Wote tumesema kuhusu Tundu Lissu lakini kwa huu wimbo wa Aslay katuzidi!

mijizi minafiki inataka kutudanganya ina machungu na Tanzania ilihali inatumia mtutu wa bunduki kuuwa wasema ukweli halikubaliki hata kidogo amazao amazetu!!
 
Kwenye wimbo wa dogo Aslay kuna maneno haya!

Lissu Get well soon!
kuna watu bwana eti wasiojulikana,
Wazalendo raha hatuna,
Tanzania amani hakuna,
wasidhani sisi ni wajinga sana,
kwa hili tunaumia roho zetu,
kwani lisu lipi baya alilofanya,
Mbona mwaharibu taifa letu,

Mwambieni ama zake ama zetu,
tutakufa nae

Mwambieni ama zake ama zetu,
tutakufa naye.

Sababu yake amani hakuna,
Ama zake ama zetu,
tutakufa naye.

Yalianzia kibiti Pwani,
na kutekana watu jamani,
siyo kama raia hatuoni,
kwa Lissu mmetugusa moyoni,


Nini chanzo bwana au ni kusema ukweli,
wasidhani sisi ni wajinga sana,
kwa hili tunaumia roho zetu,
kwani Lisu lipi baya alilofanya,
Mbona mwaharibu taifa letu?

Mwambieni ama zake ama zetu,
tutakufa naye,

Mwambieni ama zake ama zetu,
tutakufa naye.

Kwa sababu yake amani hatuna!

akiamka atafarijika sana ................ nimejikuta machozi yananitoka get well LISSU
 
Tunampongeza Dogo Aslay kwa Kuzunguka katika Kampeni za Mama Samia Nchi nzima. Ni mwanachama mzuri wa CCM.
KWAHIYO AKIWA CCM HARUHUSIWI KUMFARIJI MTANZANIA MWENZAKE ? AKILI ZA CCM ZIMEJAA FUNZA NA MNACHOTENGENEZA NI HIKI CHUKI BAINA YETU NIKIANGALIA JINSI WATANZANIA WANAFURAHIA HAYA MAMBO YA ALBADILI NAPATA PICHA KIWANGO CHA CHUKI KIMEFIKIA
UJAZOO GANI
 
Bonge la wimbo!
Message delivered..
Hata wale wanaojifanya watu wa really life (Hip Hop) kwa situation ya sasa, siwaoni wakiandika nyimbo za messages kama hizi.
 
Nimesha u - download wimbo tayari na unaunguruma repeatedly ktk gari yangu kila ninapotembea....

Nimeshachangia matibabu 15,000 na hii 20,000 naituma tena huko...!!

Asante
Peopleoooooooosssss, tunataka makamanda wa ukweli. Jf hata jero tuchangie mimi niechanga kidogo nikiongeza nitataja kwa sasa naona noma.
 
Peopleoooooooosssss, tunataka makamanda wa ukweli. Jf hata jero tuchangie mimi niechanga kidogo nikiongeza nitataja kwa sasa naona noma.
......ya umma/watuuu...!!

.....kwa maana ya "nguvuuuu 'pipozzz'........"

......kila la kheri mkuu na hata kama ni 1,00 tu, wewe changia... usihofu

Kama watu 1,000,000 tutachangia Tshs. 1,00 tu kila mmoja, maana yake zitapatikana Tshs. 100,000,000....!!!!

Kwa hiyo tusiidharau nguvu ya mia moja a. k. a "jiti"....
 
Back
Top Bottom