Edson
JF-Expert Member
- Mar 7, 2009
- 9,846
- 5,076
habari za siku ndugu zangu
napenda kushea pamoja nanyi japo kwa ufupi juu ya mazungumzo niliyofanya mimi na baba yangu alipokuja kunitembela huku nilipo pamoja na kuhudhuria sherehe za ubazo wa mjuu wake.
nilimuuliza baba juu ya mambo mbalimbali kuhusu taifa langu Tanazania na wapi linaelekea.
Edson: baba, vipi huko nyumbani kwa ujumla kuna jipya? i meana mabadiliko yoyote ya kiuchumi?
baba: kwa ujumla nyumbani hatujambo na wote wanakusalimia sana na kuhusu nchi, amani ipo ila utulivu ndo umenza kutoweka taratibu.
edson : kwa nini baba una maana gani kusema hivyo?
baba: ninaposema utulivu umeanza kuondoka ni hiv edson, kwa sasa hali ya maisha ni ngumu sana, kila kitu kimepanda bei mara dufu, yale walioahidiwa hawayaoni na mda unazidi kwenda na kikubwa kinachotia hasira ni kwamba hakuna mikakati madhubuti ya kuonyesha kuna njia mbadala inayofanyika ili walau makali ya maisha yapungue, wao huko serikalini tunasikia kuna baadhi yao wana kesi za kufuja mali ya umma lakini ndo hivyo hukumu bado.watu wamenza kukata tamaa sana na siku hizi kuvumiliana hakupo.
edson: duh! kipindi kile natoka huko niliacha sakata la richmond, vip baba akina edward walifikishwa mahakamani?
baba: edward yup? lowassa au hosea?
Edson; wote wawili.
baba: wote wapo mtaani, hiv unadhani lowassa anaweza kufikishwa mahakamani?! au huyu hosea? thubutu
edson : kwa nini baba
baba: huyu hosea waliunda sijui tume mara wakafikishwa kwa waziri mkuu, pinda akasema atatoa maamuz lakini mapaka leo ni kimya, mimi sijasiki kitu labada kama wametangaza leo iwapo wamechukuliwa hatua yoyote.
Edson: hapa majuzi nilisikia kupia mtandao, hasa jamii forum, kuwa kuna madhara yatokanayo na migodi uko musoma, watu wanadhurika sana ngozi, eti baba serikali yetu inasemaje, na hvi haya madini siku hizi vip tunafaidika nayo au ndo hakuna kabisa?
baba:jamii forum ndio nin?
edson:jamii forum ni forum inayojumuisha watu makini na wa rika tofaut kupita mtandao ambapo watu wanatoa mada na kuzijadili kwa uwazi zaid,na hapo ndipo huwa napata taarifa nying i sana juu ya matukio ya huko nyumbani
baba: unajua mwanangu, tanzania sio maskini. we are not poor by accident; we are poor by choice.nchi yetu ina kila kitu, yaani kila kitu kipo sasa hiv wanatafuta mafuta, inasemekana yapo, sisi tumekuwa kama wawindaji, unajua nini edy;
edson:ndio baba
baba. muwindaji siku zote yeye, ana tabia moja, akienda kuwinda anaweza kushinda porini siku nzima anakimbiza swala,na akirudi nyumbani jioni anarudi na swala mmoja tu.lakini kumbuka ameshinda siku nzima porin.
edson: ehe
baba: na kikubwa zaidi au tatizo kubwa zaidi au kibaya zaidi kwa lugha nyingine ni kwamba anaua kile alichopata, anakula na kesho asubuhi huyo anarud porini kuwinda.ndivyo tanzania ilivyo.
eedson: sijakuelewa baba hapo
baba; hujaelewa nini, yaani kuja kwako huku ulaya na kusoma kote huku bado hujaelewa nilichokisema!!?
edson: kweli baba, maneno magumu hayo;
baba:sikiliza nikwambie edy, kuna watu wanazaliwa tumbo moja baba mmoja na mama mmoja, wanalelewa na wazazi wao mpaka wanakuwa watu wazima lakini baadae katika maisha unakuta mmoja wao ana mwisho mbaya sana, maisha magumu nk.
edson: yaan sasa hapo baba umenipoteza kabisa!
