Wosia wa baba wa taifa Mwalimu Nyerere

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Nimeona ni jambo zuri kuwa na threadi inayokumbushia hotuba za baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Tushirikishane ujumbe katika hotuba zake mbalimbali kwa manufaa ya umoja, utaifa, uhuru, maendeleo, tunu na misingi ya taifa letu.
 
Hakuna baba wa taifa.."sema Wosia wa Rais wa Kwanza wa Tanzania"

Baba unajua maana yake ina maana aliwahi kuoa wanawake wote wa Tanzania?
 
Kwa kuanzia kuna hotuba aliitoa mwaka 1979 kule Kagera baada ya vita na Amini. Katika hotuba hiyo Baba wa taifa alisema hakutaka kabisa kabisa kupigana na Amini. Aliwaomba sana marafiki wa Amini ili wamshauri Amini aache uchokozi na kuvamia nchi yetu ili kukwepa kupigana vita na Uganda. Kwa bahati mbaya ombi lake halikukubaliwa. Akasema sisi Tanzania hatukumtuma Amini kuivamia nchi yetu. Pamoja na kuwa alikuwa anawanyanyasa wananchi wa uganda Tanzania haikuthubutu kuingilia mambo ya ndani ya Uganda kwa sababu sheria za umoja wa nchi huru za Africa zilikataza kuingilia nchi nyingine. Akasema pamoja na kuwa hakumtuma Amini kutuvamia na pamoja na kuwa Nyerere hakutaka kabisa vita na Uganda, alifurahi kwa vile uchokozi wake kwa Tanzania ulituweza kumpiga na kuikomboa sehemu ya nchi yetu aliyoivamia na pia ilikuwa faida kwa Waganda waliokuwa wananyanyaswa na Amini
 
Kusije kukajirudia haya hapa Igunga tena.

chakachua_halmashauri_mwanza1.jpg
 
Hakuna baba wa taifa.."sema Wosia wa Rais wa Kwanza wa Tanzania"

Baba unajua maana yake ina maana aliwahi kuoa wanawake wote wa Tanzania?
Hakuna nchi isiyokuwa na baba wa taifa, baba ni jina la heshima kwa waanzilishi wa mataifa mbalimbali. Sisi watanzania tumekubali kumwita baba wa taifa kwa jinsi alivyoipenda nchi yetu kama baba anavyowapenda wana wake.
 
Tanzania haikuanzishwa na nyerere ilikuwepo tu

Ameipenda angeiachana kwa mafisadi (alivyompigia debe mkapa)
 
Suala lingine muhimu alilowahi kuliongea hasa kwa siasa zinavyoendeshwa alisema mwanasiasa anayefilisika kisiasa hutumia njia za kuwagawa watu kikabila, kidini n.k.
 
Back
Top Bottom