Wote mnaotudhihaki wanaume tunaoangalia SULTAN mna wivu tu na wenye nazo

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,145
11,183
Niliona uzi humu kuwa mwanaume unaanzaje kuangalia Sultan kama sio tabia za kike, ikanibidi nicheke kwanza na kumuona yule aliyeleta ule uzi na waliokuwa wanamsupport hawana akili timamu na wanaonekana ndio wale wanaume wa startimes wenye maisha magumu
margarit_bondareva-20190210-0001.jpeg

Sultan ni tamthilia inayomuelezea mfalme wa Himaya ya ottoham aliyewahi kutawala miaka ya 1522-1577, na kitaka tamthilia hii kitu kikubwa kichofundisha hasa jamii za kiafrika ni uzuri na hatari ya mwanamke katika ndoa kama usipokuwa makini.

Katika tamthilia hii inamuonyesha mwanamke hatari na mwenye ushawishi mkubwa Hurrem Sultan ambae alisababisha mgogoro mkubwa katika familia ya mfalme Sultan the magnificent kipindi hicho, Hurem Sultan aliweza kupandikiza chuki kwa maslahi ya wanae
turkeyplus-20190210-0001.jpeg


Mwisho wa siku familia ilitawanyika Wakaanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya sumu aliyoimwaga Hirem, Mfalma Sultan akamuuwa mwanae wa kumzaa ambae elizaa na mwanamke mwingine, Shahazad Mustafa kwa kumnyonga kwa kamba, pia mfalme akampoteza mwanae Shahazad Mehemet ambae aliuwawa sababu ya Chuki, mfalme pia akamuuwa dada yake Khadija Sultan kwa sumu sabubu ya chiki iliyopandikizwa na mkewe Hurrem

So tukija kwenye familia za kibongo wanaume mnaoendeshwa na wake zenu hadi kufikia hatua ya kutelekeza ndugu zenu hadi kuuwa mpo wengi tu, wanaume mabushoke mnaosikiliza wake zenu kwa kila mnachoambiwa na kujenga chuki kwa ndugu zenu mpo wengi gumu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom