Wydad AC waipiga Al Ahly 2-0 watwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2021/2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
284497867_131173782870365_125623618948574667_n.jpg

Mabao ya dakika ya 15 na 48 yakifungwa na Zouhair El Moutaraji yameipa Wydad AC ya Morocco ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wababe wa Misri, Al Ahly.

Al Ahly ambao walikuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo wa Mei 30, 2022 wameshindwa kufurukuta katika fainali kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco.

Ubingwa huo ambao ni wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili.

284559144_554250756086836_6901572611824025448_n.jpg
 
Kipute Kimeisha..Wydad Wanaondoka Kidedea kwa Ushindi wa Mbili bila.
Mabingwa Wapya Wydad Casablanca.

Lazima hapa lipo Somo kwa Yanga, Simba, Coastal na nani sijui Watakaofuzu Michuano ya Kimataifa Mwakani.

Hakuna njia Ya Mkato.

Inahitajika KUJIPANGA..!
 
Hongera kwao wydad casablanca! Al ahly amechukua xana hacha na wengine walibebe.....waarabu wa egypt wanaenda kumfurusha pitso mosimane for sure,walimuwinda kwa kila hali ateleze sasa ameingika kwenye 18 zao....namuomba tu pitso akiwa anarudi SA ampitie nandugu yake pablo wa simba hapa waende nae huko nasikia kunatimu inamuhitaji....pole kwa miqisson kwa kushindwa kunyanyua kwapa medal ya mshindi wa pili inatosha, pole kwa msuva kwa kupishana nakikombe...
 
Simon Happygod Msuva gemu hili la fainali angekuwepo na kuonekana duniani kote hivyo kuwa rahisi kuhamia timu nyingine kubwa.

Sijui ni nini kilimkumba Msuva na Wydad Athletic Casablanca wakaachana wakati usio muafaka kwa mchezaji huyu mtanzania.
 
30 May 2022

Al Ahly SC vs. Wydad AC - TotalEnergies CAF Champions League Final 2021/2022

Source : CAF TV
 
Simon Msuva: Haki itafuata mkondo wake​

2 months ago

1653960251354.png

Kiungo Mshambuliaji wa Tanzania Saimon Happygod Msuva amesema Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ lipo pamoja naye, katika mapambano ya kudai haki zake dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Msuva anakabiliwa na changamoto ya kimaslahi na Uongozi wa klabu ya Wydad Casablanca aliyoitumikia tangu mwaka 2020, hali ambayo ilimfanya kurejea nchini hadi mambo yake yatakapokaa sawa.
Kiungo huyo ambaye aliwahi kuitumikia Young Africans kabla ya kutimkia nchini Morocco mwaka 2017, amesema anaamini suala lake la madai ya kimaslahi ambalo lipo FIFA litamalizwa kwa haki.

“TFF ndio kama baba kwa wachezaji, hivyo wapo pamoja na mimi. FIFA pia tulipopeleka mashtaka wapo pamoja na wachezaji wote wakiangalia haki na kulinda vipaji vyao, kikubwa tusubiri kesi inatoka na majibu gani, nikishindwa sijui itakuaje lakini kama nikishinda basi kuna kiasi kikubwa cha pesa nitapata.” amesema Msuva.

Msuva ametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoingia kambini baadae mwezi huu kwa ajili ya kujiandaa michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki
 
Yule dogo moutaraji amepiga bonge la goli lile la kwanza wachezaji wetu wana safari ndefu Sana sijui Kama tutafikia hatua hiyo tukiendekeza propaganda za kijinga
 
Yule dogo moutaraji amepiga bonge la goli lile la kwanza wachezaji wetu wana safari ndefu Sana sijui Kama tutafikia hatua hiyo tukiendekeza propaganda za kijinga
Lile goli mbona halina tofauti na la juzi, la Fei Toto!
 
View attachment 2245015
Mabao ya dakika ya 15 na 48 yakifungwa na Zouhair El Moutaraji yameipa Wydad AC ya Morocco ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wababe wa Misri, Al Ahly.

Al Ahly ambao walikuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo wa Mei 30, 2022 wameshindwa kufurukuta katika fainali kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco.

Ubingwa huo ambao ni wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili.

View attachment 2245016
SAFI SANA WATAKUWA NA YANGA KUNDI MOJA NA YANGA WATALETA KOMBE

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mpira ule uliopigwa nimeamini timu zetu za simba na yanga kwenye haya mashindano hatua tunakofikia nakutolewa ni stahiki yetu na kiwango chetu kinakoishia.Kama tunahitaji kupiga mpira mkubwa kama ule inatakiwa tujipange kikweli kweli sio kutegemea uswahili swahili.
 
Back
Top Bottom