X-ray

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,620
1,796
Habari zilizotujia kutoka mahakama ya mwanzo kisutu, zinasema kuwa, kijana mmoja kafikishwa mahakani kwa kosa la kumuibia dada mmoja mkufu wa dhahabu, na kuumeza tumboni, baada ya kusomewa kosa lake na kumuonyesha uthibitisho wa picha za x-ray alizofanyiwa hospitalini ili kumthibitishia kosa lake.

Hakimu akamuuliza mshitakiwa, Kama ana lolote la kujitetea?

Kijana: Ndio bwana Hakimu ninalo neno moja nataka kusema...!

Hakimu: sawa kijana unaweza kujitetea...!

Kijana: (Akaanza). Bwana Hakimu ningependa kuishukuru serikali yetu tukufu kwa kuweza kuweka vifaa vizuri vya kufichuwa vitu vikiibiwa na wezi kama mimi na hata vikifichwa tumboni kwa kumezwa, lakini ninauliza jambo moja tu Bwana Hakimu.

Kwanini serikali haijaweka vifaa X-RAY vya kufichuwa WAHESHIMIWA WANAO IBA MAMILIONI YA FEDHA AMBAZO NI MALI YA UMMA WA WATANZANIA WOTEE?!!
Asanteni Bwana Hakimu, sina zaidi...!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom