Wosia wangu ‘ Maalum ‘ kwa Wanaume wote kuwa tuache ‘ Kuwaongopea ‘ Wanawake pale tukiwa ‘ tunawatongoza ‘ kwani yamenikuta!

Kwa taarifa tu ni kwamba ukiona leo hii unamtongoza Binti / Mwanamke halafu anakuambia kuwa mpe siku tatu akufikirie usidhani kwamba labda anakufikiria kweli bali wengi wao huwa ama wanaenda kwa Waganga wa Kienyeji au wanawatafuta wale Binadamu wenzetu wenye tabia ya Kupandisha ‘ Mashetani / Viti ‘ ili wawaulize kama Sisi tunaowatongoza ni Watu wakweli na sahihi Kwao.

Kama kawaida yangu ya ‘ Kuwadanganya ‘ hivi Viumbe vya Kike kuna mmoja nilimtongoza hivi majuzi na mwenyewe nikawa ‘ najifaragua ‘ kwa ‘ mikogo ‘ yote kuwa mambo yangu ni ‘ poa ‘ Kimaisha ( wakati Kiuhalisia ni Choka Mbaya wa Kutukuka kabisa ) na nikamwambia kuwa namiliki Gari aina ya HAMMER na pia naishi Masaki karibia na Sea Cliff yote hii ili mradi tu nimpate na niweze ‘ Kumchapa ‘ nao.

Baada ya Kumtongoza vile kama kawaida yao akaniambia nimpe siku tatu atanipa majibu yangu na siku yenyewe ikafika ambayo ni leo. Kwanza ‘advertise ‘lake la Kwanza tu Kwangu huyu Dada alinitaka nikamwonyeshe hiyo Gari yangu aina ya HAMMER ili akaione kwani na Baba yake mdogo nae anataka Kununua kama hiyo.

Bado hata sijakaa sawa ( huku nikiwaza kuwa Mwanamume leo nimeumbuka utamu ) akaja na ‘ advertise ‘ la uhakika ambapo aliniuliza tena kuwa nakaa Masaki sehemu gani nami kwa ‘ Upopoma ‘ wangu bila kujua kuwa alikuwa ‘ ananitega ‘ nikamwelekeza kuwa ni karibia na Sea Cliff nyumba namba Fulani nae akaniuliza nina uhakika nikamwambia ndiyo kumbe hiyo Nyumba niliyomtajia anakaa ‘ Shangazi ‘ yake na muda mfupi tu uliopita alikuwa ametokea huko.

Huku Jasho la aibu na kuumbuka likiwa linanitiririka na linaniserereka kunako Mwili wangu ndipo huyu Mwanamke ‘ akanipasulia ‘ Siri ambayo nilikuwa siijui kuwa ile siku ambayo nilimtongoza tu alienda Buguruni kwa Mjomba wake ambaye ni Mganga wa Jadi na hapo hapo tena ana hayo ‘ Mashetani ‘ tena makali sana ndipo yalipopandisha tu yakamwambia kuwa si tu kwamba sina hiyo HAMMER bali hata Toroli tu sina na kuhusu ninapoishi akaambiwa kuwa naishi Mbagala kwa Madenge tena ‘ Uswahilini ‘ kabisa na ilipo Kambi ya Wachawi vile vile.

Kuanzia sasa nitakuwa mkweli na Mhalisia kabisa pale nikiwa ‘ nawatongoza ‘ Watoto na nimekoma! Haya na Wale Wanaume wenzangu ‘ Mapacha wa Uwongo ‘ tukiwa tunatongoza nadhani kwa kilichonikuta Mwenzenu nanyi pia Kitawafunza na mtaungana name kuwa sasa tutakuwa wakweli daima ili tuweze kuwafurahisha na kuonyesha Heshima kwa hawa Dada zetu / Wapendwa wetu.

Nawasilisha.
Aisee
Kwanza,Nikupe pole mkuu
Pili hongera kwa kuamua kuanza kuwa mkweli
 
Back
Top Bottom