Wosia.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wosia....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Dec 20, 2010.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]...bANDUGU wAPENZI...

  Kila tunapokaribia mwisho wa mwaka, ajali na vifo huwa ni kama hitimisho la mwaka. Hebu tukumbushane yaliyo muhimu, sio kila siku kusifia Infidelity tu, roho ikiacha mwili tunawaachia wafiwa kivumbi.

  Hivi, kuna umuhimu katika wosia kuwataja watoto ulokuwa umemficha mwandani wako? au ndio potelea mbali, watajuana wenyewe?

  Sio siri, wapo kina dada waliozaa enzi za sekondari, watoto wakarithiwa na bibi bila mume kujua mpaka kifo kilipotenganisha, ...kama ilivyo kwa wanaume waliozalisha na kuficha watoto mpaka siku ya msiba, ndipo kijana au binti alipoletwa.

  Kwa mtizamo wako na itavyokugusa habari hii, nini unaona ni nafuu kwako. Kuujua Ukweli toka kwa wosia wa marehemu mke/mume? au bora ya kitendawili anachofukiwa nacho -hakuona haja ya kukwambia?
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  kweli haya yanatokea sana...
  hata mimi nilizani tu watatu kwenye familia yetu ..
  mapaka nilipo mpoteza mzazi wangu mmoja ndo tukajua tuko watano..

  kwa kweli unauma sana miaka 20 na kitu unadhani we ndo wa kwanza au we ndo wa mwisho lakini sio...
  na cha kushangaza zaidi ni pale yule ambaye mlikuwa hamumjui ndo kafanana fika na mzazi...

  kwa kweli mi naona ni bora mtu aseme tu kabla kifo hakija mkuta...
  kwa mimi naona ni borea ka unawajua ndugu zako wote....

  haya matatitoza yanaweza kuwa mkubwa zaidi baadaye pale ndugu wanapokutana halafu hawajuani....
  ni damu yako hata ukikataa kwa hiyo ningependa kusema jamani hakikisha watoto wako wote wanajuana...
  ile ya mtu anakuja kwenye mazishi halafu anasema mi ni kaka au dada yako ni mbaya sana.
  hujui sasa uliye au ucheke..
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...dah, pole sana afrodenzi.
  kuna msemo 'mficha maradhi, kilio kitamuumbua...'
  siku ya msiba badala watu kuomboleza, panageuka sehemu ya kustaajabiana.

  Na akishajitokeza mmoja, mnabakia na wasiwasi huenda kuna mwingine ataibuka pia...
  Misibani kuna vituko, acheni tu.
   
 4. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Naomba kueleweshwa kitu hapa... Mbu plz...

  Wosia... Lazima uandikwe na Baba tu? Mama katika hili suala na masuala mengine (kwa mfano Mama anakuwa amejenga majumba au Miradi ambayo Mume haijui, au ana watoto ambao alizaa kabla) hatakiwi kiandika wosia?

  Ni vizuri watoto wakifahamiana, unaweza kukuta hawajuani na mwisho wa siku wakawa wachumba... Bora uondoe fedheha...

   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama watoto hawajulikani ndani ya ndoa, ni hatari sana kuwataja kwenye usia, utakuwa unaleta ugomvi usiomithilika, na kwa binafsi yangu hata ukiwaandikaje kwenye wosia wako hawapati hata mia ya urithi...Maliza kesi mapema watambulishe watoto wako kwa mkeo, na mbele ya wanandugu, then uwaaandike kwenye wosia!
   
 6. RR

  RR JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Hivi mali zilizochumwa kwa pamoja katika ndoa....nani mwenye mamlaka ya kuziweka katika wosia??? Mke au mme???? Mke ana nafasi gani katika wosia/mirathi ya mme....?
   
 7. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  ni kweli kabisa afro yaani wazazi sijui huwa wanawaza nini ni bora watu mjuane kabisa sio kustukizana siku ya msiba na kuanza kugombani sijui kijumba alichoacha mzazi. Hilo la kufanana mara nyingi watoto wa nje huwa wanafanana sana na baba sijui kwa nini, mimi mwenyewe nasikia baba ana watoto wawili huko nje tena wakubwa lakini hajawahi hata kutuonyesha na nasikia ndio wamefanana haifai mimi naona bora ijulikane tu mapema na watoto wajuane
   
 8. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135


  mh! hii naona itaanza kuleta mkanganyiko maana zamani baba ndio alikua kila kitu anafanya kazi yeye na mali zote zilikua zake sasa siku hizi wote mnafanya kazi wote labda mmechangia kujenga nyumba etc. sasa kama baba ana watoto wa nje sijui ndio watapata urithi ama? hii ni ngumu kidogo. Mimi naona tuwafunze watoto kutafuta mali zao wenyewe na wasiwe na mawazo ya kurithi mali za mzazi, mpe mtoto elimu nzuri, mfundishe maadili mema hata hao watoto wenu wa nje wapeni elimu nzuri hata kama kutakua na ambae si msikivu labda anaweza kuwa mmoja tu na hata mzazi akifa wale wengine waliojitafutia mali watamuachia tu kwani wanazo zao hii itapunguza watoto kugombania mali ambazo hata hawajui zimepatikanaje
   
 9. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #9
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  yaani mi nakwambia ni balaa tu halafu huyo mtoto wa nje ni mkubwa tu
  na ye anawatoto wawili.. yaani wajukuu..
  eti mi shangazi ambaye hata nilikuwa sijui ..
  kwa kweli lakini utafanyeje..
  ambaye unataka kumuuliza haya maswali mazito uliyonayo moyoni ndo kasha toweka hivyo..
  mpaka mkutane tena kwemye makao mapya..
  kwa hiyo sisi nikupendana tu nakusaidiana sasa...( kwani haya si makosa yao kabisa)
  haina tena maana ya kugombana....
  Yaani kilicho bakia ni kumwomba Mwenyezi Mungu atusaidie tu ...
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mbu:

  Sisi kwetu tumezaliwa 34, sasa sijui "Will" itaandikwaje? Wote tunafahamiana na Mama zetu wote wapo!
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  yaani mi nakwambia saa nyingine wazazi hawatendei haki watotot wao..
  sijui wanavyokaataa inamaanisha nini..... yaani mambo yakiuupuzi kama haya yananiudhi sana..
  sisi tumesha kuwa ni watu wazima sasa.... tunatakiwa tuelezwe kila kitu kuhusu familia zetu..
  yaani Maty mwaya mi nakuomba sana uwajue hao ndugu zako watafute mwenyewe..
  yasije yakakukuta yaliyotukuta sisi..
  usikute na we ni shangazi ambaye hujijui kama mimi hapa..
  au mshike shati baba mpaka akwambie..
  Pole sana mwaya... na usijali kama kweli ni ndugu zako utawajua tu damu ni nzito kuliko maji...
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Unaandika mali a+b+c gawanya kwa 34 ndo urithi kila mtu....jinsi ya kugawa mtajua...
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa ninavyoelewa usia lazima uandikwe/utamkwe na baba/mume na mama/mke. Wote tuna haki sawa.

  ...PJ, kimila na kiserikali ikithibitika watoto ni wa marehemu, wanahaki ya kupata sehemu ya urithi. Watapata wanachostahili.

  ...mnh, RR hiyo inategemeana zaidi na matakwa ya marehemu na makubaliano ya wanandugu, ingawa kidini na kiserikali kuna miongozo yake. Si vibaya tukakumbushana tofauti ya Wasia (wosia) na Mirathi vile vile.

  wasia nm maagizoya mtu kwa watu wakeambayo anataka yatimizwe iwapo atakufa au kuondoka; usia.

  mirathi nm 1 vitu na mali yanayoachwa na mtu aliyekufa na kupewa watu wakekwa mujibu wa mipango maalumu

  ...kweli kabisa Maty, no wonder wazazi tunashurutishwa urithi muhimu kwa watoto ni ELIMU!

  ...Baba Enock, madhali wote mnafahamiana na kwa idadi, hakuna kilicho kigumu kwenye kugawana mirathi iwapo Urithi utajumuishwa kwenye usia/wasia. Kumbuka, Usia ni mwongozo tu.
   
Loading...