Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (Mei 03, 2022), Maadhimisho hapa Nchini yameanza rasmi leo Mei 01, 2022 Jijini Arusha
Kaulimbiu ya Siku hii kwa Mwaka 2022 inasema "Uandishi wa Habari na Changamoto za Kidijiti"
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema changamoto zipo katika Tasnia ya Habari, na ni muhimu kutafuta suluhu ili kusonga mbele. Ameeleza kuwa, Serikali ipo tayari kushirikiana na Wadau wa Habari
Akizungumza leo katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ametoa rai kwa Wanahabari kuendelea kutimiza wajibu wa licha ya mazingira kuwa na changamoto kadhaa
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesisitiza Serikali inatakiwa kuwa tayari kushirikiana na Wadau wa Tasnia ya Habari
HALI ILIVYO DUNIANI
World Trends in Freedom of Expression and Media Development: Global Report 2021/22 (UNESCO)
Katika miaka mitano iliyopita, maombi ya Serikali kutaka maudhui yaondolewe kwenye majukwaa makubwa mtandaoni yameongezeka maradufu
Kati ya Mwaka 2016 hadi mwishoni mwa Mwaka 2021, Waandishi wa Habari 455 waliuawa wakiwa kazini au kutokana na kazi zao
Aidha, 85% ya Idadi ya Watu duniani kote walipitia hali ya kuzorota kwa Uhuru wa Vyombo vya Habari katika miaka mitano iliyopita
MAXENCE MELO: DIJITALI INACHOCHEA MAMLAKA KUCHUKUA HATUA MAPEMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo anasema Dijitali imetoa fursa kwa Maudhui ambayo huenda yasingekuwa rahisi kuruhusiwa na Mhariri au Chombo cha Habari
Ameeleza, "Katika safari hii ya Dijitali najua kuna uoga wa mabadiliko. Changamoto kubwa ninayoona ni dijitali imekuwa ikidhibitiwa kisiasa"
HAKI YA FARAGHA INALINDA UTU WA WATU
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums amesema katika dunia ambayo Nchi haiweki Sheria ya Faragha, utu wa watu wake unaweza kuwa matatani
Ameeleza, "Utu wako katika ulimwengu wa kidijiti ni wa kupigania kwa nguvu zote. JamiiForums kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali tunaendesha mafunzo ya usalama wa kidijiti. Tunaahidi kufanya mafunzo haya kwa Waandishi wa Habari"