wote tusome hii part two | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wote tusome hii part two

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Edson, Jul 21, 2009.

 1. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  habari za mda wana jf wenzangu.

  leo napenda pia kushea nanyi kwa mara nyingine mazungumzo yangu na baba yangu tuliyofanya kwa njia ya simu mara aliporejea nyumbani toka huku niliko alipokuwa amekuja kuhudhuria sherehe za ubatizo wa mjukuu wake.

  edson: hallooo, halloo baba!

  baba: hallo, edy

  edson; shikamoo baba

  baba; marahaba, habari za huko? mjukuu wangu hajambo?

  edson: huku salama, na mtoto hajambo. ehe baba safari ilikuwaje baba mlifika salama?

  baba;tunamshukuru Mungu sana, maana tumefika salama hatukupata tatizo lolote na pia tunakushukuru sana wewe pamoja na mkeo kwa ukarimu wenu

  edson: mama hajambo?

  baba: hajambo kabisa yuko kwenye banda la kuku anawapa maji.

  edson: vipi huko nyumbani baba mambo yakoje?

  baba: kwa ujumla wote hapa wazima japo matatizo ya hapa na pale yapo, ila mambo yanaenda. serikali iko kwenye bajet wanapitisha bajet mbalimbali.

  edson: nimekumbuka miezi ya bajeti hii.unaionaje bajet hii ya mwaka huu italeta nafuu yoyote kwa mwananchi wa kawaida?

  baba: bado mambo ni magumu, hakuna nafuu yoyote hapo.bidha zimepanda, chakula, yaani kla kitu.kwa kifupi edson hakuna nafuu.

  edson: hivi baba tatizo liko wapi mpaka nchi yetu inakuwa hivi yaani bado masikini wakati ina kila kitu?

  baba: kuna mambo mengi yanachangia, hapa kuna makosa ya serikali na pia kuna makosa yetu sisi wananchi mmoja mmoja

  edson: sasa wananchi baba wanaingiaje hapo?

  baba: subiri nikwambie mtoto, serikali haina mipango endelevu na inayolenga mbali, project nyingi ni za miaka 5 au kumi,unajua nchi yoyote ikitaka kupiga hatua lazima kwanza watu wake wawe na elimu ya kutosha, lazima serikli ianzishe taasisi za utafiti,wengine wanaziita research and development au R&D kwa kifup. vitu hiv hapa kwetu hakuna kama zipo hakuna sapot yoyote toka kwa serikali,na ndio maana sasa hv ukifika tanzania kuna watu toka nje wanafanya kazi ambazo sisi tunaweza kufanya wanalipwa mshahara mnono,elim zao za kawaida tu.pia rushwa imeinga ndani ya nchi hii yaani edy hakuna kiongozi msafi hapa. wapo wachache lakini wamefunikwa na kundi kubwa la wala rushwa..

  edson; sasa baba rais .....

  baba: subiri nikwambie usinikatishe. ukiona hadi mwanasheria mkuu wa nchi, mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa wote hawa wanakula rushwa unadhani kuna maendeleo hapo? ikiwa wezi wanajulikana lakini wapo tu tafsiri yake nini? kwa hiyo mwanangu kuna makosa upande wa serikali. na nikwambie kitu kimoja, nchi hii ina maendeleo makubwa sana ya kinadharia na si vitendo na muonekano.rais yupo na anafanya kazi lakini anaangushwa na safu ya ushambuliaji. mawaziri wake namaanisha.kuna makosa aliyafanya mwanzo wakati anaingia madarakani na ndo maana matatizo hayaishi.amekuwa mtu wa fadhila sana.

  edson:duh! nimekuelewa baba na vipi upande wa wananchi wao nao wanachangia vip umasikini wa nchi?

  baba: sasa ni hivi, nisikilize vizuri edson, you are who you are because of the decision you have made! watanzania wengi tunaridhika mapema sana, na mara nyingi tunasubiri serikali itusaidie, hatujiwekei ziada, kila tunachopata tunatumia yaani kama ninilivyokwambia siku ile nipo huko, wengi wetu tuna tabia za wawindaji. hivi nikuulize swali we mtoto;

  edson:uliza baba.

