizito kama makaa ya mawe na ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka huko Mtwara kuja BAGAMOYO, Na Nchi yetu kuwa kwenye maandalizi ya kuchimba URANIUM.Sio ajabu huyu balozi kaona maslahi makubwa ya nchi yake kutishiwa na vuguvugu la mabadiliko linaloshika kasi hapa nchini na kuhofia kupata hasara pindi Chama kingine kitakapoingia madarakani na kupitia upya mikataba yote kuona kama inamaslahi kwa nchi au la!.

Watanzania tusikubali ujinga wa nchi hizi za magharibi na Asia kutuamulia mambo yetu ya ndani kwani Chama tawala kilichopo madarakani kimeongoza muda mrefu na kutokana na muda huo wote kimeweza kuuza rasilimali za nchi na kujibinafsishia mali za taifa hili lukuki kama viwanja vya mipira vyote Tanzania,majengo makubwa makubwa,Ardhi,migodi ya madini,kuuzia nchi marafiki mbuga zetu za wanyama kwa mataifa ya kiarabu na kutoa tunu za taifa letu kama wanyama muhimu kama Twiga na tembo na kuuza mali za nchi yetu kwa mataifa rafiki kwa kisingizio cha uwekezaji na uliokuwa urafiki kati ya marais wetu watangulizi kama ilivyo kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mao Tse Tung wa china. Hivyo Chama hiki hakitasita kutuhadaa kwa kuwaleta wachina na kutuzuga ili waendelee kutubinafsisha.

Sioni logic iliyopo kwa balozi anaeiwakilisha nchi,kwenda kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuvaa kofia ya chama eti chama kilichomteua kuja nchini ni chama rafiki na ccm! kwa maana hiyo mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wako hapa si kuziwakilisha nchi zao bali kufanya siasa za nchi wanapofanyia kazi!

Ulimwengu ulishuhudia jinsi watu matajiri kutoka nje ya Afrika walivyofadhili mauwaji huko Liberia chini ya aliyekuwa Rais wa Liberia anaetumikia kifungo huko The Hague Charles Teila,walitoa silaha kwa mabadilishano na Almas.(BLOOD DIAMOND) na hapa nchini kwetu huko ndiko tunakoelekea kwani mabomu ya Arusha kwenye mkutano wa CHADEMA yalitengenezwa CHINA,na tunashuhudia jinsi China inavyojiingiza kwenye siasa za nchi yetu kwa kujitokeza kwenye majukwaa ya kisiasa na kuvaa kofia za chama tawala, pia tumeshuhudia makada wa chama cha ccm wakivaa kofia za Jeshi la China,na wengine kufunga safari ya kwenda kwenye mafunzo huko,pia tumeshuhudia mauwaji ya kutisha ya Tembo ambao pembe zao ni biashara kubwa huko asia hasahasa nchi za china na Philipines.

Wasiwasi uliopo ni kuwa kama watanzania watakiangusha chama cha ccm madarakani,tutapona kweli na mauwaji ya halaiki kama yalivyotokea kwenye nchi za wenzetu kama Liberia na Rwanda na Burundi na mauwaji ya kutisha yanayoendelea huko Somalia na SYRIA.

Wito;Tunaomba mabalozi wote walio hapa nchini kufanya kazi iliyowaweka hapo na si kuingilia siasa za nchi husika kwani Bara la Afrika limejaliwa kuwa na viongozi wasiojali maisha ya raia wao na hawaoni tatizo kukatisha maisha ya raia kulinda maslahi ya wakubwa,wako tayari kuuza utu wao kwa kuwafurahisha mabwana zao, hivyo basi iwapo balozi wa nchi yoyote atatumia wadhifa alionao kutafuta umaarufu na kuchochea vurugu kama huyu wa Balozi wa China, hakika hatutamvumilia.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
mimi ninaungana na huyo balozi kwa kuangalia value of money!! unatakiwa ufuatilie biashara yako kama uliowatuma wanafanya kazi?

Ila tunakoelekea hili bara la Africa litagawiwa vipande vipande tena. China itachua Msumbiji, Tanzania na Sudan ya Kusini. Uingerza itaichukua Zimbabwe (baada ya Mugabe kuo...), Botswana(kwa sasa wamekwisha ichukua kwa 60% paale De-Beers), Mongolia(ingawaje iko nje ya Bara), SA kilichopo ni kiini macho tu ila raslimali zote wanmiliki wao. Ghana tayari ila wameikosa Kenya. Marekani nayo ina compete na China. viongozi wetu hawa ni vibaraka tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom