Wote mlio omba mikopo kutoka heslb tafadhali angalia hapa mpyaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wote mlio omba mikopo kutoka heslb tafadhali angalia hapa mpyaa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MKINDE, Sep 4, 2012.

 1. M

  MKINDE Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  HABARI ZENU WANAJAMII WENZANGU….

  Naombeni nafasi nami niwasilishe hoja hii ndani ya jukwaa hili la elimu lenye heshima kubwa…..
  Leo nilikuwa maeneo ya ofisi za TCU hapa jijini Dar es Salaam, nilikuwa najaribu kudodosa dodosa kulikoni mbona kimya kimetanda kuhusu hawa wenzetu ambao waliomba second selection na wengine kuandikiwa wamechaguliwa chuo fulani ila unapoingia kwenye chuo husika hukuti jina, wahusika majibu waliyokuwa wakitupa ni kwamba tuwe wavumilivu kila kitu kitakuwa kwenye mtandao hivi karibuni…..
  Wanafunzi ambao walikuwa ofisini hapo hawakukubaliana na majibu hayo ndipo ikatokea kama songombingo la aina yake baada ya hapo muhusika alituliza vurugu zilizotaka kutokea na ndipo mwanafunzi mmoja wa chuo cha Mount Meru ambaye alichaguliwa second selection alipotaka kujua zaidi suala hili majibu yalibaki yale yale ya kuwa wavumilivu ila muhusika alichosema ni kwamba kwa wale ambao vyuo vyao vinafunguliwa mwezi huu wa tisa waende wasiwe na hofu kwani taarifa zao zimeshafikishwa katika vyuo husika walivyo omba na kukubaliwa hapa ndipo mwanafunzi mwingine alipotaka kujua zaidi kuhusu mikopo huku akiwa na jazba na muhusika naye akajibu huku akiwa na jazba akasema kwamba : MLIOMBA MIKOPO WOTE MTAPATA IWAPO TU KWENYE COURSE ULIYOOMBEA MKOPO ILIRUHUSU WEWE UPATE MKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU NA KIWANGO CHA MKOPO PIA KINAPATIKANA KWENYE KILE KITABU CHA TCU AMBACHO KIMEONESHA KILA COURSE NA KIWANGO CHA MKOPO KINACHOTAKIWA KULIPWA NA HESLB NA SI VINGINEVYO… hivyo aliwashauri wote ambao wanatakiwa kuanza chuo mapema mwezi huu waende kama ratiba ya chuo husika itakavyoeleza kuhusu maelekezo mengine watapewa watakapo fika huko chuoni waliko chaguliwa….
  Baada ya hapo nilijiongeza nikajiuliza inamaana majina kutoka HESLB ndio hayototoka tena au hii kauli ya muhusika ina maana gani….Ndipo nilipo ianza safari ya kwenda ofisi za HESLB ili kupata dodoso za mikopo yetu,, majibu niliyopata kutoka katika ofisi za HESLB ni kwamba iwapo TCU watatoa majina ya waliopata vyuo RASMI basi nao hawatokuwa na pingamizi kutoa majina ya wanafunzi waliopata mkopo… Niliona labda hawaelewi kama kuhusu TCU wao wamesha toa majina ya wanafunzi ambao wamepata vyuo, nilipo mkumbusha hilo nae akaniuliza hizo taarifa nimezipata wapi? Nikamjibu zipo kwenye profile zetu ambazo tuliombea vyuo.. Nae akanijibu hiyo siyo RASMI , RASMI WANAYOITAKA HAPA NI KWAMBA LAZIMA HAYO MAJINA YAONEKANE KWENYE WEBSITE YA TCU HIVYO HANA JIBU LINGINE ZAIDI YA HAPO….
  Mzee wa dodoso nikaishia hapo hivyo tuendelee kuwa wavumilivu kuhusu HESLB na kuhusu hawa wenzetu ambao wanatakiwa kwenda chuo mwezi huu ushauri wangu ni kwamba kama umejipanga kidogo kiuchumi we nenda tu kwenye chuo husika angalau wakuone wasije wakajua umegoma bure kasha wakakufuta kwenye chaguzi zao wengine tupige goti tusali baba HESLB acheke mapema maana tumejitahidi kumchekesha lakini bado tu amenuna….
  ***********************ASANTENA WANA JF*******************
   
 2. F

  Freeman Patrick Senior Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha ha ha... Mzee wa dodoso, kwa hiyo wale ambao majina yao hayapo kwenye web ya chuo nikwamba taarifa zao zilikuwa hazijapelekwa au?
   
 3. d

  dev senior JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  duuu sa hapo ndo balaaa!!HESLB wanasubr TCU wakati zimebakia wiki2 tu vyuo vingine kufunguliwa???eeeh!eeeeeh!SHULE MWAKA HUU ITAWASHINDA WENGI
   
 4. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Umefanya kazi nzuri mkuu,ila sidhani kama hawa HESLB kweli watasubiri kama TCU walivyo kuambia.Mimi ninamatumaini makubwa kwamba,wiki hii mambo yatakuwa out muda wowote. Hata hivyo ngoja tuone leo kwasababu Pokofame alisema,ankoake alimwambia yatatoka leo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  yule jamaa hamna kitu pale kila saa ana turusha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. K

  Kibulu Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da! Mimi kinachonitatanisha ni kwamba St.AUGUSTINE tunatakiwa kwenda kufanya registration tarehe14 ths manth, ktk join instruction yao wamesema kdogo mkataba na bodi hawaufikirii sana ila uende na atleast robo3 ya fee. Ila mkopo ukitoka pia pale naskia huwa shida sana kuupata kama umeshalipa hyo fees.sasa tutaenda kuishi vp?
   
 7. A

  Arnold Ndosi Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mzee Wa Dodoso,ina Maana Wale Waliochaguliwa Course Ambazo Ni Non Priority Hawapati Mkopo?.mimi Nilichagua Education,mlimani,duce,na Mzumbe.pia Nikachagua Education Katika Lugha Mzumbe.coz Za Tofaut Na Ualimu Ni Mas com Na Tourism& Cultural Heritage.wamenichagua Mascom Mlimani Licha Ya Kuiweka Ya Nne.sasa Wakininyma Mkopo Mimi Nina Makosa Gani.dah,siweze Kusoma Maana Means Testing......ni Noma!
   
 8. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  ngoja tuone,isipokuwa kweli itabidi jamaa aombe radhi,la sivyo aondoke JF.
   
 9. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  MNA MAWENGE SANA TATIZO LENU msiwe ivo bwana kama TCU wamekuchagua chuo fulani we angalia tarehe ya kufungua chuo then nenda nina uhakika hauwezi kataliwa
   
 10. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hapo mkopo kupata ni ndoto mwombe mungu sana ni ushauri tu
   
 11. A

  Apex JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 429
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Then ndo kunambia non-priority imeshakula?!!! helsb twakuomba utukumbuke sote lasivyo utatupoteza weng sana na laana zetu zitakufuata popote pale uendapo,pls tukumbuke sote ni wa tz tupeni haki ya kuzitumia kodi zetu kwa maendeleo yetu na taifa hili changa.
   
 12. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  haya bwana inamaana wanawangojea tcu?? kwel hapa kazi ipo!!!
   
 13. M

  MICHO THOMAS BK Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanana jamii fr. Mimi nashauri kama wakuu wa heslb wanatembelea hz forum ya kwamba wakifanya makosa wakatoa mkopo kwa watu wa course za priorty tu! Kiukwel kutakuwa hakuna maana ya kuwa na hz taasisi na serikal kwa ujumla.Nasema hv kwa uchungu kabisa itakuwaje mtoto wa Mkulima achague kozi ya kwanza ya Priority kwa ajil ya ili angalau asaidiwe japo haipendi ile kozi, TCU wamchague kozi ya mwisho tena asipewe mkopo hv kwel huyo mtu atasoma? Na tatizo ni kwa yeye au serikal, je kama wewe kiongoz hiyo si itakuwa dhambi kubwa kama huyu maskin atashindwa kwenda chuo? ANGALIZO: Mkiamua kufanya hv jua ya kuwa hao ndo wapiga kula 2015 jipange.
   
 14. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  ​mi nakuunga mkono...ngoja hii siku ya leo ipite!!! alisema j3,ikafika akasema tena j5....ngoja ipite!!! tena sijui yuko wap **** sana huyu jamaa...
   
 15. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kudadeki mleta mada unaona muda unazidi yoyoma?? huyo ndugu yako na wewe wote hamna kitu!
   
 16. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nilisema mleta mada hamnazo mkichwa.
   
 17. A

  Awadh Mabaraza Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah kweli TZ hakuna maisha bali maigizo. Inamaana hawa TCU wamepeleka majina vyuon kabla ya HELSB? Na je hawa wanafunz wanaotegemea mkopo ndo waende chuo watafanyaje? Kuna ambao wanategemea kuahrisha chuo wakikosa mkopo 2waweke kundi gani? Jaman jaman HELSB fanyen kaz kam taasisi cyo kama familia. Binafc nitawaheshmu nakuona mnajua kazi yenu kama mtatoa cku tano kabla ya kufunguliw kw chuo cha kwanza.. Ndugu zangu 2we wavumilivu hayo ndo maisha 2liyoyachagua
   
 18. M

  MKINDE Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kutokana na kauli za muhusika pale ofisi za TCU kuna uwezekano tusipewe mkopo wale tulioandikiwa Non Priority maana ile kauli kidogo ilichanganya wengi. Tuombe mungu HESLB wasomeke mapemaaa
   
 19. M

  MKINDE Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mzee wa dodoso bado nipo kwenye jukwaa na sitegemei kushuka jukwaani kwa kuogopa vitisho kutoka kwa baadhi ya wadau wa jukwaa hili. Kesho Mungu akipenda nitapanda jukwaani na mada nyingine ikiwa ni mwendelezo wa hii kabla sijaondoka hapa jijini Dar es salaam. ASANTENI NDUGU ZANGU
   
 20. p_prezdaa

  p_prezdaa JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  ''mliomba mikopo wote mtapata iwapo tu kwenye course uliyoombea mkopo iliruhusu wewe upate mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu na kiwango cha mkopo pia kinapatikana kwenye kile kitabu cha tcu ambacho kimeonesha kila course na kiwango cha mkopo kinachotakiwa kulipwa na heslb na si vinginevyo…''
   
Loading...