  baba: ulishawahi kuona kijiji au hata wilaya au mkoa wana ardhi nzuri lakini hawataki kufanya kazi? wapo tu wanasubiri mahindi ya serikali ili wapate chakula? .hata kuanya kazi zingine mbali na kilimo?

  edson: sijawahi kuona au kusikia, labda tu kuna mikoa flani huwa haina mvua za kutosha

  baba; no, sizungumzii wingi wa mvua hapa. nasema watu. yapo maeneo huku watu wake wako hivyo.

  edson: lakini baba....

  baba: swali lingine nakuuliza.

  edson: ehe uliza tu.

  baba: umewahi kujiuliza ni kwa nini watanzania wengi wa store za mkaa na si store za chakula?

  edson: hahahahaha baba bwana!

  baba: usifikiri ni utani wala kichekesho. kwa hiyo ni lazima kila mmoja kwa nafasi yake afanye kazi kwa bidii na maarifa na .lakini pia hekima inahitajika wakati unafanya kazi, unajua mwanangu edson....

  edson: ndio baba,

  baba: mimi baba yako nimeona watu wengi wanahangaika na maisha, tena sana.toka wakati ule niko kijana mpaka leo nimezeeka na wengine ni wacha Mungu sana. unapofanya kazi lazima uwe na hekima flani,nimekueleza tabia za muwindaji,anashinda porini siku nzima anafukuza swala, akirudi nyumba anarudi na swala mmoja begani na kibaya zaidi anamuua na kumla,kesho tena huyo porini kuwinda.edson hard work is good, but hard work without wisdom can be punishment for your life!!!. uwe mcha Mungu au la lazima ujue hilo

  edson. baba nimekuelewa vizuri.

  baba.fanya kazi na ipende kazi yako tatizo kubwa la vijana wengi ukimuuliza unafanya kazi wapi, anakujibu,'' nimejishikiza kwenye kampuni hii...
  sasa ukishaona mtu wa namna hiyo maana yake ni kwamba kuna kazi alikuwa anataka afanye amabayo ameshindwa kuipata labda kwa sababu ya kiwango cha elimu, sasa amepata kazi hii inampa kuishi lakini haithamini na kusema ''NIMEJISHIKIZA''.. pamoja na mipango ya nchi wananchi pia wananch tuna wajibu mkubwa.

  edson.nimekupata baba

  bab: hebu subiri kidogo usikate simu naomba niweke simu kwenye chaji maana naona imebaki baa moja.subiri niingie ndani,


  edson: ok baba..

  baba: hallo edson upo, tayari nimeshaweka:

  edson; nipo baba. ehe baba zile dawa ulizotoka nazo huku umezitumia?

  baba: nimezitumia, na jana nimeenda hospitali sukari imeshuka sana, naona zinasaidia, nashukuru sana mwanangu.

  edson: sasa kuna zingine nitazituma dar then kaka nae atazituma huko nyumbani.

  baba: hakuna shida nashukuruni sana wanangu.

  edson; asante mzee, mama ameshatoka kuwapa kuku maji?

  baba: ameshatoka, ila naona yuko nje hapo anaongea na binti wa kazi.

  edson: basi baba mi nashukuru sana kwa maongezi haya ila lengo lilikuwa ni kujua kama mlifika salama, wasalimie wote huko nyumbani ndugu na jamaa wote na marafiki.

  baba: sawa nasi tunashukuru sana, kikubwa nakuomba ukazane na masomo yako. kikubwa nakuomba umlee huyo mtoto vizuri aongezeke kimo na hekima, pia muishi vizuri na watu huko. mpende mkeo. jioni njema

  edson: edson asante baba kwa yote ulonambia leo. ila huku ndo kwanza saa saba mchana,

  baba.haya bwana jografia ilishahama kichwani. asante sana na Mungu awabariki
   
  Last edited: Jul 21, 2009
Loading...