Wote wanaomshabikia Cristiano Ronaldo hawajui mpira na ni Wakengeukaji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Sijaona ambacho anakifanya leo hii Christiano Ronaldo na hakikufanywa na Fundi Lionel Messi miaka miwili mitatu nyuma. Halafu nimegundua kuwa wale wote ambao kutwa wanamshabikia na kumfagilia Christiano Ronaldo ni Washamba wakubwa, wageni wa masuala ya Mpira na watupu mno Kiuchambuzi na Kiutaalam wa masuala ya mpira.

Acheni ushamba tafadhali Christiano Ronaldo bado sana kwa Lionel Messi.

Nawasilisha.
 
Huu ni ukweli mchungu.

Ronaldo ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani, lkn Messi ni kiumbe ambaye amewahi kuugusa mpira kwa nanma ambayo hakuna kiumbe chochote duniani kinachoweza kufikia japo robo ya umahiri wake. Itamchukua Mungu miaka mingi sana kumuumba Messi mwingine.
 
Messi ndio nani?

Zinedine Zidane Manager / Kocha wa Real Madrid anamjua vizuri na tena zaidi yako Wewe POPOMA wa Christiano Ronaldo. Acheni kumpamba Christiano Ronaldo wakati ni mchezaji wa kawaida mno ambaye hata Mohamed Ibrahim au Shiza Kichuya wa Simba SC wanaweza wakamfikia na hata kumzidi sema tu bahati mbaya wapo Madongo Kuinama huku Afrika na bado hawajawa tu exposed kama Yeye.

Lionel Messi ndiyo habari ya mjini na ndiyo maana hata Manguli / Legends wenyewe Pele na Maradona wameshakiri kuwa Messi siyo wa Sayari hii tunayoishi sisi Mangumbaru / Hopeless.
 
Mkuu unazungumzia kipi hicho ambacho Messi amewahi kukifanya miaka miwili mitatu nyuma?!.

Miaka 5 mfululizo Ronaldo anaongoza kwa ufungaji bora kwenye UCL,huyo Messi amefanya hivyo lini?!.

Wengi wetu tunamsifia CR7 kwa ufungaji wake wa umahili ambao ameuonysha kwa miaka 5 bila upinzani wowote hata wa huyo Messi.

Messi ni mzuri,lakini CR7 amethibitisha hana mpinzani.

Ni hayo tu.
Sijaona ambacho anakifanya leo hii Christiano Ronaldo na hakikufanywa na Fundi Lionel Messi miaka miwili mitatu nyuma. Halafu nimegundua kuwa wale wote ambao kutwa wanamshabikia na kumfagilia Christiano Ronaldo ni Washamba wakubwa, wageni wa masuala ya Mpira na watupu mno Kiuchambuzi na Kiutaalam wa masuala ya mpira.

Acheni ushamba tafadhali Christiano Ronaldo bado sana kwa Lionel Messi.

Nawasilisha.
 
Huu ni ukweli mchungu.

Ronaldo ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani, lkn Messi ni kiumbe ambaye amewahi kuugusa mpira kwa nanma ambayo hakuna kiumbe chochote duniani kinachoweza kufikia japo robo ya umahiri wake. Itamchukua Mungu miaka mingi sana kumuumba Messi mwingine.
MUNGU wako wewe!
 
Mkuu Gentamycine nini kimekusibu???
Zamani ulikua unakuja na post zenye facts na point tupu ila siku hizi unapost mataputapu kila kukicha ,heshima yako inashuka kwa kasi kama uchumi wa TZ.

Kumpenda kwako Messi hakumfanyi CR7 kutokua bora.

Jiandae kisaikolojia kumuona CR7 kama ballon dor winner kwa mwaka huu!
 
CR7 is a complete player. Anatumia miguu yote miwili kwa umahili mkubwa, ana kasi, anafunga magoli ya vichwa, penalty, adhabu ndogo na ana uchu wa ushindi. Sifa hizi Messi pia anazo ila ana upungufu mmoja hawezi kutumia mguu wa kuume kwa umahili.
 
Back
Top Bottom