Wosia wa Liyumba: Msionyeshe sura yangu kwa umma

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
MERITO Liyumba, mdogo wa marehemu, Amatus Liyumba, amesema kaka yake kabla ya kufikwa na umauti Aprili 18, mwaka huu, aliacha wosia kuwa atakapofariki dunia, mwili wake utazamwe na ndugu zake peke yao.

Wosia huo wa Liyumba, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu Tanzania (BoT), ulifanya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wake, kutopewa fursa ya kuona sura yake kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.

Ndugu huyo alitangaza utaratibu huo jana baada ya ndugu, jamaa na marafiki kufika nyumbani kwa marehemu kutoa heshima za mwisho.

Baada ya mwili kuwasili na taratibu nyingine kufanyika, Merito alisimama na kutangaza kuwa kaka yake aliacha wosia kwamba wakati wa kuagwa, ndugu pekee ndiyo wamtazame uso wake.

“Alisema watu wengine watakaoshiriki msiba wake, wapite kwenye jeneza lake likiwa limefunikwa,” alifafanua.

Baada ya utaratibu huo kutangazwa, waliofika kuaga walipita mbele ya jeneza hilo likiwa limefungwa na kutoa heshima zao za mwisho.

Aidha, alisema kutokana na taratibu za kimila, mwili huo ambao jana ulitangazwa utazikwa leo mkoani Morogoro, utaratibu umebadilika na kwamba atazikwa kesho.

“Mila zinasema mwili wa marehemu baada ya kuwasili Morogoro, unatakiwa kulala kwenye nyumba yake hadi siku inayofuata ndipo utaratibu mwingine wa maziko ufanyike. Kwa hiyo atazikwa Ijumaa (kesho),” alisema.

Miongoni mwa walioshiriki kwenye msiba huo ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa BoT.

Liyumba ameacha watoto saba, mkewe alifariki dunia miaka 10 iliyopita.

Enzi za uhai wake, alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2009 kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na kuisababaishia serikali hasara ya Sh. bilioni 221.

Hata hivyo, alishinda kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha tuhuma hizo.


Chanzo: Nipashe
 
Labda alikuwa na madhambi yake ndio maana hakupenda kutazamwa?

Hivi huu utamaduni wa Kutazama mwili wa Marehemu umeasisiwa na nani?
 
Tutaamini vipi kama amefariki.isije ikawa kama ya balali.Ila poa tu,laana za watz zikizidi mwisho huwa ni mauti
 
Hii tabia sio ya kistaarabu ya kufuata watu vyumbani na kuanza kuwapiga picha kama hivi, hapa hakuna maadili ya utu wa mtu, ni bora wapenda picha mkatafuta namna nyingine na sio hii ya kufuatana vyumbani, kuna mjinga mmoja anaitwa sam mahela wa itv aliingia ikulu kidogo aingie chumbani kwa rais kupiga picha. Ifike sehemu tuheshimiane.

3X6A4124.jpg
 
one bright Morning when man life is over Man will fly from hope to zion.RIP

Mungu ndio ajuaye Maisha yetu baada ya hapa kwenye hii dunia ya mateso na manyanyaso.
 
Sijui wale waliopewa RAV4 walikuwepo maana ni wengi watakuwa hawakuwatendea haki.
 
Kama kusingekuwepo na utaratibu wa kuaga marehemu kwa kuuonesha mwili basi yale yaliyotokea Tanga ya kubadilishowa maiti Muhimbili yasingekuwepo.
 
Back
Top Bottom