baba: ni hiv, sisi siku zote tumekuwa kama wawindaji, kila tunachokipata tunakiua,na ndio maana hatuendelei kabisa, madini yapo ya kila aina lakini hali za kiuchumu za watu ni duni sana.tumeuza na kuwapa wazungu hawa kila kitu faida ni kdogo na hata wakati mwingine hatuioni kabisa. viongozi wapo lakini porojo nyingi. kuna nchi ngapi tumepata uhuru pamoja, lakini wenzetu wako mbali.raisi mzima anatoka na ujumbe wa watu zaidi ya100 kuja huku ulaya namarekani eti kutafuta misaada na kujifunza toka huku. huu ni uppuzi wa hali ya juu sana. kuna nchi kana rwanda na burundi wale majuzi hapa wamepigana sana, wamemalizana kama kuku lakini nenda pale leo uone nchi inavyopiga hatua, kwa nini wasiende rwanda kujifunza?!
edson: yahh ni kweli baba, sasa wewe unafikiri tatizo liko wapio kwa nchi yetu:
baba: kwanza viongozi,kuanzia raisi hadi hawa wa chini huku hawana dira wapo tu bora liende, mimi nawanbia wanangu kama elimu zenu hizi mnazopata hamtazitumia kwa makini mtakufa nafanya kazi za watu.unaajiliwa tuuuuu mpaka mwisho. serikali imekosamwelekeo afadhali na kipindi kile cha nyuma, siku hizi wziri mwizi,mwnasheria mkuu anakula rushwa, jaji yaani wote.
edson: sasa baba nini kifanyike ili tuondokane na khali kama hii
baba: hv kwanza nikuulize, kwa nini umeamua kuoa huku na si nyumbani?
edson: baba tutaliongea hilo wakati mwingine lakini kwa kifupi ni uamzi tu nimefanya
baba: anyaway sawa lakini uwe makini sana, hawa watoto wapajue uliokotoka sio wakae huku na kwa nini umemwita jina hili (blanca) na si jina la mama yako kama ilivyo desturi yetu?
edson: ni jina tu baba nimemwita mwenyewe wala sikusukumwa na mtu. naomba turudi kwenye mada yetu
baba : sawa, sasa sikia kuhusu hili kwanza inabidi viongozi wache njaa, unajua ukiwa na njaa mambo mawili au matatu lazima uyapate:
edson : yapi hayo baba?
baba: kwanza utafanya maamuzi ambayo si sahihi, yaani ukiwa na njaa some one can buy you very cheap!!!. na mara nyingi mikataba mibovu ya nchii yetu iko hivyo, unakuta waziri ana njaa yake, anataka rushwa, mara mwingine afutie kodi makampuni mengine ili mradi tu amepata chake nk; raisi mwenye hatoi hotuba za kuwafanya watanzania wajitegemee kifikra zaidi. yeye akiongea sana sana utamsikia anasema '' nchi yetu bila wahisani hatuwezi kuendelea kwa hiyo safariza nje ni muhimu sana'' yaan anaongea ongea tu.lazima tujifunze kutunza kile kidogo tulicho nacho tukizalishe ili kitusaidie, muwinda mwenye akili ni yule anayewinda na anapopata anakitunza, anakizalisha ili kimsaidie kesho asikimbie tena porini kwenda kuwinda. vinginevyo tutakuwa omba omba kila siku.
edson: nafikri hiyo itasaidia kidogo na pengine watu wakitumia elimu zao vizuri, kwa manufaa ya umma na kwa taifa kwa ujumla.
baba: masomo unamaliza lini na unategemea kurudi lini nyumbani au tayari umeomba uraia huku ( huku akicheka)
edson: masomo mwaka kesho, na nitarudi tu ila namsubiri kwana huyu( mama blanca) naye amalize wakati huo mimi nitakuwa naendela na kazi.sijaomba uraia baba.
baba; sawa na sasa mahali inakwaje?
Edson: sijatoa, kwa kuwa uko huko tutaangalia uwezekano maana wazaz wote wa pande mbili mpo huku
baba: najisikia kuchoka sana,
edson: unaweza kwenda kuonga maana pilika za sherehe zilikuwa sio mchezo.