Ya akina Sabaya na awamu ya tano yasifumbiwe macho

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,444
2,000
Awamu ya tano imelalamikiwa sana kuhusiana na ukiukwaji mkubwa wa haki za watu.

Pana watu wengi wameuwawa, wamepotezwa na wengine wamejeruhiwa. Wapo ambao wamefilisiwa, wamenyanyaswa, wako magerezani au mikononi mwa dola hadi sasa kinyume kabisa na utaratibu.

Wapo waliokuwa na dhamana za kutoa haki badala yake walifanya yao.

Watuhumiwa hawa wanajulikana kwa majina yao, vyeo vyao, kwa waliyoyafanya na hata kwa waliowafanyia. Kwamba baadhi yao wangalipo serikalini awamu 6, wapo huko wakimtumikia nani?

Mama Samia unaposafisha nyumba ya awamu hii usikubali wenye mikono michafu au yenye damu za watu kuwa sehemu ya watendaji wako.

Zaidi sana, kikulacho ki nguoni mwako.

Huyu wa Hai kama papa wavumao baharini, alikuwa ni mmoja wao tu. Wapo wengi na asifumbiwe mmoja macho.

Viva awamu ya sita utuletee haki na maridhiano vilivyo kuwa vimegeuka kuwa bidhaa adhimu!
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,139
2,000
Nitafurahi sana iwapo atawafyekelea mbali Mataga wote. Walitusumbua sana shenzi hawa, enzi za yule malaika wao.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,444
2,000
Nitafurahi sana iwapo atawafyekelea mbali Mataga wote. Walitusumbua sana shenzi hawa, enzi za yule malaika wao.

Pana watu wanamzunguka pale si wema hata kidogo. Hawana hata chembe ya aibu kuweza kujitathmini wenyewe.

Mama alifyekelee mbali genge hili ambalo pia ni lile lile lililokuwa limedhamiria kumzimia yeye urais wake.

Hata Chokochoko zote zinazosikika bandarini zinalihusu sana genge hili.

Kikulacho hakijawahi kuwa nje ya nguo zako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom