Xiaomi products via AliExpress

Mtu mbalimbali

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
315
413
habari zenu wakuu
naomba kuuliza kwa wajuzi wa online martkets
ninataka kuagiza xiaomi mi 11 ultra (133$) kupitia AliExpress hivo unaomba kufahamishwa ubora wa bidhaa zao pamoja na uaminifu na accuracy ya uwasilishaji wa bidhaa zao hapa Tanzania
karibuni wakuu kwa msaada

picha
Screenshot_20210720-111640.jpeg
 
habari zenu wakuu
naomba kuuliza kwa wajuzi wa online martkets
ninataka kuagiza xiaomi mi 11 ultra (133$) kupitia AliExpress hivo unaomba kufahamishwa ubora wa bidhaa zao pamoja na uaminifu na accuracy ya uwasilishaji wa bidhaa zao hapa Tanzania
karibuni wakuu kwa msaada

picha View attachment 1860791
Kama mdau alivyokujibu hii sio simu ya Xiaomi, imeandikwa tu mi 11 ultra. Hapo unapigwa mchana kweupe.

Ukinunua kitu chochote sio lazima Aliexpress, hata Amazon ama eBay Hakikisha unanunua toka store kubwa, mfano Store yao wenyewe Xiaomi ama hata store kubwa yenye ratings nzuri.

Mfano simu kama hio kauza pisi 52 tu lazma ushtuke kidogo.
 
Nadhani utakuwa umezinduka.

Ni rejee katika maswali yako.
Swali la 1: Ubora wa bidhaa
Jibu: Bidhaa zao nyingi ni bora kulingana na uchaguzi wako na bei ya bidhaa husika.

Mfano: ni katika uchaguzi wako hapo juu hiyo bei ya simu haiendani na bei halisi na thamani ya simu husika (Original)

Umepewa hiyo bei kutokana na thamani ya bidhaa.

Muhimu kabla hujafanya malipo angalia
Specifications za bidhaa, angalia reviews za wateja walionunua bidhaa husika.
Na Seller ameuza items ngapi.

Swali la 2: Uaminifu ni mkubwa ila siwezi kusema asilimia 100% kwasababu seller lazima atatuma mzigo kulingana na aina ya msafirishaji ulie mchagua na address uliyoweka sasa panapo baki ni usalama wa mizigo wako pindi ikiwa njiani.

Lakini mzigo wako utakufikia kulingana na ainanya address uliyotumia.
Uaminifu ni mkubwa.
 
Uaminifu wa kukufikishia bidhaa yako ni mkubwa cha muhimu check na specifications za item then buyers review.

Lakini kwa uaminifu AliExpress yuko poa.
 
Ukiona kitu kinauzwa bei ndogo sana kuwa makini, angalia vizuri jina na specifications

Screenshot_2021-07-21-06-32-54-394_com.alibaba.aliexpresshd.jpg


Screenshot_2021-07-21-06-35-49-577_com.alibaba.aliexpresshd.jpg
 
habari zenu wakuu
naomba kuuliza kwa wajuzi wa online martkets
ninataka kuagiza xiaomi mi 11 ultra (133$) kupitia AliExpress hivo unaomba kufahamishwa ubora wa bidhaa zao pamoja na uaminifu na accuracy ya uwasilishaji wa bidhaa zao hapa Tanzania
karibuni wakuu kwa msaada

picha View attachment 1860791
Umefanya vema kuuliza. Kama wengine walivyosema, hakuna MI 11 Ultra ya bei hiyo. Simu halisi ya hivi inacheza hadi milioni mbili kwa sasa kama sikosei. Siku hizi usipate shida. Ingia tovuti ya kampuni husika, kula shule kwanza huko ya bidhaa zao. Mfano kwa hawa jamaa, ingia hapa uzione simu zao. Xiaomi Global丨Official Website丨Mi.com - Mi Global Home , Ikifunguka, ingia mi phones. Tafuta model yako uielewe kisha ndo uwasikilize matapeli mtandaoni.

Kuhusu ubora , kampuni haina shida. Sema bidhaa moja na nyingine zaweza kutofautiana ubora ndani ya kampuni husika. Kuhusu kununua mtandaoni, sina uzoefu hapa bongo. Lakini, uzoefu unaonesha hakuna uhakika wa 100%
 
Back
Top Bottom