Wote tukiamua kutanua mbavu zetu wanyonge watabaki salama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wote tukiamua kutanua mbavu zetu wanyonge watabaki salama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 24, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ile dhana ya kukiita CCM Chama Cha Majambazi inaonekana sasa inataka kuaminika mbele ya jamii hususani chaguzi zao na aina ya viongozi ambao wamechaguliwa kama dira ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.Miongoni mwa ahadi za wagombea wake hasa mkoani Shinyanga ni kuhakikisha wanaifutilia mbali CHADEMA.

  Miongoni mwa viongozi wake ambao ni wajumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya zao hawana sifa za kuwa viongozi kutokana na historia chafu ya maisha yao.Miongoni mwao wapo wezi wa magari,matapeli wa kutupwa ambao kwasasa wamesimama kwenye mwamvuli wa ukandarasi na wamiliki wa viwanda.

  Sasa ile dhana aliyoizungumza hayati Horace Kolimba kuwa chama kimepoteza dira na mwelekeo ndiyo imezidi kujikithirisha na kuruhusu dhana nzima ya chama cha majambazi kushika hatamu.Rais ana jua nini kinachoendelea kupitia TISS,lakini tunashindwa kujua kama ni mkakati wake wa makusudi kukiacha chama kikiwa taabani.

  Lakini kauli hii inatokana na machafuko ambayo yanaendelea katika harakati za uchaguzi wa madiwani ambazo zinategemewa kufanyika nchini tarehe 28/10/2012.Machafuko haya ni pamoja na kupigwa mshale M/kiti wa Mtaa wa Mwawaza kupitia CDM ambaye yupo ICU wakijaribu kuokoa maisha yake.Tukio hilo lina husishwa moja kwa moja na CCM kutokana na kukodi vijana ambao wamekuwa wakiwashambulia wafuasi wa CDM kila wanapotoka kwenye kampeni,pia taarifa hizo zimekuwa zikilalamikiwa na uongozi wa wilaya na mkoa wa CDM kwenye vyombo vya dola bila kupata msaada wowote.

  Siasa za mkoa huu zimekuwa tete kutokana na vitisho vinavyoendelea kutolewa na wafuasi wa CCM huku mjumbe wa NEC aliyechaguliwa hivi karibuni ambaye ni mkurugenzi wa GAKI INVESTMENT LTD kumshambulia mkurugenzi wa ulinzi na usalama taifa wa CDM mh.A Rwekatare pasi na sababu za msingi,tukio ambalo limetokea leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

  Tukio hilo lilisababishwa na mh. Gasper Kileo (GAKI) Kuwazuia waandishi wa habari kuwapiga picha wafuasi wa CDM ambao walikuwa wamekusanyika hospitalini hapo wakifuatilia hali ya M/kiti wao wa serikali ya mtaa ambaye aliyejeruhiwa kwa kutumia mkuki.Mh. A Rwekatare aliripoti tukio hilo la kupigwa kibao kituo cha polisi na polisi kumwita bwn Gasper kileo kumchukua maelezo na kisha kumuachia.Matukio yote haya mawili yamewafedhehesha sana wakazi wa manispaa hii na kuishangaa sana serikali kushindwa kusimamia amani na usalama wa wananchi wake,kiasi cha kuruhusu viongozi wa CCM kujichukulia sheria mkononi.
   
Loading...